Habari ndugu michuzi na wapenzi wa blog hii ya jamii, ndugu zangu mimi namtafuta mwalimu wangu anaitwa ADAM alikuwa mwalimu wa shule islamic ya al-haramain pale Dar kwenye miaka ya 1990-1998, na ni mtu wa morogoro. Elimu yake ya high school alipatia shycom shinyanga chuo cha biashara.

Katika juhudi zangu za kumtafuta mwalimu huyu mara ya mwisho niliambiwa yuko south africa anafundisha pale Cape town, nilijaribu kwenda SA Cape town hapo shule lakini sikufanikiwa kuonananae pengine anajulikana kwa jina lingine kwa pale Cape town.

Mimi ni ndugu, pia ni mwanafunzi wake wakaribu sana, lakini niliondoka nyumbani hapo TZ kuja ulaya kwa masomo miaka ya 1996 ndio mwisho wa kuonana nae na sikupata mawasiliano yake tangia mwaka huo.

Naomba mtu mwenye taarifa nae au Mr Adam
mwenyewe tuwasiliane kwenye email
husna77777@hotmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. pole sana,ndugu.Sasa tangu mwaka 1996 upo masomoni ulaya?bado ujamaliza kusoma?mimi pia nataka kuja huko kubeba box,kama kuna nafasi
    za kubeba box tutangazie at globu ya jamii,

    ReplyDelete
  2. ndugu yangu uliotuma maoni ya kwanza hiyo sio kawaida kama kubeba mabox huyo jamaa bado ni maisha tu kwani kama wewe uko vizuri kimaisha luck you.
    Lakini elewa hayo yote ni maisha sio wewe unavyofikilia watu hawana hata hiyo kazi za mabox kama unaandika maoni jaribu kufikiri sio kuonyesha ufupi wa upeo wako wa kufikilia maisha.
    Leo anabeba mabox pengine wewe kesho au mmoja ya familia yako atapanguza watu kinyesi kama kazi.

    ReplyDelete
  3. Bado anatumia jina hilo hilo na yupo south afrika huyu kwa kirefu anaitwa Adam ngamange.

    ReplyDelete
  4. kweli huyo mtu anaitwa adam ngamange hata mimi namjua lakini huyu ndugu yetu anatafuta contact yake, na south africa kafika kumtafuta lakini hakufanikiwa kumpata sasa ndugu uliyetuma maoni ya tatu jaribu kumsaidia kama unayo namba ya adam au kumtafuta adam awasiliane nae kwenye email aliyotoa huu ndio faida ya blog hii kusaidiana na kuwaweka watu pamoja kama watanzania.

    ReplyDelete
  5. Adam alikuwa Classmate wangu IFM in 90's.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...