Hiki ni kidokezo kifupi tu cha yale mengi yaliyomo ndani ya film mpya ya kikatuni iitwayo "Manzese". Ushauri unakaribishwa ili kuweza kuiimarisha na kupata wasambazaji. Unaweza kumwandikia moja kwa moja Dr. Boniface Mhella ambaye ni mtunzi wa Story na Producer wa Filamu nzima
( bonn-j@hotmail.com).


mie nampongeza huyu jamaa kwa kutengeza hii filamu ya animation nimependa wahusika amewachora vizuri kiafrika kabisa. pia mandhari aliyotumia pia yanaendana maeneo ya yenyewe ya jina la hii filamu . maudhui aliyokusudia kuyatoa kwa jamii ni mazuri na yanaelezea uhalisia wa maeneo ambayo ameyakusudia. ila tu katika sauti kwa baadhi ya wahusika naona kama haziridhishi kwani zimekua kitoto sana yaani kama mtu anaejifunidisha kuongea kiswahili na pia katika vitendo vya wahusika pia ni taratibu zaidi . ila kwa ujumla nimpongeze amejitahidi maana siwezi kujua pengine ndio kazi yake kwanza natarajia kila akiendelea atatoa kazi bora zaidi
ReplyDeletesafi sana mr Boni...kanzi nzuri sana
ReplyDeleteKazi nzuri sana na unique............good job Sir.
ReplyDeleteMwenyewe anataka maoni yenu ili kuboresha kazi yake ninyi mmeng'ang'ana na 'gud Job'. Hiyo itamsaidia nini? Dr. Bon, ushauri wa mdau wa kwanza ni mzuri, hususan upande wa sauti. Pia ukitumia sauti za watu mashuhuri (Bongo celebrities) itakusaidia zaidi katika mauzo.
ReplyDeleteHongera kwa kuanzisha kitu kipya Bongo, wahindi wamuza sana hizi animation na inaonekana kazi unaiweza!
Last time niliongelea sauti na leo narudia yaleyale, kweli sauti si lazima iwe ya taratiiiibu namna hiyo kama mtu anakata kauli. Zifanye ziwe halisia kama mtu anaonea kawaida. Hata motion za katuni ziwe tu kama kawaida sio slooow, sauti ya kike bado ni ya mwanaume rekebisha hivyo mbona kina shrek,the simpsons au hata katuni za watoto zilizotengenezwa zamani wanaweza? Voice overs sio lazima zitumike za celebrities kama mdau mmoja laivyo shauri, washirikishe watu wenye kuweza kutamka kiswahili vizuri na jinsia zinazo husika basi, au kama vipi tuma bongo ingiza sauti wakurudishie otherwise utafika mbali sana geza geza mpoooo!
ReplyDeleteKazi nzuri na idea nzuri sana,nachangia tu ushauri kuwa jitahidi kurekebisha speed ya sauti ili ionekane kama kweli watu wanavyoongea isonekane kama mashine,yaani ionekane live kama zilivyo sinema nyinginezo za annimation,tuko pamoja na wewe.
ReplyDeletemdau Tokyo,Japan.
Hongera Dr. Boni kwa kazi nzuri, sijawahi ona animation kutoka tz, labda ni mimi niko nyuma. Ila kama wengine walivyoshauri, hizo SAUTI inabidi uzifanyie maarifa. Huyo aliyekataa mkono wa mwenzake anaongea kama anaimba (kama filamu za bongo za zamani za wale wazee wenye pesa walivyokuwa wanaongea). Anyway kiuhalisia sidhani kama kuna mtu anayeongea kiswahili hicho. Sijajua audience ni nani, lakini hata kama ni watoto pia hiyo sauti bado ni ya kurekebisha. Napingana na mdau mmoja hapo kuhusu sauti za celebrities, sidhani kama ni lazima, unahitaji sauti za watu wanaojua kuongea kiswahili kilichonyooka maana kuna hao celebrities bado wanachanganya 'R' na 'L' kwenye matamshi wanaweza haribu zaidi. Ila kwa kifupi kazi nzuri na hongera.
ReplyDeletehuyu jamaa kanifanya nivutiwe sana na hii movie anayoiandaa its a very good idea bro..ila ushauri wangu mimi ni kwamba kwanza..SAUTI watu wanaongea taratibu sana inachukuwa muda mwingi kwa mtu mmoja kumaliza sentensi yenye maneno mafupi, i mean its too slow, PILI hata pia utembeaji wa watu its not normal inakuwa kama umewaweka kwenye slow motion hawatembei kama kawaida jaribu kuangalia animation movies za america jinsi wanavyotengeneza just to get more ideas..hayo ni mawazo tuu ila nakupa hongera sana kwa kazi yako hii kaka ni nzuei nimeipenda tumechoka na movie za kibongo...mdau kutoka..DALLAS,TEXAS..U.S.A
ReplyDeletewatu wameshika sauti taratibu-huyu bwana mkubwa hajakusudia ziwe ivyo ila kuna matatizo katika editing na software anazotumia transfer bit rate ni mbaya ni kama vile uwe na processor ndogo kisha ucheze football game.so huenda software anayotumia ni za bei rahisi-bora tumia SONY VEGAS.
ReplyDeletecha pili huenda anajaribu sauti iendane na watu hataki ikosane sasa katika edit-anakua anakisia asipoteze character's action na sauti yake ikaingia kwa mtu mwengine-badala yake inakua very slow kama gari lililojaza SHEHENA LINAVONUNG'UNIKA-NAFIKIRI anahitaji Audio editor-kazi nzuri-kama mtoto sara.
MTAALAM WA EDITING