Wheelchair mdau aliyojitolea kumnunulia kijana mlemavu Yohana Benjamin aliyeomba msaada tutani katika Globu ya Jamii majuzi (BOFYA HAPA). Mdau mwema huyu kaomba jina na bei ya wheelchair tuweke kapuni.Ndugu Michuzi kwanza nikushukru kwa kazi nzuri unayoifanya kwa faida ya jamii. Hongera sana. Pichani nimemkubidhi bwana Robert Revocatus – 0763 299960 Wheel Chair kwa ajili ya kijana Yohana Benjamin kama ulivyo onyesha umma kwenye Blog ya Jamii na TBC1 kwenye taarifa ya habari yao ya hapo jana.
Nimehakikishiwa kuwa kesho Robert atapelekwa Pugu Secondary ili akaendelee na masomo yake. Misaada zaidi itatakiwa ukizingatia hali yake na hali harisi ya shule zetu za umma. Kwa nyongeza tu nimekuja kujua kuwa Robert na Yohana ni watu wa Manyovu Kasulu waliohamia Kasangezi. Zaidi mnaweza kuwasiliana naye.
Asante sana kwa kazi nzuri.
Asante sana kwa kazi nzuri.
TEGETA OYEEE!.


Hongera sana mkuu kwa msaada Mungu akuzidishie mara 100 pale palipopungua nimefarijika sana kuona hii ila Michuzi tusaidie kuweka Account number ili tusaidie mana mkuu bado ana mahitaji mengine.
ReplyDeleteUliyetoa msaada Mwenyezi Mungu atakupa baraka njema hapa duniani na kesho akhera. (Jamani nawapa siri: Insurance ya mali zenu ni kutoa sadaka. Ukitoa sadaka basi Mwenyezi Mungu hukulinda wewe mali zako.)kama hutoi sadaka basi Mwenyezi Mungu huondoa kinga yake na hapo utaona mara umeibiwa, mara umekamatwa utoe rushwa kubwa, mara ajali, mara moto na mambo mengi ili mradi utakuta mali zako zinaangamia hivi hivi. DAWA yake ni kutoa Sadaka kwa wanaohitaji msaada.
ReplyDeleteMdau uliyejitolea nimeguswa sana kwa msaada wako wa wheelchair kwa Bw. Yohana. Mungu akubabariki sana na azidi kuneemesha mifuko yako siku zote. Amen.
ReplyDeleteSafi sana. Na kweli Mungu amzidishie baraka huyo msamaria mwema. Lakini navyoona huyo kijana Yohana Benjamin anahitaji mtu wa kumsaidia. Nilipokuwa nasoma Zanaki kulikuwa na dada mwenye hali kama yake. Walichofanya ni kumchukua mdogo wake kutoka kumsaidia. Yule dada mlemavu alikuwa Form 5, lakini mdogo wake alikuwa Form 1. Walikuwa wanakaa wote pale Zanaki Hostel. Mdogo wake alikuwa anamsaidaia mfano kuoga, Chakula, kwenda chooni etc. Kwa hali hiyo na unavyojua ugumu wa kupata elimu ya serikali enzi hizo 1970's basi mdogo wake alifaidi. Alipomaliza Form 6 yule mdogo alibaki Zanaki na wlaimchukua mtu mwingine kumsaidia hadi Chuo Kikuu. Lakini naona kama serikali walikuwa na mpango wa kusaidia walemavu enzi hizo, nashangaa huyo kijana kahangaika hivyo mpaka kuja kwenye blog kuomba msaada.
ReplyDeleteMungu ambariki na amzidishie neema mdau aliyejitolea kumsaidia kijana huyu.
ReplyDeleteMungu akuzidishi kila la kheri mdau uliejitolea Baiskeli.
ReplyDeleteKingine kinachohitajika hapo ni kuondoa ngazi au kuweka njia ambayo hiyo wheelchair itapita kwenda msalani. Majengo na maeneo mengi kwetu hayazingatii mahitaji ya walemavu, sidhani kama kinahitajika kiasi kikubwa cha pesa kutengeneza njia ya kuingilia chooni na kumuwekea choo ambacho yeye anaweza kutumia bila kwenda vichakani. Pakirekebishwa hapo wizara ya elimu itakuwa imepata mahali ambapo wanaweza kuwapeleka walemavu wengine pia.
ReplyDeleteWahusika wa wizara ya elimu shughulikieni hilo la kutengeneza mazingira ya kuwawezesha walemavu kupata huduma muhimu kama vyoo.
wewe mdau uliye jitolea kuleta hii wheelchair asante sana kwa roho yako nzuri. wengi hatuwezi kukulipa wema wako lakini mwenyezi mungu atakulipa. nina kutakia kila la kheri kwenye maisha yako
ReplyDeletemungu akubariki kwa moyo wako mwema
ReplyDeleteMwenyezi Mungu akulipe mema hapa duniani na akhera kwa msaada wako na kwa moyo wa kuwakumbuka ndugu zetu hawa wenye shida. Kama ulivyomwesezha huyu kijana Yohana benjamin na Mwenyezi Mungu akufanyie uepesi siku ya mahesabu.
ReplyDeleteKADRI SIKU ZINAVYO KWENDA NDIO UMUHIMU WA BLOG YETU HII YA JAMII INAONYESHA NI JINSI GANI INATUEWEKA KARIRIBU WANA BLOG HII JAPO HATUJUWANI,HABARI HII ILINIUMIZA SANA ZA HUYU KIJANA ILA SIKUWA NA JINSI(UWEZO)WA KUTOA MSAADA.WABARIKIWE WOTE WALIOFANIKISHA JAMBOHILI NA MUNGU AWAZIDISHIE MEMA KATIKA KILA WANALOLIFANYA.KAKA ULIOTOA MSAADA UBARIKIWE.
ReplyDeleteWATU WA ULAYA AU UGHAIBUNI MMEONGEA LETENI MISAADA ULAYA KUNA WHEECHAIR NYINGI,ACHENI KUWAONA WATU wa bongo hawana uwezo bongo watu wametulia hawaongee wewe kama mdau wa ulaya sema basi maana unachangia maneno mengi kuliko uwezo mlikuwa nao.Tufanye kazi kwa vitendo changieni watu SIO KUULIZA BANK DETAIL WEWE CHANGIA MCHUZI YUPO MTUMIE SIO BANK DETAIL huu ni utapeli.tumia west UNION
ReplyDeleteAU KAA KIMYA WEWE UPO ULAYA UNAONYESHA USIVYOKUWA MJANJA NI MANENO YA DANGANYA TOTO.TUACHE WATU WA BONGO tuwasaidie watu wewe kusanya hele za kuja kuwaonyesha wabongo umetoka ulaya
Ndugu umefanya jambo jema kabisa mbele ya Mungu na mbele ya jamii nzima kwa kujitolea kumsaidia huyu kijana ulipo pata hii habari na ukuchukua mda mlefu kweli unamoyo wakusaidi na pia upendi makuu angekuwa mtu mwingine angetangaza na kiasi alicho nunulia hiyo wheelchair nakutangaza hapo mamilioni ya pesa, Asante
ReplyDeleteJE TUNAWEZA KUWA NA MPANGO ENDELEVU JAPO KWA HUYU KIJANA, KILA MTU NA AJITOLEE KWA NAMNA ATAKAVYOBARIKIWA NIKITAMBUA KUWA MSAADA KWAKE HAUISHII KWENYE WHEEL CHAIR? NAWASILISHA
ReplyDeleteAhsante sana mdau MUNGU WETU AKUBARIKI NA AKUONGEZEE MARA SABA SABINI. WADAU wengine ninawakumbusha pia kuwa tunaweza kutuma hata kwa M-PESA kumsaidi mwanafunzi Robert. Ahsantenik wa Utayari wenu. @ sista wa Loliondo
ReplyDeleteUbarikiwe sana ewe mdau uliyenunua hiyo baiskeli. No gud words can explain, but may gid bless u million times!!
ReplyDeleteKwa wwalemavu serikali sasa inabidi izingatie kwa siku za mbele kuweka sheria za kuwarahisishia njia mbali mbali kwenye jumuiya kuanzia kwenye mabasi katika nafasi za kukaa ngazi maalum za kuwawezesha kupanda, ngazi maalum kwenye majengo majengo ,nafasi za kupakii magari kwa kuwapa vibali maalum,pamoja na vyoo maalum
ReplyDelete