Home
Unlabelled
alama mpya za jiji la dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Asante sana Michuzi kutuletea haka kavideo. Kajiji ketu si kabaya kanaweza kuingizwa kwenye ushindani na baadhi ya miji mizuri hapa Africa. Ila niliwahi kusoma habari zake kwenye wikipedia nikaona wamekandia sana kuwa dar ni moja ya miji iliyojengwa kizamani sana, mitaa ni finyu, nyumba zimesongamana hata mzunguko wa hewa unakuwa mdogo ndio maana joto linazidi. Tatizo kubwa ni kwamba wananchi nao tunachangia kuufanya mji wetu usivutie kwa kiwango cha juu. Kwanza tunatupa taka hovyo, pili tunavuka barabara mahali popote, tatu wenye magari hawajali utunzanji wa kingo za barabara, hatujali kutunza miti au maua yaliyopandwa n.k. Kwa ujumla hatufuati sheria za utunzaji wa miji. Lakinio pia serikali nayo inachangia hali hiyo kwani ilitakiwa kuwepo na mapipa ya taka kila baada ya hatua kumi, taa za kuvuka barabara kwa watembea kwa miguu ziongezwe kila mahali pengi, na mwisho wananchi wapewe elimu juu ya umuhimu wa kutunza miji yetu. Miji ya wenzetu ni mizuri kwa sababu ni wastaarabu,sheria zinafuatwa na vitendea kazi sio issue.
ReplyDeleteSasa ninyi waandishi wa habari mngechukua jukumu ka kutengeneza documentary za miji mbali mbali ikilinganishwa na DAR ili muzitumie kuwaelimisha watu kuhusu kufuata kanuni za kutunza miji. Ingependeza.
Mtoa maoni hapo juu nakupa pole sana kwa nia nzuri uliyo nayo lakini kwa wabongo kuheshimu shria au taratibu itachukua karne nyingi sana. Si viongozi wetu wala wananchi wanajua umuhimu wa kuheshimi taratibu zinapowekwa. Japo si wote lakini wachache wazuri hawaonekani.
ReplyDelete