Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania John Luwanda amefariki dunia Muhimbili leo mchana baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Mtangazaji huyo wa zamani ambaye alistaafu kazi hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1990 alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili akisumbuliwa na kisukari huku akifanyiwa uchunguzi wakansa ya kibofu cha mkojo.
Madaktari walimwambia kwamba baba yake alikufa kutokana na ugonjwa wa uti wa mgongo.
Mzee Luwanda ambaye atakumbukwa zaidi na watu wa vikundi vya sanaa kwa uandalizi wa michezo ya kuigiza ya radio, mara baada ya kustaafu alikuwa anaishi katika kijiji cha Goba akilima bustani na kufuga.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Gobakijijini na anatarajiwa kuzikwa Jumamosi wiki hii.Luwanda ameacha mke watoto 6 na wajukuu 20.

RIP John Luanda.....
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema Peponi Mzee Luanda.
ReplyDeleteMungu amlaze pema mzee Luanda
ReplyDeleteRIP MZEE JOHN LUANDA. POLENI SANA FAMILIA, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KWA MSIBA HUU MZITO.
ReplyDeleteMDAU
Rest in Peace Mzee Luanda. Pole sana Kaka Beda na wanafamilia. Ingekuwa vizuri kama RTD wangefanya kipindi maalum cha kumkumbuka.
ReplyDeleteRIP mzee wetu. Pole sana sana Beda, ndugu, jamaa na wanafamilia wote. Tulimpenda mzee lakini Mola amempenda zaidi.
ReplyDelete