Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakikata utepe kuzinduwa mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Ng’hungumalwa Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yaliyoadhimishwa leo Mkoani Mwanza, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni maji kwa ajili ya miji kukabiliana na changamoto mbalimbali mijini. kulia Waziri wa maji Profesa Mark Mwandosya. Jumla ya Shilingi Milioni 19 zimetumika hadi kukamilika kwa mradi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal kushoto na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa pamoja na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya, wakisukuma Pampu kupandisha maji kwenye uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Ng’hungumalwa Wilaya Kwimba Mkoani Mwanza katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yaliyoadhimishwa leo Mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Dorisia Mulashani Mhandisi wa Wizara ya maji kwa ushiriki bora katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa iliyoadhimishwa leo Mkoani Mwanza.
Afisa wa Mazingira katika mradi wa Ivemp ii Enrisha Mbwambo kushoto, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya, wadudu aina ya mbawakavu wanaotumika kwa ajili ya kuangamiza magugumaji alipotembelea mabanda ya maonesho katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yaliyoadhimishwa leo Mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Ng’hungumalwa baada ya kuzinduwa mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji hicho katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yaliyoadhimishwa leo Mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Heroshi Nakagawa katika, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki bora wa maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa iliyoadhimishwa leo Mkoani Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...