Simba SC leo imefunwga bao 3-2 na Tout Puissant Mazembe (zamani TP Englebert) katika mchezo wa mzunguko wa pili wa michuano hiyo Klabu Bingwa Afrika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Katika mchezo uliopigwa wiki mbili zilizopita mjini Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika Uwanja wa Kenya, Simba ililala kwa bao 3-1, hivyo ndio kusema imefungwa jumla ya mabao 6-3.
Simba leo imejitahidi katika kukipiga na TP Mazembe ambapo mabingwa hao wa Afrika wana historia kwa kuwa timu ya kwanza kufika hatua ya fainali Klabu Bingwa ya Dunia, baada ya kuitoa Elan De Mitsoudje ya Comoro kwa mabao 4-2.
Simba ambayo ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, huku wakiongoza ligi hiyo kwa pointi 44 sasa, walichesza kufa na kupona lakini vibopa hao wa Lubumbashi waliwazidi kete katika kila idara.
safi tu! midomo ilizidi...
ReplyDeleteHakuna cha kusema Simba yaikosakosa TP Mazembe, Semeni tu imefungwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
ReplyDeleteWamejitahidikwa kufungwa 3-2 Nyumbani,You are right Ankal!
ReplyDeleteShehe naona utani unapitiliza. Mechi imetuuma, acha mzaha.
ReplyDeleteMATOKEO YALIJILIKANA MBONA TANGU MWANZO NANI ANAFUNGWA . IYO KUIKOSA KOSA NDIO KAULI ZETU ZA KAWAIDA WATAINZANIA . TUMEZOEA KILA SIKU , SJUI KUIKOSAKOSA , KUFA KISHUJAA NI VITU VYA KAWAIDA KIUKWELI HATUNA KIWANGO.
ReplyDeleteSimba mandemba...
ReplyDeleteHivi jamani simba mnashindwa hata kuwa na kikosi cha tarumbeta kwa ajili ya kushangilia, mliona sie watoto wa mamba tulivyokuwa tumeuteka uwanja!???????????????
ReplyDeleteTena bahati yetu timu ilibebwa na Waganda na wakenya waliomo kwenye timu. Huwezi kuwa na wachezaji wazuri wakati umefungia michezo mashuleni.
ReplyDeleteLabda tukiandaa vizuri vijana baada ya miaka 8 ndiyo tunaweza kuwa na wachezaji wa-kitanzania wenye viwango.
Wamejitahidi kwa timu mabingwa kama wale kupigwa 6-3,wajipange upya
ReplyDelete