Na John Nditi, Morogoro
WATU watano kati yao wakiwemo wanafunzi watatu Shule ya Sekondari ya Milengwelengwe pamoja na Shule ya Msingi Mngazi , Tarafa ya Bwakila, Wilaya ya Morogoro, ni miongoni mwa walifariki dunia hapo hapo baada ya kupingwa na radi , ambayo pia iliwajeruhi wanafunzi wengine 14.
Matukio hayo ya vifo yametokea wiki moja iliyopita, ambapo kwa upande wa wanafunzi hao wa Shule ya Sekondari hiyo walipatwa na mkasa huo walikuwa ni washangiliaji kwenye mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu na timu ya Kijiji cha Gomero ,ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Ummiseta ngazi ya Wilaya ya Morogoro.
Mbali na vifo hivyo vya wanafunzi hayo pia tukio kama hilo la radi lilitokea Machi 19, mwaka huu katika Kitongoji cha Mikobola, Kata ya Ngerengere baada ya kuwaua wafugaji wawili wa jamii ya Kimasai waliotambuliwa kwa jina moja moja , la Sembeu ( 28) mkazi wa Kijiji cha Sinyaulime pamoja na Chamiti (55) mkazi wa Kijiji cha Diguzi ambapo kwa pamoja walifika katika kitongoji hicho kwa ajili ya kuhudhiria mkutano wa kifamilia.
Diwani wa Kata ya Ngarengere, Kibena Kingo , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro alisema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Wilaya ya Morogoro kuhusu tukio hilo lilolotokea wiki moja kabla ya radi kuwaua wanafunzi wa Sekondari Milengwelengwe.
Akizungumzia tukio mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Issa Machibya na viongozi wengine wa Serikali ya Wilaya na Mkoa, Mkuu wa Shule hiyo ya Milengwelengwe , Mugusi Burwae, alisema tukio hilo lilitokea saa 11: 43 jioni ya Machi 25, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Shule ya Sekondari ya Milengwelengwe, kuwa siku hiyo kulikuwepo na mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu baina ya Shule yake na timu ya Kijiji cha Gomero, ambapo kabla ya kufikia mapunziko mvua lianza kunyesha kitendo kilichowafanya wanafunzi walokuwa washangiliaji kukimbilia kujificha madarasani.
Hata hivyo alisema punde ilipiga radi kubwa wakiwa mchezoni na kuwafanya wachezaji wa timu hizo kulala chini na yenye akiwa mwamuzi wa mchezo huo kubakia amesimama, lakini baada ya dakika mbili kupita Mwalimu mwenzake alifika uwanjani kumpatia taarifa kuwa radi iliyopiga imewaua baadhi ya wanafunzi waliokuwemo wamejificha madarasani.
Aliwataja walikufa papo hapo baada ya kupigwa na radi hiyo ni Richard Abias ( 15), mwanafunzi wa kidato cha kwanza na mwingine ni Adolf Kunambi ( 20) mwanafunzi wa kidato cha nne , ambapo mwanafunzi wa shule ya Msingi Mngazi wa darasa la tano aliyekufa ni Abdallah Kibwe ( 12).
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Shule, radi hiyo ilipopiga iliwakubwa wanafunzi 17 , ambapo watatu walipoteza maisha na wengine 14 waliojeruhiwa kukimbizwa katika Zahanti ya Kijiji cha Mngazi na kulazwa , hata hivyo watatu walikuwa na hali mbaya walihamishiwa Kituo cha Afya cha Duthumi kupata matibabu zaidi.
Alisema majeruhi wawili kati ya watatu walikuwa bado wamelezwa katika Kituo cha Afya cha Duthumi na Zahanati ya Kijiji hicho walihamishiwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata matibabu zaidi , ambao ni Stella Theodori ( 16) mwanafunzi wa kidato cha pili na Seleman Omari wa kidato cha nne ,ambapo Zainabu Litambiko ( 17) wa kidato cha pili hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Machibya, alisema kuwa kabla ya kumalizika kwa mwezi Machi mwaka huu , ajali ya radi imepoteza watu wanane kwa mpigo.
Alisema kuwa majanga hayo ya radi yapo kila mahali hasa nyakati hizo za mvua na kutolea mfano kuwa katika Mkoa mpya wa Njombe ambapo yenye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa , radi iliua watu watano kwa mara moja.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, aliwataka wananchi kuwa na utulivu na kuona vifo hivyo vimetokana na mapenzi ya mungu na si kuingiza imani za ushirikina ndani yake.
Katika hatua nyingine, Serikali ya Mkoa pamoja na viongozi wengine akiwemo mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini, Innocent Kalongeries kwa pamoja walitoa sh: 700,000 kwa wafiwa wa familia hizo tatau ikiwa ni rambirambi kutokana na kufiwa na watoto wao.

Kwa upande wangu,hizo ni ajali zisozoepuka na ukizingatia kwa nchi kama Tanzania,ila mungu ni mkubwa atuepushe na hayo mabaya yanayotokea,tumwombe mungu awapokee ndugu zetu wadogo zetu walipoteza maisha na kuwatakia subira wafiwa kwa kipindi hiki kigumu,na waliopo mahospitalini wapone haraka na warudi mashuleni,tuwe watulivu na tumwombe mungu na atatusaidia.
ReplyDeleteAmin......