Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiagana na Wanafunzi wa Shule ya sekondari Felix Mrema Daraja la pili baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Ghorofa la Shule hiyo ambapo ameahidi kuchangia shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi huo. Makamu wa Rais amekamilisha ziara yake ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari Karona Wilayani Arusha wakati alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kukaguwa na kuzindu wa miradi ya maendele Mkoani Arusha leo,ambapo ameahidi kuchangia shilingi milioni tatu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Shule hiyo.
Mzee wa kabila la Muarusha katika kijiji cha Terrat Nadosollo Wilayani Arusha Saigura Loilola, akimvisha vazi la Mgolole la Heshima na Uongozi wa kabila la Muarusha (Masai) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipowasili kwenye uwanja wa Terrat Nadosollo Wilayani Arusha kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara. Makamu wa Rais amekamilisha ziara yake ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoni Arusha leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika vazi la Mgolole la Heshima na Uongozi la kabika la Muarusha (Masai) alilokabidhiwa na Wananchi wa Wilaya ya Arusha, alipowasili kwenye Uwanja wa kijiji cha Terrat Nadosollo kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara. Makamu wa Rais amekamilisha ziara yake ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo. Picha na Amour Nassor wa VPO.

Dk. Bilal ataka kupanga vipaumbele kukabiliana na changamoto za elimu


Na Penzi Nyamungumi – Arusha

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal amekiri kuwa sekta ya elimu inakabiliwa na changamoto nyingi lakini amesema kuna haja ya kupanga vipaumbele ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo hatua kwa hatua.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la shule ya sekondari Korona iliyoko maeneo ya Njiro nje kidogo ya mji wa Arusha Dk. Bilal alisema pamoja na kwamba changamoto zipo nyingi inabidi kukabiliana nazo moja baada ya nyingine.

“Nimesikiliza taarifa ya Mkuu wa Shule ameeleza changamoto nyingi. Sasa ni vyema ukajaribu kuainisha kipi kipewe msukumo wa kwanza katika kutekelezwa na mambo mengine baadaye, alisema Dk. Bilal na kuongeza “hatuwezi kutatua tatizo la korongo leo, hatuwezi kujenga nyumba za walimu leo, yote hayo yanahitaji maandalizi.”

Hata hivyo, alisema serikali ina mpango wa kujenga nyumba za walimu nchi nzima na kusema mpango huo utakapoanza yawezekana shule ya sekondari Korona ikawa ya kwanza kuletewa mradi huo.

“Tuna uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za elimu. Tulipoona kuna mahitaji makubwa ya shule za sekondari tumejenga, upungufu wa walimu nao tunaufanyia kazi,” alisema Makamu wa Rais na kubainisha

“Pia tuliahidi wakati wa kampeni kuwa watoto wote watapata vitabu vya masomo ya sayansi. Tayari tumeanza kwa kuwapatia wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili na ni imani yangu kuwa huo ni mwanzo vitabu vitafika kwa wanafunzi wote wa sekondari.”

Akitoa taarifa Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu John Ndewirwa alisema shule ya Korona ambayo ilifunguliwa rasmi Machi 14, mwaka huu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa maabara, maktaba, bwalo, umeme, jengo la utawala, huduma za maji ya uhakika, nyumba za walimu, bweni na gari la shule.

Aidha aliiomba serikali kufanya tathmini ya kisayansi ili kuchukua hatua za kudhibiti korongo lililo karibu na shule upande wa magharibi lisiongezeke na kuleta madhara.

Katika ziara yake wilayani Arusha ya kukagua shughuli za maendeleo Dk. Bilal aliweka mawe ya msingi jengo la ghorofa shule ya sekondari ya Felix Mrema na jengo la zahanati ya Nadosollo kata ya Terrat.

Akiwa wilayani Arusha Dk. Bilal alitoa jumla ya shilingi milioni 11, kati ya hizo milioni 5 zisaidie ujenzi wa ghorofa shule ya Felix Mrema, milioni 3 zitumike kununua samani kwa shule ya sekondari Korona na milioni 3 zilizobaki kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa zahanati Nadosollo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...