Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania hayati Marehemu Mzee Abeid Karume katika bustani za Afisi ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo asubuhi wakati wa maaadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha musaisi huyo
Rais wa Tanzania,Dr. Jakaya Kikwete (kulia) pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wapili Kulia) wakijumuika kwa pamoja na viongozi wengine katika kumuombea dua marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika kaburi afisi kuu ya CCM Kisiwandui leo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiweka shada la maua katika kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume leo.
Rais Jakaya Kikwete akiondoka Afisi Kuu ya CCM Zanzibar baada ya kumalizika kwa shughuli ya kisomo cha hitma ya marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume leo Mjini Zanzibar.
Rais wa Tanzania,Dr. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho na Balozi Ali Karume wakiomba dua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu mzee Abeid Amani Karume jana Mjini Unguja.
Mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume akiomba dua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume akiwa pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein,(katikati) kulia ni mke wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Mama Asha Seif Idd na wa mwisho kushoto ni mke wa Balozi Ali Karume, Huda Karume
Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (tatu kulia),Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja na viongozi wengine wakisoma hitma ya kumuombea dua Muasisi wa Mapinduzi,na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume,Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...