Ankal Salamaleko,

Hivi hawa wahusika wa hii sheli ya BP airport jijini Dar wako usingizini ? Yaani ni kawaida yao sasa kila tunapofika kutia wese na mikoko yetu wanakwambia wese kkwishnei. Yaani mafuta hakuna. Na hii ni mara kwa mara. Sasa kama biashara imewashinda si wafunge wachape lapa?

Yaani huu ni usumbufu kweli. Utakuta mtu unajipanga foleni kwenda kuweka mafuta, wafanyakazi wa hiyo Sheli wanakuangalia kwa dharau na baadaye wanabirua midomo kusema mafuta hakuna. Yaani wanaboa, we acha tu!

hebu wahusika walifanyie kazi

Mdau Uwanja wa Ndege wa Airport

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huu ni ujinga. Kama unaona hupati huduma unayotaka kwanini kila siku uende hapo halafuuje kulala mika huku? Peleka biashara yako kwingine au fungua gass station yako uweke mafuta kila siku....

    Vingine twaona huruma lakini vingine mwajitakia...Huduma mbaya hama kwa nini wang'ang'a nia hapo hapo?

    ReplyDelete
  2. baba sasa hiyo sheli ya bp inakujaje tena ndugu yangu?hizo zote mbili ni petrol station,kila kimoja nikituo cha wese.

    ReplyDelete
  3. Halafu Wakenya wakija wakichukua biashara mnashangaa... Mijitu bwana!!

    Mdau Boston, U.S.

    ReplyDelete
  4. Aiseee hawa jamaa wa hapo BP Airport ni wabovu sana, yaani kimsingi kama kuna petrol stationa ambazo zinatakiwa kufungwa na EWURA(Joka la Kibisa) ni hiyo ya hapo Airport. Tena shukuru Mungu siku hiyo haukukuta mafuta, ungekuta yapo ingekuwa taabu, coz wafanyakazi wa pale wana kiburi, nyodo as if mtu ukienda pale unaenda kukopa au kuweka mafuta bure, wanasahau kwamba ile ni biashara tena kwenye ulimwengu wa soko huria. Mimi nilikuwa mteja wao mzuri sana, lakini baada ya kuona changamoto zilizopo hazifanyiwi kazi nikaamua kutotumia huduma yao, hata ikitokea napita mitaa ile na gari yangu ipo fuel empty mpaka taa inawaka, sithubutu kuweka mafuta pale, nipo radhi nibebe kidumu nikanunue fuel kwenye any nearby Petrol station rather than going there.NAWASILISHA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...