Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwapungia mkono wananchi wa kijiji cha Busisi wakati alipokuwa akiteremka kutoka kwenye kivuko cha M.V Misungwi, alipowasili katika kijiji hicho leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Geita.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kalangalala Wilayani Geita, baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya shule hiyo leo ambapo ameahidi kuchangia shilingi milioni tano kwa ajili ya kuanzisha kitengo cha mtandao wa intanet katika Shule hapo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal, akisaliomiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kalangalala Wilayani Geita

Picha na mdau Amour Nassor wa VPO




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huo ulinzi mbona umepindukia mpaka unatutia wasiwasi??

    ReplyDelete
  2. Mikausho MikaliMarch 24, 2011

    Habari Za kazi ? natumai uko salama na unaendelea vyema na ujenzi wa taifa.Kuna kitu huwa kinanikwaza na naona nipate mahali pa kutolea kwazo langu.Ni kuhusu ili suala la kupiga picha viongozi hasa wa Tanzania yetu.Naona mara kwa mara kwenye hizi picha za viongozi watu wanapiga na picha za walinzi wake (PSU).kimaadili sidhani kama ni sawa manake kazi za hawa jamaa ni nyeti na si vizuri kuwa expose kwa kila mtu ndo maana kwenye picha za viongozi wa nchi za wenzetu ni nadra sana kwa mfano kupiga picha watu wa secret service

    ReplyDelete
  3. Mdau ambaye hutaki ukwazwe na picha za walizi aka usalama wa taifa.
    Ni kwamba tanzania yetu hawa jamaa wanajiexpose wenyewe kwenye shughuli za jamaa inatakiwa wawe mbali au wqawe karibu lakini bila kujionyesha kama ni walinzi.
    Sijawahi ona Obama akiwea na mwanajeshi nyuma yake kama Kikwete

    ReplyDelete
  4. kwee kweee kwee hizo ndio sheria za nchi za ulimwengu wa tatu, utona tu, yaani mapaka wananchi wanakaa mabali wanawaogopa hao viongozi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...