Kikosi cha Taifa Stars kilichoibanjua Afrika ya Kati
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Afrika ya Kati, Accorsi Jules (kushoto) akisalimia na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jan Poulsen mara baada ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (CAN) kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Kiungo mshambuliaji wa Taifa Stars, Mohamed Banka akitafuta mbinu za kuwatoka walinzi wa timu ya Afrika ya Kati, Manga David (kushoto) na Enza Manasse (12).
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa akimtoka
beki wa timu ya Afrika ya kati. Manga David.

Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza mshambuliaji wa timu hiyo Mbwana Samata baada ya kuifungia timu yake bao la pili dhidi ya Afrika ya Kati katika mchezo wa kuwania kufuvu fainali za mataifa ya Afrika (CAN) uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar
Mashabiki wakishangilia. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Taifa, Taifa Stars leo imeibanjua Afrika ya Kati bao 2-1 katika mechi ya awali kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwakani ilofanyika uwanja wa Taifa.

Mechi hiyo ya vuta nikuvute ambayo Stars iliahitaji ushindi ili kujiweka sawa katika mbio hizo za kuwania fainali hizo zitakazofanyika Gabon na Equatorial Guinea, ilishuhudia wenyeji wakipigwa bao mo9ja katika kipindi cha kwanza.

Stars ilisawazisha dakika ya 49 Shaaban Nditi wakati bao la ushindi liliwekwa kimiani na Mbwana Samatta dakika ya 89.

Stars ilicheza mechi ya kwanza na Algeria na kutoka sare ya bao 1-1 kabla ya kufungwa bao 1-0 na Morocco nyumbani.

Ushindi wa mechi ya leo umerejesha imani ya Tanzania kusonga mbele.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Haya ndiyo mambo tunayoyataka ushindi kwa kwenda mbele.
    Hongera STARS

    ReplyDelete
  2. Hongereni Taifa Stars!! TFF anzeni kuiandaa timu sasa kwa ajili ya mechi ya marejeo.Leo Tumefurahi sana.Ila kitendo cha TFF an TBC cha kutokukubaliana na kuonesha mechi live..kimetusikitisha sana Watanzania hasa sisi wa vijijini!!

    ReplyDelete
  3. TFF ni jukumu lenu kuhakikisha wachezaji wetu wanaocheza soka la kulipwa wanafika nchini on TIME.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...