
Miss Utalii Tanzania, 2011, Adelqueen Njozi akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali katika Idara ya Habari MAELEZO,leo jijini Dar kuhusiana na mambo ya kipaumbele ambayo anakusudia kuyatekeleza katika msimu wote wa kutumikia taji hilio la Miss Utalii Tanzania 2011.Adelqueen amesema kuwa atatumia fursa aliyonayo kuzunguka nchi nzima mijini na vijijini kuelimisha na kuhamasisha jamii nini maana ya utalii,utamaduni na faida zake kwa jamii na Taifa kiuchumi na kwa maendeleo ya Taifa,kama vile haitoshi ameongeza kuwa yeye pamoja na washindi wengine wataanzisha kampeni ya kuhamasisha jamii kutumia sekta ya utalii kama moja ya nyenzo madhubuti ya kupambana na umasikini,kupitia vikundi vya ujasiliamali vya utalii,ambavyo vitafanya shughuli mbalimbali ya ususi,uchongaji,ufinyanzi,uchezaji ngoma,ushonaji na uongozaji watalii na mambo mengineyo n.k
Miss Utalii Tz, 2011, Adelqueen Njozi, pamoja na washindi wengine wakijitambulisha mmoja mmoja mbele ya Waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,jijini Dar leo.Aidha mshindi huyo amevitaka vyombo vya habari nchini kutoa ushirikiano wa kutosha ilei iwe rahisi kwake kutekeleza malengo yake ya kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania Kitaifa na Kimataifa.Kutoka kulia ni Mshindi wa pili,Happy Andrew,Wa tatu kutoka kulia ni Mshindi wa tatu,Marim Rabii pamoja na Mshiriki aliyeibuka na taji la Mshiriki mwenye kipaji Miss Utalii Tanzania 2011,Daisy Mushumbusi.
Hao mabinti warembo lakini hasa nimependa mavazi yao. Siyo mambo ya kuiga wazungu na kuvaa nguo za kizungu! MaMiss wangevaa nguo za kiafrika wangesifika zaidi wakiwa nje ya nchi.
ReplyDelete