
Dada wa kizungu akimlilia mbwa aliyegongwa na gari
Jumapili ya Pasaka Kijitonyama, Dar es salaam
Hei Issa
Licha ya kuwa kuna Mbwa wengi wanakufa na kuishi maisha ya taabu sana na wala haiwi habari, lakini hii ya Mbwa huyu wa Mzungu inashawishi.
Tukitokea kanisani St Peters siku ya Jumapili ya Pasaka tr 24.04, kwa mbali nikiwa ndani ya gari langu, mkabala na Kijiji cha Makumbusho, niliona kitu kimegongwa na kiko chini ya gari Land Cruiser V8 ya Polisi, huku gari hiyo ikiwa imepunguza mwendo; nilipokaribia, kwa pembeni pia nilimwona mdada wa kizungu (utaifa sijaufahamu) akilia huku mikono iko kichwani.
Nilipokaribia zaidi, na magari yalipopungua na lile na polisi kusonga mbele, niligundua ni mbwa alikuwa amegongwa na gari. Yule mdada wa kizungu ghafla naye alikimbilia barabarani na kuanza kumpetapeta na kuendelea kulia kwa sauti "Oh God, Oh God". Hapo ndipo nilipojua kuwa alikuwa ni mbwa wake. Ilibidi magari yasimame kwa muda, mana yeye (kama anavyoonekana kwenye picha) alichuchumaa chini katikati ya barabara bila kujali magari yaliyokuwa yanaenda na kurudi.
Hali ya mbwa yule ilikuwa mbaya, alikuwa akitoka damu kichwani. Madereva taxie wa maeneo ya Makumbusho walienda kumsaidia. Licha ya kuwa ni mbwa, lakini ukianisha mapenzi ya mnyama huyu ambaye ni rafiki mkuu wa binadamu, na hasa asili ya wenzetu wazungu na wanyama kama mbwa na paka, kwa kweli nilimwonea huruma. Nilichukua picha hii, nikaendelea na safari yangu, sikujua kilichoendelea baada ya pale.
Mdau Edmund


mdau siyo tabiya nzuri ya kupiga picha watu osiyo wajuwa mama wakizungu anayo haki ya kukuweka korokooni vilevile huwezi juwa kazi iliyomleta bongo unaweza kumfukuzisha kazi au kumtiya matatani hata kuhatarisha maisha yake tuheshimu privect ya mtu
ReplyDeleteWazungu wanathamini mbwa zaidi kuliko binadamu. Waswahili hilo ni geni kwao, mbwa ni mnyama tu!!
ReplyDeleteAcha ushamba wewe mtoa maoni wakwanza. Picha ni kitu cha kawaida kuchukua, wako nchini kwetu lazima tuchukue matukio yanayotokea barabarani.
ReplyDeletemdau wa kwanza sijakuelewa, nadhan unachanganya mambo.
ReplyDeleteYah , kwa kweli hata mimi binafsi picha hii imenihuzunisha sana.
ReplyDeleteKwa kweli kuna uhitaji wa kuwajali viumbe hawa tunapoendesha magari yetu, madereva tujaribu kufikiria kitu UHAI, kila kiumbe kina haki ya kuishi.
wewe Anonymous 08;0300 AM kwa upande wako umetupa somo juu ya hilo ulilo ongea, pia mdau Edmund katupa somo pia juu ya hii hali, kwa hiyo tunawashukuruni wote. Ahsanteni.
Huyu mzungu amenikumbusha mbali sana, Kuna siku mbwa alikuwa amebebwa kwenye tela, baiskeli ya nyuma ikagonga lile tela na yule mbwa akadondoka, hii ilikuwa ni kwenye mataa ya kuongozea magari..... heeeee taa zilisimama, kila mtu alikimbilia kwa yule mbwa, akabebwa, watu wakalia, akarudishwa kwenye tela lake na taa ndio zikawaka......
ReplyDeleteWe mdau wa kwanza hii si mara ya kwanza kuona watu waliopigwa picha bila ridhaa yao kutokea kwenye vyombo vya habari..Ajali zote tunazoonaga humu, kwenye magazeti au tv?huwa wanaombwa kupigwa picha...??au kwa sababu huyu mzungu?alafu ni "privacy" siyo "privect".
ReplyDeleteYaani, hakuna mnyama mwenye upendo wa dhati kama mbwa, mimi nilikuwa hakimu wa wilaya fulani TZ, mbwa wangu alikufa kwa tatizo la minyoo maana nilichelewa kupata dawa, yaani siku naletewa habari nilikuwa chamber nasikiliza kesi, nilianza kutokwa na machozi na nikashindwa kuendelea na kesi, alikuwa amenizoea kiasi kwamba usiku nilipokuwa nachelewa kufika alipokuwa akisikia gari langu kwa mbali utamkuta yuko pale kwenye kona ya barabara ya kwenda nyumbani ananisubiri na analisindikiza hadi ahakikishe nimeshuka na kuingia ndani. Alikuwa ananipenda kuliko hata mwenza wangu. Yaani we acha tu, nimekumbuka mbali.
ReplyDeleteKisheria hakuna mtu anayeruhusiwa kuweka picha ya mtu kwenye internet bila kupata ruhusa kutoka kwa mwenyewe. Nafikiri mdau wa kwanza ndivyo alivyokuwa anamaanisha. Mwenye jukumu hapa na ambaye anaweza kuchukuliwa hatua ni Michuzi, siyo mpiga picha.
ReplyDeletemtoa mada wa kwanza kauzi, nafikiri labda hajaona umuhimu wa pcha hii au hana uwezo wa kupambanua mambo. Wanyama wana haki ya kuishi na ndio maana hata sasa Tz tuna mashirika yanashoghulika na Animal rights and Welfare. Hata Waziri Magufuli aliwahi kuzungumzia hili swala. Tuwajali wanyama wa Tz.Kama ntamuuzi mtoa maoni wa 1, aniwie radhi
ReplyDeleteMdau asemaye
ReplyDeleteWazungu wanathamani mbwa zaidi kuliko binadamu
Amenishtua sana na pia pengine kaniamsha kutoka kwenye usingizi,Kwani miye nina mke mzungu na pia nina mbwa
Wakatabahu
Ama sijaona mantiki ya wewe anony wa kwanza kujenga wasiwasi na kwamba amekosea kuleta hii habari what matters it is a news as other news.mbona unatujengea nidhamu ya uwaoga bila mantiki vipi bwana mzungu au mgeni hiyo sio sababu tunachotaka habari na yenye msingi.Wala hajabeza mtu hapo sasa suala privacy linakujaje tena.Kama nami sijui zaidi basi mnisamehe na kunielewesha wadau.
ReplyDeleteHuyo dada wa kizungu ni mengi yanayomliza.Si vizuri kutowajali wanyama na inewezekana huyo mbwa anafanana pia na wa kwake aliyemuacha nyumbani kwao ambaye huwa anafanya naye mapenzi kwani hayo ni moja wapo ya matumizi ya mbwa kwa baadhi ya wanawake wa kizungu.Nyie waoneni wakija huku kwetu lakini mambo wanayoyafanya kwao hata mtu ambaye hajaenda hata darasa la kwanza kwetu hawezi kuyafanya.
ReplyDeleteMimi mwenyewe nimelia mbwa wangu 'Blackie'alivyokufa Bongo. Nilikaa naye miaka minane halafu kafa kipuuzi. Huyo mbwa alikuwa mlinzi wangu, mfano, alinizuia nisikanyage nyoka aina ya kifutu siku moja. Alikuwa rafiki. Ni kweli kama hapa USA mzungu anakuwa na mbwa badala ya mtoto, huwezi kujua uhusiano wao ni nini. Pia ni kweli kuwa Tanzania tunamwona mbwa ni mnyama tu. Natoa pole kwa huyo dada. Natumaini Vet aliweza kumsaidia mbwa wake apone.
ReplyDeleteTSPCA ipo, wafanyakazi wa TSPCA wapo, mishahara wanapata, lakini kazi wanayoifanya haionekani?
ReplyDeleteSi waafrika wengi wanapenda wananyama wakufugwa kama mbwa na paka...
mdau wa watatu unayeita watu washamba pls tuwekee picha ya dada au mama yako akiwa jikoni au akichuma mboga halafu tutajuwa nani mshamba wewe au mdau no 1 kuna mweziyo anazungumziya haki ya wanyama bongo hakuna haki za binadamu itakuwa myama kisheriya huwezi kumpiga picha mtu ambaye hana kosa kisheriya ikiwa mbongo au mzungu au muhindi hishimu utu wa mtu jee ikiwa anatafutwa au anamtafuta mtu si ushaigiliya kazi za watu umbeya utatuponza kazi zamapaparazi
ReplyDeleteSote twajua kuwa waislam wengi hawana upendo wa mbwa, na wengi husema kuwa mbwa ni najis.Ukweli ni kwamba katika Quraan mbwa wametajwa vizuri na mara nyingi...kwa mfano surat kahf (18),hadithi nyingi za chuki za mbwa zilianzishwa na Abu Hurayra, aliitwa hivyo kwa kuwa alikuwa na paka, na anajulikana kuwa aliwachukia sana mbwa (na pia wanawake).Huyo jamaa alikuwa ni mmanga wa Yemen na jina lake ni Abd al-Rahman ibn Sakhr Al Azdi
ReplyDeleteWakatabahu
A human being can betray his or her Boss, but a dog will never do that. It will always love and respect you as a friend or a Boss. Hiyo ndo sababu kubwa ya wenzetu kupenda mbwa kiasi hicho. Sisi Binadamu hata rafiki yako mkikwaruzana kidogo tu basi tutaanza ku gosip na kuonyeshana nani zaidi. Zaidi ya hapo mbwa ni kiumbe ambaye naye ana feelings kama sisi, akiumia naye anasikia uchungu na ndo maana akipigwa au asipomwona muhudumu wake kwa muda huchanganyikiwa na kufanya awe nervous. Sasa kwanini na sisi binadamu tusiwe na feelings au orho za hurumu kuwalilia au kusikitika wanapopata majanga kama hayo.
ReplyDeleteKalenga Boy.
Ref. mdau wa hapo juu( Thur Apr28.08:08:PM 2011). Dini ya Kiislam haikazi mbwa au kuwa fanya waumini wachukie mbwa. Mwislamu anaruhusiwa kabisa kufuga mbwa mradi afuate taratibu za kiislamu za ufagaji wa mbwa. Pia waislamu tunahimizwa sana kuwa na huruma sana kwa viumbe wote wa mwenyezimungu ikiwa ni pamoja na mimea pia. Na ndo maana hata kukata mti au kuua sisimizi bila sababu muhimu ni kosa kubwa kwani Allah Subhana wataala has Created the universe in balance. Mimi kaka Muislamu ninafuga Mbwa na kuwa penda sana.
ReplyDeleteKalenga Boy.
Brother Kalenga Boy
ReplyDeleteAsalaam aleykum
Ikiwa umefikiri kuwa nimesema dini ya kiislam hairuhusu kufuga mbwa,naomba samahani nimeshindwa kujieleza fasaha. Nimesema kuna waislamu wengine,yaani watu, na siyo dini ndio wanaochukia mbwa.Wasema kuna utaratibu wa kiislam kuhusu ufugaji wa mbwa,tafadhal nifahamishe aya na juzuu au hadith. Allah yebarik
Wakatabahu
Wee mdau wa kwanza hapo juu, na wengine (nadhani ni wewe tu!) usijifanye mjuaji. Nitajie sheria ipi na ya nchi gani inayokataza kupiga picha mtu bila ridhaa yake in public???? Ridhaa???? na wewe uko public area nami nikuombe ridhaaa?? Gimme a break. Kama uko mita tatu nje ya nyumba yako ujue uko katika public domain. Nakupiga picha nawe hufanyi lolote. Upo hapo wewe na wenzio? Usitake kudanganya watu hapa!!! Ebo. Hebu kwanza soma hiyo (kama unajua ung'en'ge)
ReplyDeleteThe tort of invasion of privacy likely would apply in this situation. Invasion of privacy refers to a collection of causes of actions designed to protect a person’s right to be let alone. Born in the late nineteenth century, this tort actually consists of four different types: (1) intrusion, (2) public disclosure of private facts, (3) false light, and (4) appropriation.
Intrusion applies when a tortfeasor unreasonably intrudes on a person’s physical privacy by following them, photographing them, or opening their private mail. Public disclosure of private facts occurs when a person discloses material of a person’s personal private life that is not of legitimate concern to the public. This tort differs from defamation, because the tortfeasor can be sued for the disclosure of even true information. False light refers to placing a person in a false light in a manner that would be highly offensive to a reasonable person. Let’s say a television program ran a program on the problems of street prostitution and featured stock footage of a woman walking down the street. That woman may have a claim for false light, claiming that the placement of the footage falsely implied she was a prostitute. The final type of invasion of privacy is appropriation, which refers to the use of a plaintiff’s name or likeness for financial gain without permission.
Is it legal to take photos of people without asking?
In public places where there is no right to privacy, yes you can. The same applies in private places where you have the permission of the landowner or the landowner has stated no restrictions on photography. However photographing someone without asking their permission can cause a lot of trouble if not handled sensitively. If someone does not want to be photographed it is best to respect their wishes unless there is an overriding reason not to. Most people in most circumstances respond well to friendly explanation, especially if you show them the photo. Nevertheless some will object that you have violated their rights in some interesting way, and it's best to have the explanations ready.
'You can't take my photo without permission'. Oh yes you can, usually. Point to the CCTV cameras and wave, they never asked either. Of course it is perfectly understandable that individuals may feel singled out and perhaps intimidated, frightened or angry not to be in control, but it's not a legal point.
ReplyDelete'You have violated my copyright'. This is in no sense true. There is no copyright in the human face or form, and copying would anyway mean cloning them, not creating an image. An image of a person is copyright of the photographer.
'You have violated my privacy'. Legally this is unlikely to be true. There is no right to privacy in public places as a rule. There is a right to privacy in private places and in public places where there is a reasonable expectation of privacy (eg public toilets), but how extensive this is depends on circumstances.
In private places that are open to the public, permission of the landowner is usually sufficient to be able to photograph visitors and staff. However a recent court case upheld a right to eat a meal in a restaurant in privacy even though the restaurant owner had consented to the photography, because in the court's view it was a customer's normal expectation not to be photographed there. If in doubt, this is probably the question to ask yourself.
'You have violated my human rights'. Police seem to sometimes object to being photographed on the grounds that their 'Human Rights' are being violated. This really means the same thing as 'privacy' and there is none in the street as the presence of CCTV and police photographers shows.
The Human Rights Act 1998 recognises a human right to expect privacy wherever privacy is normal, eg in the home. So photographs taken where privacy may be expected require permission of the subject. EG photographs taken from public places that depict someone within their home in a situation where they expect privacy, for instance through a window using a telephoto lens, will be actionable.
'You are harassing me'. Photography can indeed constitute harassment, but for an act to constitute harassment requires deliberate acts of harassment on at least 2 separate occasions. The complainant may then seek a restraining order from the court.
Harassment is potentially an issue for paparazzi in their pursuit of celebrities, but equally a restraining order has been used to suppress inconvenient photography by npower at Radley lakes.
'You need a model release'. Model releases are not necessary for anything except photographs to be used for commercial purposes. For editorial or artistic purposes they have no relevance unless you intend defaming the subject and need them to make a contractual agreement not to sue you for libel. If you intend selling the image for marketing or advertising use that implies endorsement by the subject, then yes, you need a model release (or rather, the advertiser does).
'You have violated data protection law'. Superficially this seems correct as the Data Protection Act does indeed prohibit the recording of data that identifies an individual. A photograph certainly qualifies and the DPA certainly applies to CCTV monitoring, ID photos etc. However the DPA Part 1 Section 3 specifically exempts as a 'special purpose' photographs or other data recorded for journalism, or for artistic or literary purposes.
PAPARAZZI
mdau wa kwamza ametoa ushauri mzuri kwa kurumia sheria ifuatayo.Photography tends to be protected by the law through copyright and moral rights. Photography tends to be restricted by the law through miscellaneous criminal offences.
ReplyDeletePublishing certain photographs can be restricted by privacy law.It is an offence under the Counter-Terrorism Act 2008 to publish or communicate a photograph of a constable (not including PCSOs), a member of the armed forces, or a member of the security services=huenda na huyu dada akawa mmoja wao na pia kwa sheria hii.
A right to privacy exists in the law, as a consequence of the incorporation of the European Convention on Human Rights into domestic law through the Human Rights Act 1998. This can result in restrictions on the publication of photography.
Ila general law ni hii:
Members of the public have virtually no privacy rights when they are in public places. Basically, anyone can be photographed without consent except when they have secluded themselves in places where they have a reasonable expectation of privacy such as dressing rooms, restrooms, medical facilities, or inside a private residence.
kwa kumalizia
Photographing accident scenes and law enforcement activities is usually legal.
taalam wa mapicha
Nice explanation iro of the laws cited.unfortunately the laws cited i.e counter-terrorism act,2008 and humna rights act,1998 are UK Statutes and not applicable here in Tanzania. The only law which is applicable here in Tanzanis is the law of tort by virtue of Judicature and Application of Laws Act (JALA) Chapter 358 R.E.2002 which allows inter alia application of Common Law in Tanzania.
ReplyDeleteWatu wote mnajiongelesha kuhusu picha mtu mwenyewe hata haonekani tunaona manywele kuweni na akili kidogo sio kupenda kubisha kusiko na maana, so far tunaona sura ya mbwa. HONGERA CATHERINE NA WILLIAM MUNGU AWAPE MAISHA MEMA.
ReplyDelete