ankal natumaini habari za kimajukumu zipo shwari. mimi ni kijana wa kiume,umri wangu ni miaka 30,elimu yangu ni shahada(degree), rangi maji ya kunde, urefu futi5.5. kipato cha kawaida(kina jitosheleza), sijawahi kuoa na sina mtoto.dini-mkristo.

natafuta rafiki wa kike kwa mahusiano ya muda mrefu ambayo kama yatafanikiwa vizuri yanweza kuzaa matunda ya ndoa,napendelea msichana mwenye sifa zifuatazo:- umri-miaka 19-25, elimu-form six mtarajia kuingia chuo,mwanachuo,stashahada,shahada,shahada ya udhamili,phD. RANGI-maji yakunde hadi mweupe. urefu kuanzia ft5.5 kuendelea juu. dini ningependelea mkristo,lakini sio pingamizi,ila sinampango wa kubadili dini. kwa watakaowasiliana na mimi nitapendelea kubadilishana picha. natanguliza shukrani. JM. E-mail: jm4real44@yahoo.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Umekisha wakati upo chuo ulikuwa umezubaa tu, leo unahangaika. Unataka kabila gani hujasema? Na wewe kabila gani maana kuna makabila kama ya kule Mara tunayaogopa!

    ReplyDelete
  2. hakuna muoaji hapo, yani mika 30 leo ndo unatafuta mahusiano ya mda mrefu wakati wanaume wenzio wanaoa wakiwa na miaka 27? au nawe ndo wale wale? huna jipya wewe? tafuta hao uliosoma nao lazima utabahatisha

    ReplyDelete
  3. sasa sifa zote ulizoambatanisha hapo utafanya usaili nn!! kila la heri

    ReplyDelete
  4. acha hizo dogo mademu umewaacha ukiwa chuo sasa unatafuta kwenye internet hahaha wrong method....utaopoa JINI bure mdogo wangu kaaa chini muombe Mungu akusaidie kupata mke mwema acha tamaa za mwili utakufa

    ReplyDelete
  5. Kwenda zako usitupotezee muda watu tunaishu za maana za kufikiria wachumba kibao uswahilini we vipi bwana!. Kaka michuzi naomba nisaidie jambo moja, hivi kukodi helikopta kwenda kwa babu loliondo inaweza kughalimu kiasi gani nifanyie utafiti ili kama ni affodable basi tujichange na washkaji tuone tunafanyaje na hii si kwangu tu bali kwa taharifa hii watu wengi wanaweza kujikusanya na kukodi hicho chombo. Tuwekee kwenye front page ukishapata data kamili. AKHSANTE MDAU wa stockhorm

    ReplyDelete
  6. Domo zito wee... kwani huna wazazi? Watu ambao hawana uwezo wa kutafuta mademu wao wenyewe, hutumia njia ya kizamani... "baba/mama/mjomba... mimi nataka mke" kisha wao watakurekebishia. Hii njia ni ya kizamani, lakini bado ni njia nzuri sana ya kupata mwenza. Takwimu zetu zinaonyesha watu wanaopata wenza kwa njia hii huwa na mahusiano yenye mafanikio zaidi kuliko wale wanaotafutana wenyewe.

    ReplyDelete
  7. HAHAHAHAHAAHAAA!!!!! BOI U NEED JESUS!! WIF IS NOT A PUSSYCAT DOLL

    ReplyDelete
  8. The guy is good, it seems he is too honest. Alifuata maelekezo yote ya walimu na wazazi kwamba asome kwanza mambo ya mapenzi baadae. Sasa ndo wakati umefika. Inaonesha hata kwa mke atakuwa mwaminifu na mtiifu. Wadada wenye akili this is the good deal (lakini na nyie muwe watiifu kama alivyo msije mkamchanganya.

    ReplyDelete
  9. Mwacheni jamaa aendelee na msako kwa amani. Ya Mungu mengi :)

    ReplyDelete
  10. Haaaaa Umefulia wewe m2 yani 30 yrs ndo unatafuta df,domo zege(Inspector) tulia utakufa kwa tamaa za mademu wa internet wengi wameukwaa miwaya,ukimpata mkapime,pili sikiliza kipindi cha dr.ndodi alizungumza m2 kama wewe mwenye degree unataja vigezo vya kutafuta mchumba na vyote ulivyotaja ni upuuzi m2pu

    Young Money
    TEXAS

    ReplyDelete
  11. Usikate tamaa kijana. Kutafuta mwenza ni kazi ngumu. Hasa kwa mtu kama wewe ambae unajimudu kimatumizi ya muhimu. Inaonyesha unapenda vya rangi. Nafikiri vya rangi wengi wao wanapenda mfuko uliomnono. Sasa kijana jitayarisha na mapesa ili uvutie hao weupe.

    ReplyDelete
  12. Ngoja nikupe program ya kutafuta wife

    public class WifeFinder extends Girlfriend {

    Dame[] possiblewife;//array objects called dame

    public wife getWife (String name)
    {
    for(i=0;i<possiblewife.length;i++){
    if !((possiblewife[i].getDisease("HIV")){
    }
    return wife;
    }

    ReplyDelete
  13. hahaha watu mbona wanamjia juu bwana mheshimiwa hapa,jamani huu ni ulimwengu wa mtandao kila mmoja ana uhuru wa kufanya mambo yake kwa njia anayoiona inamfaa. sasa kwa ambao wanampiga madongo mimi pia ningewashauri watumie njia zao,hahaha we kaka usikonde watu wapo tu tena wasio feki utawapata tu mtandaonim achana na walio kariri kuwa 4 ni 2x2 tu,hawajui pia hata 2+2, 6-2,12/3, -2+6, yote jibu lake ni 4.
    uko right mkuu usiogope waoshavinywa tulisha wazoa sisi

    ReplyDelete
  14. duh wemkaka umetubania sana wengine,sie wengine 27 na sifa nyingine pia tunazo ila age inalimit, age is nothing bwana but a number,fungua mlango nawenginee pia twazea pata mmwenzi.

    ReplyDelete
  15. Nenda kwa babu ambi ukapate kikombe, labda kitakusaidia.

    ReplyDelete
  16. Ndugu msubiri Bwana Yesu atakupatia mke unayemtaka. Hata ukifikisha miaka 50, wakati wa bwana bado upo. Uende kanisani pia ukaombe hayo maombi yako.

    ReplyDelete
  17. KUDADADEKI KWEA MNAZI KWA MKONO MMOJA TU GHARAMA ZA NINI?

    ReplyDelete
  18. Jamani kwani tatizo liko wapi...kwani lazima ucomment humu...Kwanza waliocomment si ajabu hawana hata wa kukumbatia usiku...Mwenzenu anatafuta ndio maana kapost ....huwezijua kila mtu na yake...dada yangu walikutana na mumewe kwenye mainternet ...kwanza ndio zilikua zinaanza sasa hivi 24 years na three kids in the house...

    Kaeni kimya kama uko kwenye range yake jaribu bahati yako...Sio wote watakao mpenda kwa vile mapenzi ni two ways ..Hivyo shurti kuapply kwa wengi chemistry ikikubali ni juu yao...

    SO people try to mind your own business na sio lazima kucomment kila kitu humu. kama shuleni hakutafuta mchumba alikua busy kusoma...

    ReplyDelete
  19. Mimi chichem kitu,
    Ila wangangiaji msimkandie jamaa hivyo.
    na wewe ndugu kwani hujui kutongoza mpaka unaamua kutafuta msichana hapa?
    acha masihara wewe.

    ReplyDelete
  20. Mke anaatoka mbiguni. Mwombe M/Mungu atakupa. Achana na waliofilisika hao. Wewe una nia njema tu kuna wanawake nao vile vile wanatafuta waume lakini hawawezi kwa sababu ya utamaduni. Wenye kutafuta wapenzi wakiwa shuleni wengi ni wazinzi, wanaishia kuzoeana sana, wakifika stage ya ndoa wameshachokana. Wewe vumilia tu mwanangu iko siku milango ya mbinguni itafunguka na atatokea mke mwema. Sala usiache.

    ReplyDelete
  21. Pole sana.Yaonekana kutongoza hujui maanake siamini kama hapo ulipo hakuna mademu mpaka utupotezee muda wetu kusoma ujinga! Kwanza nakushauri nakupa ushauri mambo yafuatayo:
    Tafuta wanaojitangaza kwenye internet kama wewe. Ukiwakosa nenda kule mgombani kwa akina nanihii huwa hawana utamaduni wa kutongozana. Unabeba tu juu kwa juu na ukishamweka kwako usiku mmoja ni mke huyo tayari. Au hata nguvu ya kubeba huna? Kodisha vijana.

    ReplyDelete
  22. Waheshimiwa saana
    Mkuu Katoa Tangazo kama Hali kuhusu kwanini unamponda
    Pamoja na kuponda kote umepata nini
    unachotakiwa kutoa ushauri

    Kumbuka kuwa kila mtu anamalengo yake na ndio maana hakuwa na girlfriend kwa wakati huo

    Pia alifikiria nini anahitaji sio kuoa tuu harafu wanao unawapeleka kwa mjomba wakasomeshe au kwa baba mdogo or Mkubwa

    ustaraabu jamani


    MKUU NAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA NA UTAPATAMKE MWEMA AU G.F BOMBA KABISA WASIKUKATISHE TAMAA.

    ReplyDelete
  23. mmhh ningependa nami ni post kaemail kangu hapa nipitie mgongo wake lakini hayo majungu naogopaaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  24. Nyie watoa maoni bwana mnadhani miaka ya sasa ni ya kizamani watu wanapata wake au waume kwa kutumia internet.Mwachekesha kweli nyie,mbona email uloweka haipo au umekosea mdau?

    ReplyDelete
  25. Asante kwa ujumbe michuzi nakupenda coz unawasaidia watz wa kila aina kupublish nandoz zao na maaplication.mwambie mdau tuwasiliane kwa email linanoel@ymail.com.Asante Ankari

    ReplyDelete
  26. hahahhahahah. matangazo kama haya yananichekesha! please let us know if you are successful!

    ReplyDelete
  27. Ankari acha waseme utaona kama jamaa kama hatakujulisha kuhusu mafanikio yake.Atampata tena mcha Mungu kama anavyotaka.Huwezi jua kama kapata kikombe kwa babu kapata maona ya kusearch kwa mtandao.

    ReplyDelete
  28. We kaka usijali maneno yao kwani niwewe naisio wao "Be who you are and say what you feel, because those who mind don't matter and those who matter don't mind. But mind you now you gonna receive everything so be very careful unless otherwise madunga embe yapo. Sali sana ndoa ni baraka kutoka kwa Mungu hivyo ukiomba kwa bidii utapata.
    Siku ya harusi weka kwenye net pia tuje kufurahia wadau.
    Mwanafunzi- Ughaibuni

    ReplyDelete
  29. atawapata malaya waliosuswa mitaani kwa umalaya wao. Ni waliokata tamaa. hapo utasema umepata mke? kila mahali utakapopita watu wanakucheka kimoyomoyo kwani walishakula wakakuachia makombo. Wanawake wa maana hawapatikani kwenye mitandao kama hivi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...