Mdau Lukwangule, Beda Msimbe, anapenda kuiarifu jamii nzima ya wanalibeneke kwamba Misa ya kumuombea marehemu baba yake mzazi hayati John Luwanda, Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania, itafanyika katika kituo cha maombi cha Marian Faith Healing Centre, Riverside Ubungo Jumamosi Aprili 30, saa 12 asubuhi.
Misa hiyo itafuatiwa na upandaji wa Msalaba katika kaburi la Marehemu Goba Kibululu na kisha sadaka kidogo kwa watakaofika kuadhimisha upandaji wa Msalaba.
Nyote mnaoweza kufika mnaalikwa na wale wasioweza tuwe sote katika roho kwa sala.
Mungu ametoa, Mungu ametwaa Amina. Roho ya Marehemu John Luwanda na Marehemu wote zipumzike kwa amani Amina.

Poleni sana ndugu wafiwa mungu ailaze pahali pema roho ya mzee wetu John Luanda,napenda kuuliza huyu mzee J.Luanda ndiye yule aliyekuwa mmiliki wa bendi ya Chamwino kule Tnadale miaka ya 80 ??naoma kufahamishwa hili.
ReplyDeletemdau Tokyo,Japan.
poleni wanafamilia na marafiki wa marehemu mzee John Luanda,kama sikosei huyu ndiye aliyekuwa mmiliki wa bendi ya Chamwino miaka ya nyuma, iliyokuwa na makao yake sehemu za Manzese/Tandale Dar,mungu amuweke mahali pema peponi.
ReplyDeleteRIP Mzee John Luanda,RTD(enzi hizo)na Chamwino Jazz Tandale Dar.
ReplyDelete