Sehemu ya umati wa wakazi wa mkoa wa Kagera walivyokuwa wakisherekea sikukuu ya pasaka kwenye ufukwe maarufu uliko kando ya ziwa victoria eneo la hoteli ya Spice, eneo hili huwavuta watu wengi toka maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera hasa wakati wa sikukuu ama mwishoni mwa wiki.
Afisa uhusiano wa benki ya CRDB Bi. Rose Mollel akiwasilisha mada wakati wa kikao kilichoandaliwa na benki ya CRDB cha kuwahamasisha wateja wake wakubwa hasa wanunuzi wa mazao wa mikoa ya Kagera na Kigoma wanaotumia benki hiyo kuopata fedha za kununua mazao toka kwa wakulima kufungua akaunti za fedha za kigeni, kushoto ni Meneja wa benki ya CRDB tawi la Bukoba Bw. Emmanuel Chaburuma.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani ya mkoa wa Kagera Bw. Wiston Kabantega akifafanua jambo alipokuwa akiongea na madereva wa magari yanayobeba abiria na mzigo juu ya taratibu ambazo inabidi madereva wazifuate ili waweze kupata leseni mpya za udereva. Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...