Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi Vitabu kwa waakilishi wa Shule Nne za Sekondari za jijini Dar.Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba,Mary Mpagata na Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Aboud Jumbe,Rose Mkono.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano akionyesha moja ya kitabu kwa wanahabari.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano (kulia) akikabidhi vitabu kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Aboud Jumbe,Rose Mkono (kati) na kushoto ni Kaka Mkuu wa shule hiyo,Paschal Revocatus.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, inayotoa huduma za gharama nafuu nchini, leo imekabidhi msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule za sekondari nne za mkoani Dare s Salaam, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaidia jamii hapa nchini.

Shule zilizopata msaada wa vitabu ni Sekondari za Barabara ya Mwinyi na Aboud Jumbe zilizopo katika wilaya ya Temeke pamoja na Yusufu Makamba na Turiani zilizopo wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano cha Airtel, Beatrice Singano, alisema kuwa shule hizi nne za jijini Dar es salaam ni kati ya shule 104 kutoka nchi nzima ambazo zimenufaika na msaada wa vitabu vyenye thamani ya Shilingi milioni 104, kufuatia droo maalum iliyofanyika mapema mwaka huu kwa kujumuisha jumla ya shule za sekondari 520.

“Tumeamua kuweka uwiano sawa wa shule kutoka kila mkoa ili kuhakikisha kuwa vitabu hivi vinawafikia wanafunzi katika maeneo yote nchini. Tumetenga Shilingi milioni 104 na hivyo kuwezesha kila shule kupata vitabu vyenye thamani ya Shilingi milioni moja”, alisema Singano.

Aliongeza kuwa, kwa kuzingatia ya kwamba kila shule ina mahitaji ya vitabu tofauti tofauti kulingana na mitaala waliyonayo, shule zote zimepewa vitabu kutokana na mapendekezo waliyotoa juu ya aina gani ya vitabu wanahitaji na kampuni ya Airtel kuwapatia ili kuziwezesha shule hizo kukabilianana uhaba wa vitabu.

“Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kinaongezeka, hasa kupitia upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Tangu tulipoanza mpango wetu wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali za sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita, tumeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 800”, alisema Singano.

Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.

Mbali na shule 104 za sekondari ambazo zimenufaika na mpango huu wa kusaidia vitabu vya ziada na kiada, Airtel Tanzania tayari inao mradi wa kusaidia shule za msingi hapa nchini, ambapo kampuni imejitolea kufanya ukarabati mkubwa katika moja ya shule wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Katika sehemu ya majaribio ya mradi huu, kampuni ya Airtel mbali na ukarabati wa shule hiyo, pia imejenge majengo mapya kumi.

Baada ya mwaka huu, kampuni itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kuendeleza juhudi hizi na kuweza kuzifikia shule nyingi zaidi nchi nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimeona vitabu nikakumbuka tuliyosoma enzi za UPE...Ilikua notebook ikijaa unapeleka kwenye store ya vitabu mwalimu anakagua halafu anaikata katikati anakupa nyingine. Tulikua civilized kishenzi, ufisadi, uchakachuaji ulikua hamna kabisa. Unakwenda kusafisha store ya vitabu lakini wala hutoki na kitabu chochote. Nakumbuka mwalimu aliyekua anasimamia ile store alikua anaitwa Mwalimu Kipengele....NAURA Primary School mpoooooooooooo???????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...