Kwa picha za tukio lote
BOFYA HAPA
Katika uteuzi wa JK ambao unaanza mara moja, Bw. Fanuel Mbonde anakuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu. Kabla ya hapo Bw. Mbonde alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu. Bw. Hussein Othman Katanga anakuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakati Bw. John Haule anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo Bw. Herbert Mrango anakwenda Wizara ya Ujenzi na Bw. Eric Shitindi anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira.
Kabla ya uteuzi, Bw. Katanga alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakati Bw. Haule alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, ambapo Bw. Mrango alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Bw. Shitindi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Waliohamishwa ni Sazi Salula kutoka Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenda Ofisi ya Makamu wa Rais; Maimuna Tarishi anatoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii. Wengine ni Omar Chambo sasa anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi akitokea iliyokuwa Wizara ya Miundombinu; na Kijakazi Mtengwa anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Pia Dk. Ladislaus Komba, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anapangiwa kazi maalumu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo Elizabeth Nyambibo amehamia Wizara ya Fedha na Uchumi ambako anakuwa Naibu Katibu Mkuu akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Haule. Kabla ya uhamisho huo, Nyambibo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Mambo ya Ndani ya Nchi.

Haya hongereni na tunataka muchape kazi mumsaidie Mheshimiwa Rais.
ReplyDelete