Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanznaia (TBL) Mwanza, Richmond Raymond akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya jinsi kiwanda hicho kilivyoweka utaratibu wa kuwapatia wananchi maji ya bure kutoka kiwandani hapo. Prof. Mwandosya alifanya ziara kiwandani hapo kuona juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya Binadamu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra ya maadhimisho za Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya (katikati) na wadau wengine wa maji,wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha TBL Mwanza,Jeremia Kamambi (kulia) walipotembelea kiwanda hicho kuona uzalishaji wa bia na juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya Watu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo imefikia kilele juzi jijini Mwanza.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya (kulia) na Meneja wa Kiwanda cha TBL Mwanza, Richmond Raymond (kushoto) pamoja na Meneja Ubora wa Bidhaa wa kiwanda hicho, Caroline Nhonoli (katikati) wakiwa ndani ya kiwanda hicho wakati Waziri alipotembelea kiwanda hicho kuona uzalishaji wa bia na juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya Watu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nachompendea Mwandosya, kasoma alafu hana upumbavu wa kupaka dawa nywele zake. Ukubwa dawa!

    ReplyDelete
  2. halaf waandishi muwe makini jaman huyo ni waziri wa maji,sio maji na umwagiliaji....umwagiliaji ilisharudi wizara ya kilimo...hiv waandishi mbona mnareport vitu vya ajabu wakat baraza jipya lilipotangazwa kitu cha kwanza alisema idara ya umwagiliaji imerudi kilimo lakin mpaka leo mnasema wizara ya maji na umwagiliaji huu ni ukosefu wa umakini na kazi yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...