Wanachama wa Union of Women Friends (UWF) pamoja na Wageni waalikwa mbalimbali wakiserebuka jana jioni ndani ya Club Continental, kwenye hafla yao fupi kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake ambayo itafanyika kesho Duniani kote.Tafrija hiyo ndogo iliandaliwa na kikundi hicho kwa madhumuni ya kuienzi siku hiyo ya Wanawake Duniani ambayo husherehekewa Machi 8 kila Mwaka.Aidha sherehe hiyo ambayo inaadhimishwa kesho itabeba ujumbe mzito- Haki sawa katika elimu,mafunzo ya sayansi na teknolojia ili kuwapa fursa nzuri.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo,ambaye pia ni Mkurugenzi wa NIMR,Dr Mwele Malecela akifafanua jambo kwa umakini mkubwe mbele ya wanachama wa UWF pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tafrija hiyo fupi iliyofanyika ndani ukumbi wa Continental club,jijini Dar.
Meneja Udhibiti wa masuala ya kisayansi kutoka Nestle Tanzania, Bi. Masha Yambi akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kusherehekea siku ya wanawake Duniani,iliyoandaliwa na kikundi cha umoja wa akina mama/wanawake Marafiki (UWF)
Wa pili kushoto ni Meneja Udhibiti wa masuala ya kisayansi kutoka Nestle Tanzania,Bi. Masha Yambi akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa UWF.
Mwenyekiti wa UWF.Bi Mwate Madinda akiwakaribisha wageni waalikwa akiwemo mgeni rasmi kwenye tafrija hiyo
Wa pili kushoto ni mgeni rasmi wa hafla hiyo,ambaye pia ni Mkurugenzi wa NIMR,Dr Mwele Malecela akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa UWF.Ukitaka kuona matukio mbalimbali yaliwahi kufanywa na UWF,BOFYA HAPA
pichani kulia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Vodacom Foundations,Mwamvita Makamba akikaribishwa kwenye hafla hiyo,iliyofanyika katika club ya Continental,jijini Dar.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Vodacom Foundations,Mwamvita Makamba akiwa amepozi na baadhi ya Wanachama wa UWF.
Wageni waalikwa Wanachama wakiwasili kwenye hafla hiyo jana jioni ndani ya Club Continental,jijini Dar.





huyo si ni masha makata?? basi kamichuzi heri uwe unaandika na majina yao ya zamani tunayoyajua, anaonyesha kawa mtu mzima sasa nisingemjua mpaka nilivyoona picha ya pili
ReplyDeleteGo masha waonyeshe wanawake jinsi ya kuwa BOSS