Habari za leo Ankal,
Mi ni msomaji mzuri wa blog ya jamii, , lakini sijawahi kuchangia. Ila leo
naomba uniweke hadharani ili nitoe dukuduku langu kuhusu hivi vikombe.
kwa kweli inaniuma na kunisikitisha ninapoona hali kama hii ikiendelea
na watu tunashabikia na kufurahia. hebu tuchukuea kama dakika moja
hivi kufikiri na kutafakari ni nini hasa kinachoendelea. ufuatao ni
muono wangu.
Hii inaonyesha ni jinsi gani Watanzania tulivyokata tamaa, tunahaha
kutafuta suluhisho la matatizo yetu na tumebaki kuishi kwa matumaini
tuu. Kinachonisikitisha mimi ni kuwa hata wale wachache tuliobahatika
kupata elimu nzuri na kufunguka kitaaluma, elimu zetu hazijatusaidia.
Inasikitisha kuona jambo kama hili linatokea katika karne hii, watu
wanahadaika na serikali na vyombo vyake wako kimya tuu, viongozi
waliosoma na kuelimika ndo wanakuwa wa kwanza kwenda kupata vikombe,
ama kweli kua uyaone... Hii inanikumbusha enzi zile za Kinjekitile
wakati wa vita ya majimaji, haina utofauti. Kibaya zaidi ni kwamba
Serikali yetu pia imeshindwa kutusaidia sisi wananchi wake. Mpaka sasa
msimamo wa Serikali haujulikani ni nini kuhusu hili.
Haihitaji elimu kubwa na ujuzi wa hali ya juu. kwa nini Serikali (na
maanisha Wizara ya Afya) ikiwa imesheheni maprofesa na madaktari
bingwa wasingefanya jaribio rahisi tuu. Wangechagua wagonjwa kadhaa
ambao wamethibitika kuwa wanaumwa, kisha wawapeleke kwa babu wapate
vikombe halafu warudi na kuanza kuwaangalia afya zao kama kweli
wamepona au wanaendelea kupona au la, matokeo wangetueleza wananchi
ukweli, mwezi mmoja unatosha sana kumuangalia mtu kama kapona au vipi.
Lakini hadi sasa wizara imesema kuwa dawa haina madhara, ofcourse hata
ukichemsha majani ya mchicha hayana madhara, lakini huwezi kupona
(ingawaje kwenye mchicha unaweza kupata madini na vitamins kidogo).
Matokeo yake sasa ni kwamba watu wanakufa na wataendelea kufa na
wanaweza kufa wengi zaidi baada ya imani yao kuwa wamepona na kupuuzia
matibabu na taratibu na masharti mengine kulingana na magonjwa yao.
sijui tunakwenda wapi. Mimi binafsi nasikitika sana kuona bado
tunazidi kuwa kama mababu zetu waliombiwa ukioga haya maji risasi
haiingii mwilini...Tunakoenda si kuzuri.
Asante
--
Mtemi H. Miya
Dar es Salaam
Tanzania
Mi ni msomaji mzuri wa blog ya jamii, , lakini sijawahi kuchangia. Ila leo
naomba uniweke hadharani ili nitoe dukuduku langu kuhusu hivi vikombe.
kwa kweli inaniuma na kunisikitisha ninapoona hali kama hii ikiendelea
na watu tunashabikia na kufurahia. hebu tuchukuea kama dakika moja
hivi kufikiri na kutafakari ni nini hasa kinachoendelea. ufuatao ni
muono wangu.
Hii inaonyesha ni jinsi gani Watanzania tulivyokata tamaa, tunahaha
kutafuta suluhisho la matatizo yetu na tumebaki kuishi kwa matumaini
tuu. Kinachonisikitisha mimi ni kuwa hata wale wachache tuliobahatika
kupata elimu nzuri na kufunguka kitaaluma, elimu zetu hazijatusaidia.
Inasikitisha kuona jambo kama hili linatokea katika karne hii, watu
wanahadaika na serikali na vyombo vyake wako kimya tuu, viongozi
waliosoma na kuelimika ndo wanakuwa wa kwanza kwenda kupata vikombe,
ama kweli kua uyaone... Hii inanikumbusha enzi zile za Kinjekitile
wakati wa vita ya majimaji, haina utofauti. Kibaya zaidi ni kwamba
Serikali yetu pia imeshindwa kutusaidia sisi wananchi wake. Mpaka sasa
msimamo wa Serikali haujulikani ni nini kuhusu hili.
Haihitaji elimu kubwa na ujuzi wa hali ya juu. kwa nini Serikali (na
maanisha Wizara ya Afya) ikiwa imesheheni maprofesa na madaktari
bingwa wasingefanya jaribio rahisi tuu. Wangechagua wagonjwa kadhaa
ambao wamethibitika kuwa wanaumwa, kisha wawapeleke kwa babu wapate
vikombe halafu warudi na kuanza kuwaangalia afya zao kama kweli
wamepona au wanaendelea kupona au la, matokeo wangetueleza wananchi
ukweli, mwezi mmoja unatosha sana kumuangalia mtu kama kapona au vipi.
Lakini hadi sasa wizara imesema kuwa dawa haina madhara, ofcourse hata
ukichemsha majani ya mchicha hayana madhara, lakini huwezi kupona
(ingawaje kwenye mchicha unaweza kupata madini na vitamins kidogo).
Matokeo yake sasa ni kwamba watu wanakufa na wataendelea kufa na
wanaweza kufa wengi zaidi baada ya imani yao kuwa wamepona na kupuuzia
matibabu na taratibu na masharti mengine kulingana na magonjwa yao.
sijui tunakwenda wapi. Mimi binafsi nasikitika sana kuona bado
tunazidi kuwa kama mababu zetu waliombiwa ukioga haya maji risasi
haiingii mwilini...Tunakoenda si kuzuri.
Asante
--
Mtemi H. Miya
Dar es Salaam
Tanzania
Pole ndg yangu kwa kuumizwa roho na hivi vikombe. Hivi ni vijmambo tu. Tatizo ni nini hasa? Kwa vile vimejitangaza sana hasa cha loliondo au tatizo ni hizo dawa zinazonywewa? Kama umaaraufu wa hao watu hasa babu wa loli ndio umekukera, huo ni wivu. Epuka sana wivu!!. Hawa watu wamejitangaza wenyewe baada ya kuponywa magonjwa yao. Pia kama tatito ni dawa usiseme chochote kwa vile mitishamba ilikuwa inanywewa kila kukicha tangu zamani. Umeshaambiwa dawa ya loli ilikuwa inanywewa na wamasai, wasonjo na wagogo tangu zamani, mbona hukuiomba serikali itoe tamko? Vilevile kumbuka kwamba watu wanapokuwa wagonjwa kwa kipindi kirefu bila kupona kwa hizo dawa zilizothibitishwa, huamua kujaribu kila kinachowezekana ili mradi tu. Katika kujaribu huko wapo wanaopona na wapo wasiopona-hilo ni jambo la kawaida. Waache wanaoenda waende wasioenda waendelee kunywa dawa toka india na marekani.
ReplyDeleteNajua wivu wenu uko kwa babu.
Sie wabongo tumeendekeza haya mambo, utasikia popo bawa, mara ukiua albino utakua tajiri, ukitaka kupandacheo au kupata mafanikio ya kazi au biashara utaambiwa uende bagamoyo au sumbawanga, ukizunguka mtaani utakuta mabango kibao ya waganga wa jadi, ukiota ndoto mbaya basi lazima uende kwa mtaalam, mtoto akizaliwa basi anavishwa "makufuli" mpaka shingo inapinda!
ReplyDeleteBongo kwetu kila kitu ni imani, hakuna swala la kuupima mwili, tunasahau mwili unatakiwa kuangaliwa kisayansi. Kila kukicha utaona picha na kusikia habari eti mwanga kaanguka kwenye ungo! Au fulani kaenda kuoga kwenye mbuyu, au fulani hawezi kuamia nyumba yake mpaka mtaalam aje kuzindika, au fulani kaua mtoto au watoto ndo kafanikiwa na biashara, au timu zetu hasa simba na yanga haziwezi kushinda bila kulala makaburini. Basi inakua vumbi, katika yote haya wanaofaidika ni matapeli wanaojifanya waganga.
Lini tutafumbua macho?!
Hongera Mtemi kwa kutoa maoni yako. Nadhani umesikia kuwa serikali itajenga barabara kwenda Loliondo. Hilo linaweza kukupa fununu kuhusu msimamo wa serikali. Kuhusu wizara kupima wagonjwa, waganga wa kienyeji wako wengi saaaana Tanzania. Sasa sijui kila mganga mpya akijitokeza serikali iwe ina fanya hivyo? Lakini pia babu amewashika watanzania pabaya, maana anatumia mgongo wa Imani. Hapo kuna maslahi yatakayolindwa hata kama maisha ya watu yataendelea kupotea.
ReplyDeleteshukrani mdau uliyeleta mada hii, ila ningependa kutofutiana na wewe juu ya kitu kimoja:
ReplyDeletekatika masuala ya haki za binadam serikali au wataalam hawaruhusiwi kufanya majaribio yao moja kwa moja katika miili ya binadam kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na umeuwa kama itatokea mjaribiwa amefariki hivyo kuna hatua mbali mbali za kupitia katika majaribio na hatua ya mwisho kabisa ndio binadam wanaweza kujaribiwa tena kwa hiyari yao.
dawa ya babu bado haijapitia majaribio hayo yote zaidi kuambiwa na serikali kua dawa hina madhara kwa watumiaji, hata components za dawa yenyewe hatujaambiwa, uwezo wa dawa katika kutibu au kutuliza nk pia bado. Hivyo serikali haiwezi kuchukua lawama kwa kuwapeleka watu kwa babu kwa majaribio ya dawa hiyo.
Kwa upande mwingine nakubaliana na ushauri huo ila kama ifuatavyo:
Tangu babu wa loliondo amevuma kwa kasi ni zaidi ya mwezi sasa na watu walioshakunywa dawa hiyo kwa hiyari ni wengi sana hivyo basi serikali kwa kuwatumia wataalam wake pamoja na wale wakujitegemea wangeweza kufanya uchunguzi na kubaini maendeleo ya wagonjwa hao pamoja na kuwa-encourage watu hao ili wajitokeze kwa wingi na kufanyiwa vipimo na kubaini maendeleo ya afya zao kama wamepona, maumivu yamepungua, au hawakupona kabisa, au madhara mengine yanayoweza kuonekana katika miili yao. wakati huo serikali ikiendelea na utafiti juu ya dawa hiyo ambao kwa hakika utachukua mda mrefu hata zaidi ya mwaka au miaka. Hivyo kwa sababu hii nakubaliana nawe kua ni rahisi kwa serikali kufuatilia na kuchunguza kwa karibu hao waliosha kunywa hiyo dawa pamoja na kuwafanyia uchunguzi wa kina wale wanaojitokeza na kudai wamepona na kisha kufanya tathimini wakati wakiendelea na utafiti wa maabara kwa dawa ya babu.
Kumbuka pia serikali yetu haitakua ya kwanza kufanya majaribio katika mti huo wa Mugariga kwani majaribio katika mti huo yameshafanyika kwa mda mrefu hapa India, Ethiopia, Kenya nk na machapisho yao yapo online pia.
asante.
J. E
Wewe unarudia hoja ile ile kwamba ufanyile utafiti wa hizi dawa. Sasa hivi kuna dawa kama za aina tatu: ya Babu ambayo inaendana na imani za kimiujiza za kidini (kwamba utapona kwa imani yako), ya pili ni kijana wa Mbeya ambaye kasema ameachiwa mikoba na mama yake (mganga) na ya tatu ni huyo wa mbeya ambaye ni kama "doctor" (kwa maana kwamba hatumii imani za dini). Nakubali kamba utafiti ufanyike kwa dawa za kiganga (aina ya pili) na dawa ya "doctor" (aina ya tatu) lakini kwa dawa inayotokana na imani ya dini, hiyo haitawezekana kwa sababu dini ni imani huwezi kuitafiti. Na dio maana Babu wa Arusha anapata watu wengi zaidi, hata viongozi wa serikali sababu wengi wao wanamwamini Mungu ambaye hawajawahi kumfanyia utafiti au kumuona.
ReplyDeleteMimi naungana na mdau, kwa kweli napata mashaka na hili maana hatujathibitishiwa km kweli kuna watu wamepona zaidi ya kusikia tu mtaanai na mbaya zaidi tunaendelea kusikia kuwa watu wanaendelea kupoteza maisha kabla au baada ya kupata kikombe, inasikitisha na ni aibu kwa Taifa letu jamani , kinachonisikitisha zaidi ni kuona wanaibuka kila kukicha hao watoa vikombe hivi hatupaswi kujiuliza kweli kwamba pana ukweli au ni usanii tu unaendelea? Uchunguzi wa kina unahitajika ndugu zangu.
ReplyDeleteMimi naona kuwa serikali ichukue hatua na kuwashitaki wale wote wanaodanganya wengine kwa njia kama hizo. Tatizo ni kuwa hata serikali imekula chenga kwa hawa waganga wadanganyifu. Bongo oyeeee!
ReplyDeleteMalisa(BG)
lakini mdau au wadau mnasahau kwamba kujakumwona specialist muhimbili unaweza ukakaa miezi mpaka sita au mwaka kamahujahonga? muwe makini halafu dawa ya miti sio ushirikina
ReplyDeleteTatizo hapo ni nini sasa? kama ni kwenda kwa babu hakuna yeyote anaelazimishwa kwenda kunywa hiyo dawa, na kama ni kudhurika basi hakutakuwa na wa kulaumiwa kwa sababu watu wote walioenda Loliondo kunywa hiyo dawa walienda kwa hiari kama yeyote anaekwenda kutibiwa popote aidha kwa ramli au hospitalini... Na babu anapokupa hiyo tiba hakukatazi kuendelea na dozi zako za dawa za kizungu. Na utakapomkataza yeyote asiende kunywa dawa kwa babu itakuwa hujamtendea haki sababu hata hospitali zenyewe hapa nchini hazina dawa wala vifaa vya kutosha kukidhi mahitaji ya watanzania wengi ambao ni maskini. Hata kwa mie nisiejua hesabu naona wazi kwamba ni idadi kubwa sana ya watanzania wanaotibiwa kwa mitishamba, hasa idadi kubwa ya walio vijijini na sababu kubwa ni kwamba hizo dawa za kizungu hazishikiki kwa gharama kubwa. Je wakisema kumdhibiti babu na wengine kadhaa walioko huko vijijini kama alipo yeye je? nao wadhibitiwe? halafu???
ReplyDeleteMdau anaeponda kwa kusema watanzania wana imani za kichawi anagusa watu pabaya... Kwa yeye mwenye uwezo hata akiugua pesa yake itamsaidia kupata matibabu, sasa wasio na uwezo je? kuna hospitali ngapi Tanzania ambazo tunaweza kujigamba zinatosheleza mahitaji ya population yote na zitoe huduma bure au rahisi kukidhi mahitaji ya watu wote?
Siku zote watu waliokata tamaa hutegemea miujiza. Ajabu ni kwamba wale waliokuwa wanawa kashifu viongozi wa makanisa ya Pentekoste kama kina Kakobe na Mama Lwakatare ndiyo wako mstari wa mbele kenda kwa Babu ambaye pia ni Mpetekoste. Kina Kakobe wanaendesha maombi - lazima uende kanisani kwao kwani wanadai wao ndiyo wenye uweza wa kufanya maajabu kwa jina la Mungu. Babu yeye kaoteshwa dawa- anachofanya ni kupika (akisaidiwa na vijana wake)na kugawa dawa. Sijui ni kwa nini lazima agawe yeye dawa, maana ugwaji wake wake hauendi na maombi.
ReplyDeleteWAtu 78 wamekufa wakisubiri kupata kikombe huku wakubwa kama mawaziri na wabunge waki-antilog. Kwani akikoroga dawa ikapelekwa kwenye vituo vya ugawaji haitafanya kazi? Kwa kuwa yeye ni Nabii haitoshi kuweka baraka zake katika hiyo dawa ili mwingine aigawe?
Wale wote wanaoumia kwa sababu watu wanaenda Loliondo wana agenda yao nyingine. Hakuna mtu anaweza kukasirishwa na mtu ambaye anasaidia watu kwa uwazi na ukweli.
ReplyDeleteKwa babu hakuna masharti yoyote ya kishirikina. Nimesikiliza ushuhuda wa Mchungaji wa jinsi Mungu alivyomwelekeza kutoa hii tiba. Ushuhuda umekaa vizuri.
Jamani Viongozi wa Dini mnaomsema huyu babu ni Mganga Kumbukeni kwamba hata Bwana Yesu aliambia ana mapepo na hilo ndilo kosa alilohukumiwa nalo Yesu na akasulubisha na Wayahudi kwani walidai anawachafulia dini yao.
Viongozi wa Dhehebu fulani la Kikristo wamekuwa mstari wa mbele kumshambulia Mchungaji huyu kwa sababu walifikiri kuwa wao peke yao ndiyo wanaweza kutumiwa na Mungu sasa wameona Mungu amemtumia " Msamaria Mwema" badala yao wanaojiona kama ndiyo mafarisayo wayahudi.
Ukisoma Ufunuo 22:7 na kuendelea utaona kuwa MUNGU ATAWEKA MTI WA UZIMA KWENYE HUKO KWENYE YERUSALEM MPYA NA MTI HUU WENYE KUZAA MATUNDA 12 KWA MWAKA UTAKUWA NA MAJANI YATAKAYOKUWA YANAPONYA WAGONJWA.
Sasa kama Mungu ameweka mti kwenye Ulimwengu mpya ujao baada ya kiama kuwepo, ilihali yeye mwenyewe Yesu atakuwepo sembuse Leo. Mbona ni mara nyingi ti Mungu ametumia miti kwenye biblia kwa kuwaongoza watumishi wake.
HOJA YANGU NI KUWA BABU WA LOLIONDO NI MTUMISHI WA MUNGU. WENGINE NI WAGANGA NATUNAWAACHIA MAMBO YAO WENYEWE.
TUACHE WIVU WATANZANIA
Ni kweli kabisa Mtemi alichokisema... kwan kumekuwa na hili sasa kama mwezi mmoja umepita, na serikali imefumba macho tu na mbaya zaid kupeleka usalama wa taifa, nikam vile serikali inasisitiza swala hili, inaamina babu anaweza tibia ahta Ukimwi, jaman watanzania tufumbue mamcho fikilien na wanaondelea na matibabu ya magonjwa yao waendelee kwan kwa uharisia ni vigumu kikombe kutibu ukimwi..Serikali tunaomba itoe watu wanaumwa hayo magonjwa sugu kutoka hospital kama muhimbili wawasafirishe kwa gharama ya serikali, then wakanywe kikombe cha babu then we should wait in a month kama Mtemi alivyoshauri then tupate conlusion ya kwamba kikombe cha babu cha tibu magonjwa sugu kwa sasa ni kama hatuna mtu aliyetoa testimony au ushuhuda kusema yeye alikuwa anaumwa nini na vyti vya kudhibitisha ugonjwa wake na sasa kapima hana magonjwa hayo na vyeti pia kutoka kwa Dactari aliyempima.....Tunaomba serikali ichunguze kwa makin na ifanye research kuhusu dawa ya babu na kama kweli ya tibu magonjwa hayo then dunia nzima wajue jaman.....
ReplyDeleteNimesoma andiko hilo hapo juu na nikakuta lipo kwenye ufunuo sura 22.2.
ReplyDeleteTena nimeona mahali ambapo Musa aliambiwa na Mungu akate tawi la mti na kutumbukiza kwenye kisima cha maji machungu (chumvi) walipokuwa jangwani wana wa israeli. Na akafanya hivyo na maji yakawa mazuri na watu wakanywa.
Halafu nikaona sehemu nyingine ambako mfalme hezekia alikuwa anaumwa na nabii akatumwa na Mungu akamwambie Mfalme Hezekia atengeneze mkate wa tini na kisha auweke juu ua majipu yake. Na alipofanya hivyo akapona.
Yesu alimponya mtu mmoja aliyekuwa mgonjwa miaka mingi. Lakini Mafarisayo wakakasirika sana kwa kuwa alimponya siku ya sabato. Wakaanza kumshinikiza yule mtu aseme kama yesu ametoka kwa Mungu au la. Yule bwana akawapa jibu moja tu.
"KAMA ANA DHAMBI AU LA MIMI SIJUI..LAKINI MIMI NILIKUWA MGONJWA NA SASA NIMEPONA"
Kwa hiyo wanaosema Babu Mganga watajiju tunachojua ni kwamba tulikuwa ni wagonjwa na sasa tumepona. Hayo mengine tunawaachie nyie watakatifu kuliko sisi.
Babu alisema kunywa kikombe kwa imani yako na utapona. Nadhani inatosha, tumeteseka sana na matibabu, watanzania tunaimani sana na mungu, ameteuwa taifa letu kutupatia dawa. Ni mara ngapi tumemuomba mung,na mumgu atusaidie tupone, tuweze kutunza familia zetu, kwa imani yako dawa imekuja na kwa imani yako utapona. Serikali yetu tunaishukuru kwa kile walichokifanya hata kumlinda babu aendelaa kutupa dawa. Tunashukuru hata kupata hcho kikombe. Tatizo kubwa ambalo tuliopo kwenye mtandao tumesahau kwamba hiki chombo ni watu wachahce ambao wanakitumia, asilimi kubwa ya waliokwenda loliondo hawajui komputa ni kitu gani sasa kama unataraji kupata jibu hapa kuhsu nani kapona nani kafa huwezi kupata jibu lakini unakaribishwa kwenda kwa babu kwa imani yako.
ReplyDeleteMchungaji Ambilikile anatibu kwa kutumia dawa ambayo alioteshwa na Mungu, hivyo dawa hiyo inatibu kwa imani. Imani si kitu cha kupima, cha msingi kimeshafanyika kwamba serikali imepima dawa hiyo na kuona haina madhara kwa binadamu.... period!! Wewe unaeibeza utakuwa huumwi but kwa mtu ambae anaumwa na keshahangaika sana na matibabu huwezi kumwambia loloteee ataenda tu kupata kikombe. Mtu anaeumwa anahangaika huku na kule kutafuta tiba kwaiyo waache watu waende nao wakajaribu bahati zao kwa kutumia imani zao. HIVYO, NA WEWE MTEMI MHIYA NAKUSHAURI UENDE LOLIONDO, KIJIJI CHA SAMUNGE KWA MCHUNGAJI AMBILIKILE MWASAPILA UKAPATE KIKOMBE!!
ReplyDeleteSasa sijui mnalalamika nini!! Serikali imeshahalalisha, na sasa inajenga barabara ya kwenda kwa babu. KKKT nayo itajenga jengo la wagonjwa kupumzikia. Kwa ufupi babu ameshakubalika. Sasa hao wengine ni wasanii au wametumwa na watu wengine ili wamuaribie babu. Pamoja na maelezo yangu yote, namalizia kwa kusema kuwa sina uhakika juu ya hiyo dawa kama inatibu au la. Maana kuna mama wa rafiki yangu alipelekwa kwa babu akapata kikombe ili atibu kisukari pamoja na kansa. Siku saba zimepita tangu apige kikombe lakini hakuna mabadiliko. Imebidi apelekwe Muhimbili na mpaka sasa amelazwa. Lakini kuhusu dawa ya babu nafikiri wengi wanakosea masharti. Tiba inaenda na imani ya dini, lakini watu wanatoa rushwa ili waruhusiwe na polisi kwenda, kinyume na utaratibu, hapo unategemea nini?
ReplyDeleteImani imani imani! what you believe is what you get.Watanzania wenzangu,hebu kaeni mfikiri msipoteze muda bure kwa kudai dawa hii inaponya kama dawa ya ukweli kwa nini wengine wapone wengine wasipone indapo wanaumwa ugonjwa mmoja? Huyu babu anatibu imani, mwenye imani akienda kutokana na imani ile aliyonayo anapata nafuu na wala haponi!mtu yoyote anaedai amepona mpeni miezi sita kwanza, huyu babu hata miezi mitatu haijaisha wabongo wanadai wamepona jamani! mwaka 2005-6 nilikuwa nipo huko bongo, kuna babu mwingine (kijana) ambaye ni marehemu sasa, alikuwa Tegeta! it was the same story like this of loliondo!na watu walimuamini sana na walikili kuwa anaponya, baada ya huyo babu kuaga dunia, walioamini wamepona magonjwa yalibaki pale pale na wengi walimfuata! kwa magonjwa hayo hayo waliodai waliponywa!, ITS SAD!.
ReplyDeleteLABDA NITOE USHAURI KIDOGO TU,WATANZANIA TUPUNGUZE STAREHE!NA AMINI KABISA , WAGONJWA WENGI WA BABU NI WALE WALIOATHIRIKA NA UPUNGUFU WA KINGA MWILINI!.Na source hasa unaelewa mdau!.Hii ndio hasa inaowajaza watu huko kwa babu, japokuwa wapo wa magonjwa mengine but this one is the head of them.Taifa letu linateketea wadau!Tutatue tatizo la ongezeko la huu ugonjwa kwanza, na wale waliothirika tayari zingatia rishe bora, na wagonjwa wa cancer which is more worse, kwani pain killer zake so expensive kwa famillia zetu, ila kwa wale ambao hawajaathirika, nawashauri mjiwekee utaratitu wa kufanya check up mara kwa kara, kwani cancer ukiiwahi uwezekano wa kupona nimkubwa sana!.
Hapa si swala la kumwonea wivu babu, tunaelimishana na kufumbuana macho!so is up to you mdau take or leave it!. You don't need to be aggitated or angry! ushauri mzuri ufuate na mbaya kwa hisia zako achana nao!WAINGEREZA WANASEMA, WHATCH THE GAP BETWEEN PLATFORM AND TRAIN, usipokuwa makini tu utateleza na kupoteza maisha kwani kuna gap pale. ila mie nakumbioa mtanzania mwenzangu watch the gap btn you and kikombe!, usipokuwa makini utapoteza pesa zako nyingi instead ungekaa home nkupata chakula bora kudumisha maisha yako au ungenunua dawa za cancer au ungeenda kucheck afya yako.THINK BEFORE YOU MAKE A STEP TO ANY KIKOMBE.
Cha kushangaza ni zile story za watu, hakuna aliejitokeza na vyeti, kuwa alikua anaumwa ukimwi na magonjwa mengine makubwa na kutuonyesha kwa vyeti vya vipimo kuwa kapona au wamepona.
ReplyDeleteTunaomba waje wajitokeze, watuambie, kuwa walikua wanaumwa na vyeti vya kuumwa hivi, na baada ya kikombe wakaenda tena kupimwa na vyeti wakapewa tena na tuvione!
Zaidi ya hapo itakua kudanganyana tu kama kawaida yetu.
Mara popo bawa, mara babu Loliondo, mama Tabora, Mama Morogoro, sijui ukiua albino unakua tajiri, au kuiona bibi kizee mwanza au shinyanga basi mchawi, au “wataalam” wamejaa Bagamoyo! Au Sumbawanga kumejaa wachawi na waganga (wakati ni maskini wa kutupwa, huku rasilimali za kila aina zimezagaa tu!).
Tuachane hayo mambo ya imani za ajabu.
Tukumbuke dini ilianzishwa na binadamu na ndo maana kila kukicha wazungu wanabadilisha masharti ili yaendane na maisha yao! Kama waarabu ndo usiseme, yalioandikwa kwenye koran yanakua machungu kwao, wanataka “democracy” isio na “mujahedinas!”
Leo sisi ndo tunajifanya hizo dini tulianzisha sisi na tunazijua kinoma!
Fumbueni macho wabongo!
Comments
ReplyDelete0 #4 kajap 2011-04-07 12:58
'God' does not have anything to do with the medicine. Using plants and trees as medicine in scientific, and the application of this tree as medicine is found long time ago, The God factor is only helping psycologically. If somebody wants to know more abt this medicine pls refer Ayurveda (Its a science- not a myth!)
Quote
#3 MbongoHalisi 2011-04-07 12:03
I wonder whether God has to got to do with anything with BABU discovering this so called medicine?, should we then state that other scientists such as Newtons gravitational force, Enstein E=mc2 and others like Archimedes Aristotle, Niels Bohr, Nicolaus Copernicus, Marie Curie, Charles Darwin, Leonardo Da Vinci, Rene Descartes, Thomas Alva Edison, Benjamin Franklin,
Galileo Galilei, Max Planck, Wilhelm Conrad Rontgen, Carl SaganNikola Tesla. WOTE WALIOTESHWA NA KUPEWA FORMULA ZAO??????
Sio siri bado tuko maskini wa kutupwa duniani!
Quote
0 #2 Rumishael Shoo 2011-04-07 11:44
: :This is yet another example of how much we have lost direction!!!!
Quote
0 #1 kajap 2011-04-07 09:17
The reserchers, please go to India and refer the encient Ayurveda.. abt 2000 yrs ago this was used for chronic deceases, and is good for "T
Source : http://www.thecitizen.co.tz/news/4-national-news/9719-herb-analysis-could-take-a-long-time