Mwenyekiti wa Chawatiata mkoa wa

Iringa Bi, Christina Mgongolwa


Wakati idadi ya vikombe vya tiba kwa watu wenye magonjwa sugu zikizidi kuongezaka siku baada ya siku,chama cha waganga wa tiba asilia Tanzania (CHAWATIATA) mkoa wa Iringa kimempongeza babu wa Loliondo mchungaji mstaafu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ambilikile Mwasapila na wengine wanaojitokeza kuwa wameseidia kuifumbua macho serikali kuamini kazi ya tiba asilia.

Wakati mshauri mkuu wa waganga wa tiba asilia Tanzania Anton Mwandulami akiitaka serikali kupiga marufuku watoaji wa vikombe kuendelea kujitangaza huku akidai kuwa mti huo wa babu wa Loliondo si mgeni kwake na yeye alikuwa akitumia mti huo kwa kuchanganya na dawa nyingine kutibu wagonjwa sugu ila zaidi ilikuwa ni wale wenye matatizo ya miguu na kuwa dawa hiyo alikuwa akitoa dozi ya vikombe vitatu kwa zaidi ya miaka 18 sasa baada ya kuoteshwa na baba yake mzazi.



Akizungumza na blogu dada ya www.francisgodwin.blogspot.com mwenyekiti wa Chawatiata mkoa wa Iringa Christina Mgongolwa ,alisema kuwa watu wote walioibuka kutoa vikombe wanatumia miti shamba kama wanavyofanya waganga wa kienyeji na kuwa ni vema serikali sasa kutoendelea kuwapuuza waganga wa kienyeji katika kutoa tiba kwa jamii na kuwa kinachojitokeza sasa na nguvu ya Mungu katika kuliaminisha Taifa kuwa tiba hizo ni za kweli.


Hivyo alisema kuwa wao kama waganga wa kienyeji wanaungana na wenzao wote waliojitokeza na kutoa vikombe na serikali kuwaamini katika huduma hiyo na hivyo kuikumbusha serikali kuharakisha zoezi la utoaji wa leseni kwa waganga wote nchini akiwemo babu wa Loliondo ili kuifanya huduma hiyo kupanuka zaidi.




"Mungu ana makusudi yake kweli huyu babu wa Loliondo ametusaidia waganga sasa kutambuliwa na kuheshimiwa rasmi kwa kikombe hicho ambacho kinatumia dawa kama za kweli za miti shamba ...hivyo sasa ni vizuri serikali kubaliki wote kujitangaza kwani wapo wengine wanauwezo wa kutibu kwa nusu kiombe kutokana na tatizo la mgonjwa, alisema Mama Mgongolwa"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mwengine kaoteshwa huyooo!!

    ReplyDelete
  2. Cha kushangaza ni zile story za watu, hakuna aliejitokeza na vyeti, kuwa alikua anaumwa ukimwi na magonjwa mengine makubwa na kutuonyesha kwa vyeti vya vipimo kuwa kapona au wamepona.
    Tunaomba waje wajitokeze, watuambie, kuwa walikua wanaumwa na vyeti vya kuumwa hivi, na baada ya kikombe wakaenda tena kupimwa na vyeti wakapewa tena na tuvione!
    Zaidi ya hapo itakua kudanganyana tu kama kawaida yetu.
    Mara popo bawa, mara babu Loliondo, mama Tabora, Mama Morogoro, sijui ukiua albino unakua tajiri, au kuiona bibi kizee mwanza au shinyanga basi mchawi, au “wataalam” wamejaa Bagamoyo! Au Sumbawanga kumejaa wachawi na waganga (wakati ni maskini wa kutupwa, huku rasilimali za kila aina zimezagaa tu!).
    Tuachane hayo mambo ya imani za ajabu.
    Tukumbuke dini ilianzishwa na binadamu na ndo maana kila kukicha wazungu wanabadilisha masharti ili yaendane na maisha yao! Kama waarabu ndo usiseme, yalioandikwa kwenye koran yanakua machungu kwao, wanataka “democracy” isio na “majahedinas!”
    Leo sisi ndo tunajifanya hzio dini tulianzisha sisi na tuanzijua kinoma!

    Fumbueni macho wabongo!

    ReplyDelete
  3. Kaoteshwa tena na baba yake> dozi vikombe 3!. Binafsi naona haya ni yale Yahya alisema magonjwa sugu yatatibiwa mwaka huu!. Utabiri wa Shehe Yahya umetimia kwa kasi hivi!. Kwa kweli nyakati za mwisho hizi.

    ReplyDelete
  4. Mimi naamini tiba za asili kama mizizi, majani, magome ya miti, mbegu etc etc. Hizo naamini sana kwa vile hata hizi dawa za hospital zote zinatokana na michanganyiko ya vitu hivyo hivyo..Nisichoamini ni ile ya Babu kutaka kila mtu aende huko ili apewe kikombe na yeye. Kama hayo maji yatakua na the same ingredients kwa nini watu wasiende kuwachukulia tu na kuwapelekea ndugu zao wagonjwa na kueleza jinsi ya kunywa? Hiyo logic ya kuwa ni lazima yeye akunywishe hiyo dawa ndiyo siielewi. Is it fair kuona watu zaidi ya 50 wanakufa wakiwa wanasubiri kumwona? Common sense

    ReplyDelete
  5. http://www.newhabari.com/2011/04/04/loliondo-medicine-demystified/

    someni hii link,
    huu mzizi unaitwa Carissa Spinarum
    Widely used as traditional medicine in India, Maasai land, China and Australia
    It is anti viral hypoglycemic, anticonvalescent drug
    It does not require spiritual invocation
    Widely available in Chinese medicines outlets

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...