Naomba wadau wa blog ya jamii wanisaidie, mimi mwanangu ana tatizo la kukohoa mara nyingi usiku na mchana kidogo tena mpaka anatapika nimehangaika sana mahospitalini imekuwa ngumu na nimechoka kumpa dawa.

Basi nikaenda kwa Dokta Masawe pale Moroko (wengi humu wenye watoto hasa wamama watakuwa wanamjua Dr Masawe) mtoto akaniambia ana allergy( mzio kwa lugha ya kimatumbi) ya kitu chochote kinachotokana na ng'ombe kama maziwa ,nyama na mchuzi wake chocolete n.k


Sasa kwa mtoto ngumu hiyo na hasa kama anasoma shule huko walimu wananiambia mwanao hataki kutengwa anataka wanachokula wenzake yaani inaniwia vigumu nimejaribu hata dawa za kienyeji kama zile anazosemaga Ndodi za chakula kama vitunguu,asali ,tangawizi n.k lakini wapi.

Na mjuwe kukohoa kunaumiza tena kufua kikavu anaumia sana mwanangu imebidi niweke wazi wadau wanishauri vitu gani naweza katumia kama dawa ili mwanangu nae awe katika uzima wa kufua chake.Nimesahau ana umri wa miaka 3.


Mama P.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. WAHI LOLIONDO DEAR

    ReplyDelete
  2. mimi sio mtaalam lakni pia nitakushauri, vyakula vyenye nuts, muepushe mtoto, kwani nuts zina allegy sio kwa mtoto tu hata watu wazima, na mafuta na baadhi ya mafuuta ya kupikia yanacontain nuts, inatakiwa uwe muangalifu, nyama nnavyoujua mimi kama anasubuliwa na amfua nyama sio nzuri hasa red meat. pia kuna dawa inaitwa ASWAT ni chungu lakni pia ni nzuri inatibu maradhi mengi ikiwemo kifua sugu, jaribu na itafute.

    ReplyDelete
  3. nenda loliondo kwa babu labda kama unaamini

    ReplyDelete
  4. Kwa maoni yangu jaribu dawa za asthma, ALBUTEROL hata kama han athuma hii huwa inasaidia tu kufunguwa mapafu mtoto anweza kupumuwa sawa. Naomba pia uwe advocate kwa mtoto wako, jaribu kutembelea darasa lake kaa ne wakati wankuwala, muelimishe umuhimu wa yeye kula vitu gani na kitu gani hatakiwi kula. Naomba usisubiri mwalimu pekee, nadhani sisi wazazi tunamajukumu makubwa pia. Pia hakikisha hanywi maji baridi na pia siyo unaogesha mtoto kila siku.Kama hali ya hewa hairuhusu mwache akalale siku moja au mbili hazimsababishi mtoto kukosa usingizi. Kikubwa ni afya yake. Pia inabidi uwe kakini kungalia nichakula gani kinaweza kumsababishia hili tatizo. Wakati wmwingine ni moshi wa magari na vumbi la kawaida nje na ndani ya nyumba. Angalia suala la Mold, kuna shule zimejaa Mold, nyumba zetu mambomba yanvuja chini ya sink kumejaa MOLD. Vitu ni vingi. Angalia www.web MD na usome kuhudu Asthma, Mold na allegy. Nadhani unaweza ukagunduwa mtoto wako anfit wapi. Lakini usimpe tu hizo antibiotcs tafadhali.

    ReplyDelete
  5. Pole mama na mwanao,
    Nahisi unavyojisikia, je alishachunguza ukubwa wa moyo wake? kwani moyo ukiwa mkubwa unasababisha kikohozi kisichokoma,
    Mtoto wangu ktk umri wa miaka 6-7 alikuwa na kitu kama hicho nadhani, ila alipopimwa wakasema ana mzio pia, isipokuwa dokta akanishauri asiwe anatumia vyakula vikiwa katika hali ya ubaridi, na awe anavaa nguo 2 juu,yaani kifuani muda wote avae nguo 2 kama t-sheti alafu blauzi juu,jioni au asubuhi aongeze nguo kama hewa itakua ya baridi zaidi.Tukajaribu hiyo na ilisaidia, hadi hivi ana umri wa miaka 11 yupo mzima,kikohozi kwisha, hamna mzio wala nini! ila watu hutofautiana,jaribu kucheki na moyo wake afu jaribu zoezi la kudhibiti baridi hata kama ni ndogo, ina madhara kwa watu wanao kohoa.aweza pona kama mwenzake,namuombea kwa MUNGU.
    Mama Pendo-KIA.

    ReplyDelete
  6. Naomba sana huyo mtoto miaka mitatu bado anhitaji kukaa nyumbani , kama nakifuwa ndiyo unakwenda kukiongezea huko. Mwache nyumbani wegine tulianza darasa la kwanza miaka saba na hakuna chekechea,na tumepata elimu za juu kama wengine waliofukuzwa nyumbani kwao wakiwa wadogo. Mtoto anahitaji upendo zaidi nyumbani, na siyo shule wakiwa wadogo. Nadhani kama umesoma na umeendelea, kukimbiza mtoto shule siyo dawa, dawa ni wewe kuwaonyesha upendo na kuwasaidia kujenge ubongo wao sawa. Watoto wankomaa miili tofauti sasa htaki azidi kupata madahra zaidi.

    ReplyDelete
  7. Acheni utani na masuala serious jamani, huyo babu anatibu Alergy? Mdau, kabla ya kupata suluhisho la kisayansi au la kienyeji, jaribu kumuepusha mtoto na mazingira hayo kama ulivyoshauriwa na daktari Masawe. Sioni uhusiano wa alergy na Kisukari, ukimwi au presha (hata kwa wanao amini Loliondo) na Alergy kwa mtoto wa miaka 3. Huko mtoto atapewa dozi sawa na ya mtu mzima ya dawa isiyojulikana content yake wala uwezo wake, na madhara yake sio lazima uyaone leo.

    ReplyDelete
  8. Yanga ImaraMarch 24, 2011

    Kuna watu humu akili zao kama nguruwe tuu, punguwani kabisa. Mwanamama anaeleza matatizo yanayomsumbua mwanawe, nguruwe wa kizungu wanasema "nenda loliondo", aaagh!!! ndiyo mna uhuru wa kuuonyesha upumbavu wenu, lakini kwenye matatizo ya watu msilete mzaha.

    ReplyDelete
  9. Sela pole wee wavo P!

    Anao uo mwana awajwa nini waa? Twekiti ni mbeho mhh, Dar tehena mbeho ya huvo, sari ao mavumbi na vijo. polewe mama wavo mwana mgheshe vijo hesa umanye vila vyemsua.

    ReplyDelete
  10. nadhani alivyoshauri daktari ni vizuri kama utachukua muda zaidi kumelelewesha mtoto, mimi napiga box la kulea watoto ughaibuni kwenye nursery, naona wazazi huku wamejitahidi zaidi kuwaeleza watoto wao nini wasile,ikifika muda wa kuwapa chakula mtoto mwenyewe anakueleza yeye ana allegy ya kitu fulani usimpe, jaribu kufata ushauri wa dokta pia muelimishe kujifahamu zaidi hatakiwi kula nini

    ReplyDelete
  11. Mimi vile vile si daktari lakini nadhani ni tatizo la allergy kwa hiyo dawa ni kujiepusha na hizo triggers. Lakini cha kukupa moyo ni kwamba kuna baadhi ya matatizo kama haya huwa yanaisha yenyewe umri unapoongezeka. Mimi mwenyewe nilikuwa chronic wa allergy ya vumbi na kibaridi hasa nikienda high altitude na nilitumia kila dawa lakini wapi. Tatizo liliisha lenyewe nakumbuka mara tu nilipomaliza form six!

    ReplyDelete
  12. mimi huwa nashindwa kuelewa watu wengine huwa wana maanisha nini, mtafuta msaada unadai umekwenda kwa dr.masawe(nadhani ni dr.furaha masawe)kama sikosei niliondoka nikaacha anaclinic yake hapo moroko, nayeye kama daktari wa watoto nadhani hilo jibu la mwanao kuwa na allergy ya baadhi ya protein hakulitoa tu bali alifikia baada ya kupata history ya ugongwa,kumpima n.k
    sasa inaelekea hukuamini tactic aliyoitumia dr ktk kumtibu na kushauri jinsi ya ku handle issue ya tatizo la mwanao? basi nadhani wewe kinachokufaa sasa ni kwenda kwa wale watu ambao wanatibu bila kujua tatizo linaanzia wapi na wapi pa kushika ili kulizuia ili wakupe ushauri bubu huenda utakufaa,na ukisha maliza pesa yako huko pamoja na kuichakaza afya ya mwanao kwa dawa usizojua zinavyo tibu namini utarudi tu hospitalini na hapo utapata tena msaada kwa mwnao,na usipo fanya hivyo basi huyo mwanao atakapo kuwa mkubwa wa kutafuta msaada peke yake,ataupata hospitalini.
    unachohitaji ni kupata shule ya kutosha kuhusu allergy,na mwanao kufanya test zitakazo onyesha ana allergy na protein zipi,kisha kuziepuka popote pale zitakapo kuwa iwe ni ktk chakula,vipodozi,dawa,n.k
    dawa ya kwanza ya allergy ni kuepuka kukutana na allergens(visababisha mzio).
    nadhani umenielewa vizuri ninacho kisema. lakini kama utaukimbia ushauri wa wataalam na kutafuta wa watu wanaoguess bila kujuwa nini tatizo,utaishia kumfanya mwanao sehemu ya majaribio ya kila oni unalopewa humu.na pia sikushauri kuanza kusoma ktk internet na kuanza kujitibia mwanao,hiyo itakuweka ktk hatari usiyo itegemea.maanakama daktari nakwenda shule miaka mingi akijifunza hilo unalo taka kujifunza masaa kadhaa ktk internet ukidhani utapata elimu ya kutosha huko,utaishia kuwa mtu anayeingia ktk internet kusoma jinsi ya kuwasha na kurusha ndege kwa masaa kadhaa kisha kujifanya pilot ili urushe ndege,na huu ni ushauri si kwako tu bali na kwa wasomaji wengine pia wa hii blog ambao sio ma daktari na wanao penda kujitibia,kumbukeni elimu duni ya kitu flani ni hatari kuliko kutokuwa nayo kabisa.maana kama hunayo utaogopa kujaribu,ukiwa nayo duni utajaribu na itakugeuka usivyotegemea.
    DR.

    ReplyDelete
  13. pole mama.. mimi mwanangu alikuwa na tatizo hilo hilo la kukohoa mpaka kutapika nikaambiwa vitu vingi sna dada yangu.. kuja kutambua alikuwa ana minyoo pia na kimeo sijui kinaitwaje kwa kiswahili kamili.. basi nikampa dawa ya minyoo ila kimeo wameshindwa kumkata kwani ana umri wa miaka 2 na huku nje ya nchi hurusiwi kufanya hivyo ila namshukuru mungu sasa hivi hajambo jaribu na dawa za minyoo pia ila usijaribu kumpa antibiotics kwani bado mdogo na mwili wake unabuild antbodies. kwa hiyo maantibiotiocs sio mazuri sana kwa watoto dear...

    ReplyDelete
  14. MAMA P. NIPE CONTACT ZAKO EMAIL OR ANY CONTACT. NIKUPE USHAURI . KUTOKANA NA EXPERIENCE NILIYOIPATA KWA MWANANGU. ALIKUWA NA MATATIZO KAMA YA WAKWAKO. SASA YUKO 7YR NA KAPONA.ILA ALIPATA TABU AKIWA 2YRS HADI HAPO 4. THANX MAMA MWENZIO. UK.

    ReplyDelete
  15. Kama DR ameshakuambia hivyo basi fuata masharti hayo na wala usiseme kuwa anataka wanacholla. Ndio hivyo ni kama kilema chake na inabidi uhangaike kama mzazi. Mwanangu mmoja ana allergy mbaya sana ya peanuts na inabidi tusome kila kitu kabla hatujaingiza humu ndani. Na shuleni inajulikana na walimu wanakua very careful kwa watoto wenye allergies. Ni ngumu sana na tuna mpango wa kurudi TZ katika miaka mitatu najiuliza huko TZ sio kila kitu kinakua labeled sasa sijui itakuaje?

    Ndio hivyo maadamu umeshajua kuwa ana allegey ya dairy fuuata masharti. Uzazi sio lele mama na ukiona mwanao anakohoa najua inauma sana..Sisi wa kwetu akipata hiyo kama hayupo karibu na hospital anaweza kufa.

    ReplyDelete
  16. dawa ya minyoo sugu umejaribu?. Ni tofauti na dawa za minyoo ya kawaida. Kuna minyoo migumu sana kufa kwa dawa za kawaida, hasa ile inayokaa kwenye nyama kama za nguruwe! Jaribu kuchunguza kwanza!

    ReplyDelete
  17. Umeshakutana na daktari bingwa wa watoto, amempima amekwambia na tatizo ni allergy ya vitu hivyo, kwa hiyo hapa mwenye tatizo ni wewe mwenyewe unayeshindwa kumuepusha mwanao na vitu vinavyomdhuru full stop. Kama shule anayaosoma wanashindwa kumtengea chakula na kumlinda wakati wa kula basi mwamishie shule nyingine. Kumbuka mengi ya maoni hapo juu si sahihi kwa mwanao kwani udaktari hatutumii experince bali elimu. Ingekuwa udaktari ni experience basi mabibi zetu na mababu zetu wote wangekuwa madaktari .

    ReplyDelete
  18. mADAKTARI WA SIKU HIZI VIMEO. HATA KAMA ANA UZOEFU WA SIKU NYINGI. HAWAJI-UPDATE. DAKTARI UKIMWAMBIA KIMEO HAELEWI. ATAISHIA KUKWAMBIA ALEJI TUU.

    ILE OVULA (KIMEO)INAPOPATA INFECTION INAVIMBA, PENGINE INAWEZA KUTOA USAA, WENZETU VIJIJINI HUWA WANAVIKATA NA NJIA HII SI NZURI. KAA NA DR MWINGINE UMWELEZE. LAKINI MCHEKI KWANZA KIMEO ( OVULA) KAMA AMEVIMBA. KILE KIKIVIMBA KINAGUSA CHINI AMBAPO HAKIPASWI KUGUSA? HIVYO MTOTO HUKELEKETWA NA KUKOHOA. NA KIKOHOZI CHA NAMNA HIYO WALA HAKIMUUMIZI KIFUA. UKIMUULIZA MTOTO ATAKAWMBIA HAUMII.

    WAZO LINGINE ANAWEZA KUWA NA KIFADULO ( WHOOPING COUGH ) NAYO HUCHUKUA MUDA MREFU KUPONA. HAYA YOTE YACHUNGUZE UONGEE NA DR. DAKTARI AKIWA MSTAARABU ATAKUSIKILIZA NA ATAKUSAIDIA

    USHAURI WANGU NI HUO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...