Mwimbaji nyota wa muziki wa nyimbo za injili,Anastazia Mukabwa ambae kwa sasa anatamba na wimbo wake wa kiatu kivue alioshirikiana na Rose Muhando,akiimba jukwaani jioni ya leo kwenye uwanja wa ccm-kirumba,ambapo ilikuwa ni muendelezo wa tamasha la pasaka lililoanzia jijin Dar,kisha Dodoma na kumalizikia jijini Mwanza,ambapo ilikuwa ni siku ya sherehe za muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Christina Shusho akiimba jukwaani jioni ya leo mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi kutoka sehemu mbalimbali,ambapo leo ilikuwa ni siku ya Muungano,lakini limefanyika tamasha la muziki wa injili,lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions kwa ajili ya wakazi wa jiji la Mwanza ambapo wakazi wake bado walikuwa mapumzikoni.
Mmoja wa wakali wa nyimbo za injili nchini,Rose Muhando akiimba wimbo moja ya wimbo wake uliowahi kutamba siku kadhaa za nyuma uitwao nibebe,wimbo huo uliwavutia wengi uwanjani hapo na kujikuta wakicheza na kuimba kwa pamoja,hali iliyomfanya Rose Muhando apandishe mzuka wa kuimba na kucheza zaidi.
Anaitwa Bonny Mwaitege ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake kadhaa ikiwemo ule wa Mama ni Mama pamoja na Njoo ufanyiwe maombi,nyimbo ambazo pia jioni ya leo ameziimba mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza.
Nyota mwingine wa nyimbo za injili kutoka nchini DRC-Congo,Solomoni Mukubwa akiwaimbia wakazi wa jiji la Mwanza jioni ya leo kwenye tamasha la nyimbo za muziki wa injili lililowakutanisha wakazi mbalimbali jioni ya leo,ambapo ilikuwa ilikuwa ni siku ya Muungano.
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama (waandaaji wa tamasha) akimsikiliza kwa makini mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM (kituo cha Mwanza),Albert Sengo kuhusiana na albamu mpya ya Anastazia Mukabwa aliomshirikisha Rose Muhando,iitwayo Kivue kiatu,pichani kati ni mfanyakazi wa Clouds FM ndani ya jiji la Mwanza aitwaye Samadu akisikiliza pia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani mimi nimefuatilia sana haya matamasha ya muziki wa injili,naona kuna wasanii mbali mbali hata kutoka nchi jirani wametia fora sana.Kikubwa kinachonisumbua ni kuwa mbona hatumuoni gwiji wetu wa muziki wa injili Cosmas Thobias Chidumule ???au ndio amekwisha ki muziki???inaonekana kuwa aliweza kuonyesha mafanikio makubwa ya muziki alipokuwa katika muziki wa dansi,mimi naona kujiingiza kwake katika muziki huu wa injili ni kama amekwenda kujizika kabisa kimuziki,matamasha ya aina hii tulitegemea yeye ndiye atakayeongoza kutokana na ujuzi wake wa muziki wa siku nyingi !!!Nomba wadau mnisaidie kunijulisha kama nguli huyu bado yupo ??au kuokoka kwake kunamzuia kushiriki ktk matamasha ya aina hii au pengine ni dhambi kwake ???
    mpenda muziki Dar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...