Meya wa manispaa ya Moshi,Mstahiki Jafary Michael akizungumza na wananchi katika kata ya Kiusa ambako alizundua mpango wa hifadhi mazingira .
Sajini Meja wa kambi ya polisi iliyopo kata ya Kiusa Afande George akipanda mti katika eneo la line polisi mara baaada ya uzinduzi wa mpango wa kuhifadhi mazingira katika kata ya Kiusa.
Mstahiki Meya wa Moshi Jafary Michael akiotesha mti wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuhifadhi
mazingira uliozinduliwa katika kata ya Kiusa.
Mstahiki Meya Jafary Michael akipanda mti
Diwani wa kata ya Kiusa Bw. Steven Ngasa akimnawisha mikono Meya Jafary Michael mara baada ya kuzindua mpango wa hifadhi mazingira katika kata ya kiusa.
Picha na habari na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii, Moshi.
MEYA wa manispaa ya Moshi,Mstahiki ,Jafary Michael(Chadema) amezindua mpango rasmi wa hifadhi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya wazi,vyanzo vya maji na makazi ya wananchi ambapo kwa kipindi cha mwaka huu wanatarajia kuotesha na kuitunza zaidi ya miti 2000 katika kata ya Kiusa.
Akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni hiyo,Meya Michael alipongeza kata ya Kata ya kiusa kwa kutambua suala la mazingira ambalo ni sehemu ya mipango ya manispaa katika kutunza mazingira jambo ambalo limeiujengea heshma mji huo.
Alitoa rai kwa kata nyingine kuiga mfano huo ili kuleta mapinduzi ya mji wa Moshi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na kwamba manispaa itawaunga mkono wananchi katika utekelezaji wa suala hilo.
Aidha Meya Michael alisema manispaa pia inafanya mipango ya kutunga sheria ndogo ndogo ambazo zitavithamini,kuvitambua na kuvilinda vikundi vya kijamii ambavyo vimeundwa kwa lengo la kutunza mazingira.
Awali diwani wa kata hiyo,Stephen Ngasa alisema mpango wa utunzaji mazingira utahusisha zaidi ya nyumba 16,000 katika kata hiyo ambapo kila nyumba inatakiwa kuotesha miti mawili mbele ya nyumba.
Alisema katika uzinduzi huo zaidi ya miti 700 iliyotolewa na kikundi cha mazingira kata ya Kiusa(KIMAKAKI)itaoteshwa katika eneo lililopo mkabala na kambi ya jeshi la Polisi mjini humo huku pia familia za
askari zitashirikisha ili kuotesha katika makazi yao.
Mapema mwenyekiti wa Kikundi cha Kimakaki,Redemta Shirima alisema kikundi hicho kilichoanzishwa mwaka 2006 tayari kimeotesha na kuitunza zaidi ya miti 3000 katika shule za Msingi Kilimanjaro,Muungano,Kiusa na Jamuhuri kando ya barabara tofauti.
Bi Shirima pia aliomba manispaa hiyo kuwasaidia misaada mbalimbali ikiwamo utaalamu wa kudhibiti magonjwa ya mimea,vyanzo vya kudumu ya mapato ili waweze kupata uwezo wa kueneza elimu ya utunzaji wa mazingira katika taasisi nyingi zaidi..


Hongera sana Mstahiki Meya wetu Bw Jafary. Nikuhamasihe wewe na madiwani wote Manispaa na nje ya manispaa-mtoke na kuhamasisha wakaazi wote walao kupanda miti mitatu kila familia katika kipindi hiki cha mvua. Moshi yetu imekuwa kame na hali mbaya ya ujoto kwa kuwa tumeharibu sana mazingira ikiwa ni pamoja na kukata miti mingi bila ya kupanda mingine. Hongera baba hongera na usiishie hapo. Moshi tuamke tupande miti mingi - wakati ni huu.
ReplyDeleteMdau mpenda mazingira.