Waziri wa Katiba na Sheria, Mh. Celina Kombani akifungua mchakato wa kupokea maoni ya kujadili mwenendo wa uundwaji wa Katiba Mpya ndani ya Ukumbi wa Pius msekwa mjini Dodoma leo
Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (katikati) akishauriana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. James Nsekela (kulia) na Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema (kushoto) wakati wa kudhibiti vurugu zilizojitokeza leo katika maeneo ya viwanja vya Bunge Dodoma kufuatia utoaji maoni ya mchakato wa kuunda tume ya kushughulikia katiba mpya kuona ni lipi la kufanya baada ya Ukumbi wa Msekwa kuonekana ni mdogo. Hivyo ikakubalika kuwa Ukumbi wa Chimwaga utumike. Hata hivyo wanafunafunzi walikataa pendekezo hilo.
Katibu wa Bunge akifafanua kwa waandishi wa habari sababu zilizopelekea nguvu kutumika ili kurejesha amani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Bw. Jossey S. Mwakasyuka.
Hali ya kuvurugika kwa amani katika lango la Bunge ilianza kuashiria hatua iliyopelekea polisi kurusha risasi za mpira
Wadau wakisubiri kujua utaratibu wa kuingia katika ukumbi wa Msekwa ili kutoa maoni yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...