Mkuu wa kitengo cha Tanzania International Container Teminal Services (TICTS) Bw. Neviile Bisset kulia, akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, shughuli zinazofanywa na kitengo chake wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika Bandari ya Dar es salaam, sehemu ya uteremshaji Makontena kwa ajili ya kuangalia shughuli mbalimbali za utendaji kazi Bandarini hapo leo.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omar Nundu kulia, akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, baadhi ya Shughuli mbalimbali za kiutendaji wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika Bandari ya Dar es salaam leo kwa ajili ya kuangalia shughuli za utendaji kazi. Katikati Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mandari Tanzania Ephraim Ngoza Mgawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Natumaini walimweleza na procedures za mtu jinsi anavyo go through kukomboa mzigo wake katika hiyo bandari...

    ReplyDelete
  2. Inabidi pia viongozi hawa wa discuss uozo na ubadhirifu uliodumu kwa muda mrefu hapo bandarini Dar,Kero ya bandari yetu imekuwa kama ugonjwa sugu usiokuwa na dawa !!serikali zetu za awamu zote zimeshindwa kudhibiti rushwa,uzungushaji na ubabaishaji uliokithiri katka bandari yetu,kutoa mizigo au magari bandarini limekuwa tatizo kubwa kwa miaka mingi,hata kama unazo pesa keshi za kutolea mzigo wako,lazima utapitishwa kwenye mlolongo mrefu ili mradi tu utoe chochote.Tra nao waangaliwe hao ndio mafisadi wengine,ikibidi wawe wanapewa tranfer kila baada ya muda mfupi ili kuweza kudhibiti huo mtandao wao wa rushwa.Tumechoshwa na mateso ya bandarini na Tra.
    mwananchi Dsm.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli uzungushaji,ubabaishaji,kupoteza muda mwingi katka kutoa mizigo kumezidi,na mwisho baadhi ya watanzania huamua kwenda kutolea mizigo yao mombasa.Kinachotakiwa ipatikane njia ya kudumu kukomesha rushwa na mzunguuko mkubwa ambao siyo wa lazima katika kutoa mizigo kwenye bandari zetu,bila kusahau Tra,hao ndio kichocheo kikubwa cha rushwa na usumbufu,wananchi tuungane kupinga mateso na manyanyaso tunayoyapata bandarini na Tra.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...