Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu kanuni za uendeshaji wa shughuli za bunge leo mjini Dodoma
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia)akijadili jambo na Waziri Ofisi ya Rais ,Utawala Bora Mathias Chikawe ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Sheria na Katiba Celina Kombani akitoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu namna ya kuingia katika zoezi la upatikanaji wa katiba mpya na namna wananchi watakavyoshiriki kutoa maoni yao katika mchakato wa upatikanaji wa katiba hiyo bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijibu maswali kutoka kwa wabung juu ya ufanyaji wa tathmini na ulipaji wa fidia kwa wananchi kutoka kwa makampuni yanayofanya utafiti wa madini ya dhahabu nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma.

Wabunge wakiwa katika kipindi cha maswali na majibu ndani ya mkutano wa wa tatu wa kikao cha kwanza cha bunge leo mjini Dodoma. Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunawatarajia sana waheshimiwa wetu safari hii mpate ufumbuzi wa haya matatizo yaliyowekwa hadharani kwenye kipindi cha kampeni hasa ya ufisadi, rasilimali nyingi lakini watu masikini, Mikataba mibovu na matumizi mabaya ya madaraka ambapo mtawala anafanya kazi kujinufaisha mwenyewe na sio taifa. chonde chonde nawapigieni magoti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...