Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Ezekiel Maige

Watu waliovamia maeneo ya hifadhi za Maliasili katika mkoa wa Rukwa wametakiwa kuondoka kutoka kwenye hifadhi hizo ifikapo tarehe 31 Julai 2011 Muda huo umewekwa ili wahusika waweze kuvuna mazao waliyopanda hifadhini.

Hayo yalisemwa Jumatatu na Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Ezekiel Maige alipokuwa anatoa majumuisho kwa viongozi wa mkoa wa Rukwa baada ya kufanya ziara ya siku kumi katika mkoa huo kukagua shughuli za uhifadhi zinazosimamiwa na wizara yake.

endelea kusoma huko>>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mh Maige nimekuwa nikifuatilia sana utendaji kazi wako tangu mwanzoni kabisa. Sina shaka unania ya dhati kabisa kuiendeleza maliasili yetu na kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo ya Tanzania na wananchi wake hasa katika kupambana na suala la umasikini uliokithiri miongoni mwa wananchi hasa wanaoishi karibu na mapori na hifadhi zetu.

    Kuna mambo mengi sana yanayozunguka usimamizi wa maliasili hizi hata kufikia hali tulio nayo sasa: Nitasema machache kwa leo, yamkini kama Mh. unapata nafasi pia kusoma mtandao huu unaweza kuyatia manane.

    Suala la kwanza:
    Dunia ya leo imekuwa na matatizo ya kimazingira kutokana na uharibifu unaofanywa na wanadamu ikewemo ukataji miti ovyo kwa ajili ya nishati ya kupikia na mambo mengine. Katika hili kinachanishangaza ni kuwa pamoja na kuwepo kwa takwimu za kutosha kuhusiana na kasi ya kupotea kwa misitu yetu bado wizara na idara zake hazijachukua hatua mathubuti na kwa vitendo kuliangalia suala hili kwa undani na kufikiri ni kwanamna gani tuondokane nalo. Kwa mfano; suala la uchomaji wa mkaa limeelezwa kuwa ni mojawapo ya sababu ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi tuanayoyaona sasa. Watu ambao wamekuwa wakikamatwa na mikaa bila vibali wanatozwa faini, mkaa unachukuliwa na mamlaka husika, halafu unapigwa mnada kwa watumishi?!!?!! Ili na watumishi nao waendelee kuzalisha hewa ya ukaa, lakini wizara hiyo hiyo kipindi cha maonesho ya sabasaba na nanenane wapo kimbelembele kuhamasisha watu kuondokana na matumizi ya mkaa kutokana na sababu nilizotaja hapo juu. Ningekuwa mimi ndo mwenye mamlaka watumishi wote wa wizara, serikali kuu na halmashauri zote wangehamasishwa matumizi ya majiko mbadala ikiwemo gesi ili kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira, hata ikiwa kuwakopesha majiko hayo pamoja na mitungi ya gesi ya kuanzia. Polepole Tanzania yote tungefikia kusema mkaa au kuni basi tena.
    Mh. makampuni katika hifadhi zetu yaliyomengi yanatumia mkaa kupikia, huu pia ni uharibifu wa mazingira, watu hawa si masikini hata washindwe kutumia majiko ya gesi, imagine kuchemsha maji ya watalii mapipa kwa mapipa unatumia kuni sijui kwa msimu mmoja kampuni inatumia kiasi gani cha miti (ambayo ni makazi ya viumbe tena mhimu sana katika ekolojia wakiwemo wadudu). Sina hakika labda tukifanya utafiti tutajua kiasi gani cha miti kinapotea katika hili na kiasi gani cha hewa ya ukaa kinazalishwa, wakuu wako zaidi wanachoangalia ni lini nitapata safari. na wakikutana na wamiliki wa makampuni haya wanawachekea tu. Hii si sawa, kwani ukicheka na nyani utavuna mabua!!!

    suala jingine: linafuatana maagizo uliyoyatoa huko Rukwa-Lukwati, moja ambalo limenifurahisha ni kutaka kufanyike utafiti ni kwa kiasi gani mapori na hifadhi vimevamia na mifugo. mambo kama haya vijana wamekuwa wanataka kuyafanya tena bila gharama lakini mara nyingi wanakuwa wanakwazwa na kunyimwa fursa pengine kwakuwa mara nyingi wakuu wanaona hayana maana au hayana masilahi kwa wakubwa na kuonekana kama wanajifanya wanajuwa zaidi kuliko wakuu walioko katika viti vya enzi!, hivyo mambo yanalala kama unavyoona. Agizo kama hili si ajabu wakatafutwa wataalam na kuwalipa mipesa mingi ili wafanye huo utafiti kumbe kitu kama hicho ndo incentive kwa watumishi na ndo changamoto wanazotakiwa kukabiliana nazo.

    Wizara na idara zako kwa sasa zinawasomi wengi sana lakini wanatumika sivyo ndivyo, hawa watu wanatakiwa watumike na kutupatia majawabu ya matatizo mengi yanayoikabili wizara yetu na maliasili ya nchi hii.

    Haki yani kwa maliasili japo kwa uchache wa rasilimali tungekuwa seriuos na kuziendeleza tungekuwa mbali. Yamkini umeweza kuwauliza vijana hasa chini ya wahifadhi wakuu kwa mfano vitu gani wangefikiri vifanyike kuziendeleza maliasili zetu, kama sivyo ningependa kazi hiyo ulioianza ifike muda ukutane na watumishi hasa wa kati kwa pamoja ukaongea nao ukiwa kama kijana mwenzao nina hakika utapata mambo mengi ya kuendeleza nchi yetu.

    Nakutakia kazi njema na uwaamshe hawa watu wamelala sana hasa hiyo layer ya juu. Wanfikiria mikutano zaidi na si utendaji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...