Mchungaji Ambilikile Mwasapila akipanda gari ili aondoka katika kijiji cha Samunge, mkoani Arusha juzi, kwenda Babati kuhudhuria mazishi ya mtoto wake,Jackson Mwasapila aliyefariki katika Hospitali ya wilaya ya Babati.
Picha na Mussa Juma

Mchungaji Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge Loliondo, juzi jioni aliondoka hapa kwenda Babati, Manyara kuhudhuria mazishi ya mtoto wake huku safari yake hiyo ikiratibiwa na Serikali na akipewa ulinzi mkali wa maofisa usalama na polisi.

Aliondoka Samunge saa 12:20 jioni na gari la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwa na maofisa hao wa usalama, polisi na wasaidizi wake. Kabla ya kuondoka Samunge, watu mbalimbali walikuwa wamejitolea kumpatia usafiri mchungaji huyo lakini walizuiwa kutokana na sababu za kiusalama.

"Tulikaa kama kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, tukaona ni busara tuchukue jukumu la kumsafirisha Mchungaji hasa kutokana na sababu za kiusalama," alisema ofisa mmoja mwandamizi wa serikali wilayani hapa.Alisema mchungaji huyo atalindwa akiwa msibani na atakaporejea Samunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. pole sana kwa msiba mungu akutie nguvu

    ReplyDelete
  2. Si nilishawashauri kuwa kwa vile watafiti wamesema dawa ilishatumika kabla ya babu hivyo watu wajichimbie wenyewe wanywe na watapona. Sasa mbona bado mnamuendekeza? Kachimbeni dawa mnywe mtapona acheni kusongamana hapo kwa babu!!!

    ReplyDelete
  3. Kwani adui zake ni akina nani? yeye anatibu watu wenye magonjwa sugu, kwa mtazamo wangu ni kuwa mtu huyu anatakiwa kuwa na marafiki wengi zaidi. Maana hata kama leo mimi ni mzima wa afya naweza kuugua kesho au hata leo hii ndugu yangu fulani atapata tiba.

    Sioni sababu ya serikali kujitolea ulinzi kila siku hapo kwake na leo hii serikali inatoa magari na maaskari wa kumlinda utadhani yeye ni mkuu wa nchi. Hii naanza kuona kama imekaa kisiasa zaidi.

    Madaktari bingwa pale Muhimbili hawana usafiri wa serikali. Inakuwaje kuhusu huyu. Kwani atauawa na nani? Tena kwa kosa lipi ililofanya kwa jamii.

    Sasa naanza kuwa na maswali mengi kuhusu huyu babu na tiba yake, zaidi ni ushiriki wa serikali katika huduma yake.

    ReplyDelete
  4. Hivi hii dawa ni ya serikali? Inamtumia tu babu? Maana haya maelezo siyaelewi elewi, hebu nidadavulieni waungwana.

    ReplyDelete
  5. Mhhhhhh kweli Tanzania yetu. Yaani huyu Babu sasa amekuwa wa kupewa ulizi mkali !!! kulikoni??? Kama alivyosema mwenzangu hapo juu Madaktari kwenye Hospitals mbali mbali hawana usafiri, Wagonjwa mahututi hawana usafiri ( Ambulance) Jamaani tunaelekea wapi??? Au Babu yuko kwa ajili ya kuwawakilisha watu Fulani ( Wakubwa kwenye Serikali yetu) Hii inasikitisha sana. Hizo resorces zingetumika kusaidia wananchi wenye kuhitaji misaada ya ukweli na sio Babu kwenda kuzika mtoto wake.

    ReplyDelete
  6. cant agree with you more mdau wa tatu!

    ReplyDelete
  7. Babu amekuwa celebrity! ni mtu muhimu sana katika jamii! maadau ni wale wenye hospitali binafsi kwani wamepoteza wateja sasa hivi! hivyo ni hatari kumwacha babu asafiri peke yake wanammaliza kabla ya kumaliza kazi yake.

    ReplyDelete
  8. Tunawaogopa wanaodai kumuombea afe kumbe wanapanga njama za kumdhuru.

    Ahsante serikali kumlinda Babu. Mapato ya baadhi ya wanaodai kuombea wagonjwa yamepungua.

    Penye rizki hapakosi fitna

    ReplyDelete
  9. jamani watanzania tusiishi ivi, kumbukeni kuwa ata huku nchi za wenzetu watu wanaogundulika kuwa na vipaji au uvumbuzi wa jambo fulani uwa wanalindwa nakuendelezwa hili kufikia malengo yao..leo hii huyu babu ametokea kwetu na ameponyesha watu walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali tena kwa nji ya ajabu tu na kwa gharama nafuu zaidi bila kuchoka. Sasa serikali kumpa usafiri wa kwenda kumzika mtoto wake imekoa kosa jamani!!? tukumbuke kuwa naye ni binadamu pia amesaidia ndugu zetu wangapi??!!
    Leo hii tunamponda serikari eti kisa imejitolea asafiri na ulinzi kwa babu kwenda kuzika, mbona hatokuongea pale ambapo serikari ilitoa BILIONI TATU kuwaleta brazil wakatu watanzania wanalala na njaa!!! hio bilioni tatu ingenunua magari kwa madaktari wangapi!!
    Tuwe na utu sometimes.

    ReplyDelete
  10. Namuunga mkono mtoa maoni wa pili hapo juu. Wanaosema dawa hii ilikuwa inatumika mwanzo kabla ya babu, waende wakachimbe wanywe ili foleni ipungue.

    Sisi wenye imani tuendelee kwenda kwa Babu. Na wale mnaoendelea kuomba Mungu wakati dawa imeshakuja mnnaomba ili mungu afanye nini?

    Mungu kesha jibu nendeni mkanywe dawa

    ReplyDelete
  11. Watu tusiwe wajinga jamani huyu babu anatoa huduma zinazoaminika kwa wanaohitaji,kama hutaki usiende kwake,na sioni sababu ya kushangaa babu
    kupewa ulinzi ni kweli kwa sasa lazima maisha yake yatakuwa hatarini maana waganga wengi matapeli na baadhi ya wahubiri matapeli wanaona wanapoteza wafuasi kwa sababu ya huyu babu,na kumekuwepo na ushahidi wa wazi wazi kuonyesha baadhi ya watu au vikundi vukimpinga babu.Kama tunavyojua Tanzania yetu kumtoa mtu roho ni kitu rahisi sana na watu wako tayari hata kugharamia ili kummaliza mtu kama babu.Acha babu apewe ulinzi, tunashindwa kulalamikia mabilioni ya benki kuu yaliyoliwa na akina Liyumba na mwisho anafungwa miaka miwili.tunalalamika ulinzi mdogo tu anaopewa huyu babu,huu ni upuuzi mtupu.Wacheni babu alindwe ili ahudumie wananchi wenye matatizo.
    mdau London.

    ReplyDelete
  12. Mimi simchukii babu hata kdg pia huduma yake juu kuna watu wamepona ila kitendo cha serikali kumpa ulinzi walaghi hakiniingiii kbs akilini km wadau wenzangu juu.Babu ni m2 wa Mungu anaogopa nini???? MUngu anasema ukikaandani yangu nani nikiwa ndani yako kila ktu kin akuwa sawa hata maadui wanakuogopa sasa babu ulinzi wa nini????????serikali yetu bwana mi sometymz siiielewi hata kdg kila siku wanajipya ndomana chadema wanawaendesha. Wanatumia mapungufu yao km haya kuwavuruga

    ReplyDelete
  13. Babu lazima alindwe kwa sababu wengi mmeonyesha chuki naye tena hata kwa comments zetu.Pia tumeona malalamiko ya madaktari na maaskofu ambao mapato yao yameshuka kutokana na watu wao kukimbilia tiba ya babu.

    Kwa taarifa yako, babu ana maana zaidi kuliko hao madaktari wenu unaosema hawana usafiri wakati wako kuwanyanya wagonjwa kila kukicha na kuwakimbilia matajiri na wenye vyeo kuwatibu.Babu ameongeza mapato kwa watu binafsi, kwa serikali na kwa kanisa, hivyo ni muhimu apewe ulinzi.Kwani unaposema yeye ni raisi anapewa ulinzi kwani rais yeye ana maadui gani?Kwani yeye si binadamu tu kama wewe?yeye ameleta maendeleo gani zaidi ya kuwanuifaisha marafiki wanaopeana nao vyeo.

    Koma kabisa kumkomalia Babu ambaye ameiendeleza lolyondo kwa kasi hadi barabara inajengwa na ushuru unalipwa kwa wageni wanaoingia.Ninyi mmeka mnasaga matako tu na kuikandia serikali inayofanya kazi yake vema.Acheni chuki zenu za udini.Babu ametukuka ametukuka tu hata msemeje imekula kwenu period.

    ReplyDelete
  14. Ninyi mnaompinga babu na kumbeza mmekosa maarifa kabisa. Mungu kupitia Babu ameleta dawa inayoponya watu kwa bei poa. Halafu kupita Babu serikali imepata mapato mengi bila hata ya ku-plan kabla. Biashara inayofanyika hapa (revenue) ni kubwa na ni endelevu.

    Ndio maana kwa sasa Serikali ni Mbia kamili wa Babu. Yaani Manufaa ya Babu ni Makubwa sana na kama tungekuwa na akili watanzania tungenyamaza kimya na kumwacha Mungu atuinue kupitia huyu Babu. Bado Mataifa ya Ulaya na Marekani wanakuja. Babu alionyeshwa watakuja.

    Yaani inatakiwa tukae mkao wa kumshukuru Mungu tu na kujiandaa kunufaika.

    MUNGU AMETUPA DAWA HALAFU IMEKUWA NI MRADI HALALI KABISA KWA KANISA, SERIKALI, WASAFIRISHAJI, MAKAMPUNI YA SIMU, BIASHARA ZA VYAKULA, TRA YAANI NI BARAKA KWA KWENDA MBELE.

    HALAFU SASA NI MAPATO ENDELEVU. BABU ALINDWE KWA NGUVU ZOTE. TUACHANE NA HAO MITUME WANAOOMBA WATU WAFILISIKE!

    Mchungaji (Pentecostal)
    Dar es salaam

    ReplyDelete
  15. hihihi dah kweli wabongo tumecha sasa tunashindwa hata kufikiri eti babu dah inasikitisha sana mimi naomba serikali iwangalie sana wabongo wameshachoka sasa wakimaliza uzushi wa huyo babu mm naona wabongo watakuja kufanya kitu kibaya sana nchini wa2wamechoka kweli ila namuomba MUngu lisije likatokea balaa kubwa bongo maana inasikitisha serikali nawambia wa2 wamechoka mke tayari kupambana nao ukimaliza huo uzushi wa babu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...