.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)

Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Bw. Richard Wells akikabidhi funguo za
jengo hilo la Kliniki ya macho kwa Mkurugenzi mkuu Hospitali ya KCMC Bw. Moshi Ntabaye.

Mkuu H. Mizengo Pinda akisoma risala yake wakati alipozinduz kliniki ya macho katika hospitali ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro leo, wengine katika picha kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami,Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) Teddy Mapunda na Mkurugezni Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Richard Wells anayemuangalia Waziri Mkuu,na pichani kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa la (KKKT) Tanzania Alex Malasusa na Askofu Martin Shao.

Mkurugezni Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi wa kliniki ya macho KCMC mapema leo asubuhi,Wells pia alizungumzia mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanywa na kampuni yake kuisaidia jamii.
Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL),Teddy Mapunda akimkaribisha mgeni rasmi,Waziri Mkuu Mh Pinda pamoja na wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa kliniki ya Macho ya KCMC mapema leo asubuhi.

Baada ya kuzindulia rasmi.

Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimpongeza Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells, mara baada ya kukata utepe kuashiria kuwa kliniki hiyo imezinduliwa rasmi leo,Kliniki hiyo ya Macho iliyojengwa na kampuni ya Serengeti SBL katika hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro leo, imegharimu kampuni ya Serengeti kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 265.6 za kitanzania.

Waziri Mkuu,Mh Pinda akisalimiana na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Richard Wells mara baa ya kuwasili kwenye uzinduzi wa kituo cha Kiliniki ya Macho cha KCMC,kilichojengwa kupitia mfuko wa EABL na Serengeti Breweries mapema leo asubuhi mjini Moshi,pichani kati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL),Teddy Mapunda.

Waziri Mkuu,Mh Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya Serengeti Breweries (SBL),Teddy Mapunda mara baa ya kuwasili kwenye uzinduzi wa kituo cha Kiliniki ya Macho cha KCMC,kilichojengwa kupitia mfuko wa EABL na Serengeti Breweries mapema leo asubuhi mjini Moshi,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Mkuu wa KCMC,Bw.Moshi Ntabaye ambao ndio watakao kuwa wakikisimamia kituo hicho.Nyuma kushoto ya Waziri Mkuu ni Askofu Mkuu wa kanisa la (KKKT) Tanzania Alex Malasusa na Askofu Martin Shao.
Huyu dada kwenye hizo picha si mara moja namuona akisalimiana au kuzungumza na waheshimiwa na watu mbali mbali anakuwa amevaa hiyo miwani nadhani ni ya jua. Miwani hii huvaliwa mtu unapokuwa una-face jua moja kwa moja na zaidi unapoendesha gari wakati kuna jua. Pia miwani hii hutumika pale ambapo kwa sababu fulani hutaki kuonyesha macho au sura yako kwa ujumla. Majambazi na wahalifu wengine utakuta wameivaa hata usiku! Kwa sababu hawataki kuonekana. Walioumia usoni pia au ambao wana magonjwa ya macho huficha kwa kuvaa hiyo. Sasa huyu dada, anaposalimiana na waziri mkuu, miwani ya macho ya nini! Kama jua kali si anatoa mara moja akimaliza anairudishia? Ni heshima kweli hiyo unasalimiana na mtu umeficha macho yako hata hayaonekani, wewe tu ndo unamwona. Ni matumizi sahihi haya ya hiyo miwani au ndo kama kawaida yetu wabongo tunaiga mpaka tunapitiliza! Hadi usiku disco watu wanavaa wanaishia kutupiga vikumbo tu kwa sababu hawaoni vizuri!
ReplyDelete