
Kamati ya mpito ya Jumuia ya watanzania waishio New York na vitongoji vyake, inawakaribisha Watanzania wote na marafiki zao, kujumuika kwenye mkutano utakaofanyika tarehe 30 April, 2011 saa nane mchana (1400hrs).
Anuani ya sehemu ya mkutano ni
30 Overhill Road,
Mount Vernon,
New York NY 10552.
Dondoo za mkutano zitakuwa kama ifuatavyo:
Kuitambulisha Jumuia.
Kujiunga na Jumuia.
Uchaguzi wa nafasi mbali mbali za uongozi.
Kuzungumzia hali ya maendeleo ya Jumuia ya Watanzania New York
Tafadhali nenda kwenye website ya
www.nytanzaniancommunity.org
kupata taarifa zaidi.
Fomu za kujiunga na Jumuia na kugombea nafasi zipo kwenye website, tunakusihi jaza fomu zote. Tunaomba wakina mama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hizo na jitihada zitafanyika kuzingatia gender kwenye uongozi. Shukrani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...