Mama na Baba Afrika
Da' Chemi katika costume ya kwanza kama Ms. Thelma, David Bowden kama Aaron Douglas na kijana Zaccai kama Rudy the Paper Boy.
Da'Chemi na Comaseen Lawrence. Hapa ni katika costume ya pili
kama Ms. Thelma. Comaseen aligiza kama Ethel Waters.

Wiki iliyopita Da’Chemi Chemponda aliigiza tena kama Mama Afrika katika mchezo wa Kuiigiza The Harlem Renaissance Revisited, katika maonesho Chuo KIkuu cha U-Mass Boston. Watu walipenda sana jinsi Da’Chemi alivyokuwa anaongea kiswahili na kiingereza kwa lahaja ya kiafrika. Katika mchezo Mama Afrika analilia wanae waliochukuliwa kuwa watumwa katika nchi za Marekani. Lakini Baba Afrika anamwambia kuwa hao watoto watafanya makuu duniani.

Pia Jumanne alikuwa katika TV show Body of Proof ambayo stelingi ni Dana Delany. Inaonyeshwa kwenye ABC. Da’Chemi alikuwa 'extra' na aliigiza kama kama karani kwenye deski ya mapokezi kwenye kituo cha polisi.

Globu ya Jamii inampongezake Da’Chemi kwa kuendeleza libeneke la uigizaji huko ughaibuni na kwa juhudi zake iko siku atatoka tu. Tunamwombea hilo kwa udi na uvumba...
Habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. UBARIKIWE

    ReplyDelete
  2. Hongera Dada Chemi. Moyo wa sanaa unayo. Utafika! Kuna siku tutakuona na wewe kwenye Oscars! Keep it up!

    ReplyDelete
  3. Da Chemi naona mguu umeingia Hollywood. Karibu tutakusikia kwenye sinema kubwa kubwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...