Abiria wanaotumia stendi ya Njombe jana wamekwama kuitumia stendi hiyo baada ya kuibuka vurugu kubwa za kupinga ubovu wa stendi hiyo na kiwango kikubwa cha ushuru pasipo kufanya ukarabati wa stendi hiyo.

Hali hiyo imekuja huku spika wa bunge na mbunge wa jimbo hilo Anne Makinda akiwa katika mapokezi ya ugeni wa kamati ya bunge hesabu za serikali na mashirika ya umma ambayo ilikuwa safarini kuelekea Ludewa .
Wameueleza mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa wamefanya hivyo ili uongozi wa mji wa Njombe kutengeneza stendi hiyo ambayo imekuwa ikitegenezwa na fundi selemara na kuwaacha wakandarasi ambao wanasifa ya kufanya kazi hiyo.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika vurugu hizo ambazo zilipelekea pia spika wa bunge kujaribu kuwatuliza vijana hao bila mafanikio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mungu ibariki Tanzania, dumisha uhuru na umoja! CHADEMA wanakuja huko then CCM mseme tena kuwa wanachochea uasi!

    ReplyDelete
  2. Watanzania wenzangu watu wanaongea, vyombo vya habari vinalalamika kuhusu baadhi ya mikoa ilivyo sahaulika haya ni makataba ambayo serikali inayaona lakini hawajali sasa kaeni mkijua wanapohitaji kura zenu hao viongozi wanakuwa waungwana hebu amkeni msiwape kura zenu wanajua kabisa kama wataboresha sehemu muhimu kama hizo wakaazi wengi mtajipatia ruzuku lakini wapi vichwa vyao juu kama nyoka hawana hata imani na wananchi wao vikao vya bunge kila siku kinachifanyika hatuvioni kazi kubishana tu wananchi wao wanateseka. Kiongozi unakuwa na furaha unapowatatulia matatizo wananchi wako lakini si viongozi wetu wao wanaona fahari watu wanavyo teseka hii ndiyo bongo yetu msasa aliotupiga hayati baba wa taifa ndiyo unaotuasaidi sasa hivi nchi kuwa na amani kama hii ila mkumbuke binaadamu atakapo choka ni afadhali ya SIMBA simnaona watu wanavyo jifunga mabomu kwenye viuno hao wamechoka.MUNGU TUSAIDIE.

    ReplyDelete
  3. HAO CHADEMA TU!

    ReplyDelete
  4. Poleni sana yawezekana mtatengenezewa MAMA siameona mlivyokomaa, vinginevyo wanataka ubaya. Na mkoa mmepata pataboreshwa tu, japo hiyo stendi ni ndogo sana sijui mna eneo jingine la kuweka stendi mpya na ya kisasa? Nashauri eneo la Uwanja wa ndege wa Chaugingi libadilishwe matumizi ijengwe stendi kubwa na maduka makubwa kuzunguka. Uwanja uwekwe nje ya mji!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...