Na Woinde Shizza,Arusha
CHAMA cha soka mkoani Arusha(ARDF) kimewateua makocha wawili ,Madaraka Bendera na Ally Mohammed kubeba jahazi la kukinoa kikosi Cha timu ya mkoa wa Arusha maarufu kama “Mt. Meru Warriors”katika michuano ya Kili Taifa Cup inayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo mwezi ujao.
Akihojiwa na Mwanahabari wetu kuhusu maandalizi ya timu ya mkoa wa Arusha,katibu wa chama hicho,Adam Brown alisema kuwa chama hicho kimemteua aliyewahi kuwa mchezaji wa klabu ya Simba hapa nchini,Madaraka Bendera kuwa kocha mkuu akisaidiwa na Ally Mohammed ambaye ni kocha aliyeipandisha daraja katika ligi kuu klabu ya JKT Oljoro ya mkoani Arusha kutokana na vigezo mbalimbali walivyonavyo kikiwemo cha uzoefu.
“Chama cha soka mkoani Arusha kimewateua Madaraka Bendera kuwa kocha mkuu akisaidiwa na Ally Mohamed kukinoa kikosi cha Mt,Meru Warriors kutokana na vigezo mbalimbali ikiwemo experience(uzoefu) walionao”alisema Brown Hatahivyo,Brown alisema kuwa tayari timu hiyo imesahaanza mazoezi yake ya kujiandaa na michuano hiyo ya Kili Taifa Cup katika viwanja vya shule ya sekondari ya Arusha Meru ulipo wilayani Arusha.
Aliwataka wakazi wa Arusha wakiwemo viongozi wa serikali mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu hiyo huku akisisitiza kwamba timu hyo siyo mali ya ARFA bali ni ya wakai wote wa mkoa wa Arusha.
“Wakazi wa Arusha watambue ya kuwa hii timu siyo mali ya ARFA bali ni mali yao,hivyo nawasihi wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao”alisisitiza Brown

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...