Na Ripota wa Globu ya Jamii,Tarime
MBUNGE wa Singida Mashariki (CHADEMA) ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani bungeni Mh. Tundu Lissu pamoja na watu wengine saba, wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime na kushtakiwa kwa makosa matatu, huku wakinyimwa dhamana.
Mh. Lissu pamoja na watu hao saba akiwamo mkurugenzi wa Sera wa CHADEMA Bw. Mwita Mwikabwe Waitara, wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka na Hakimu Yusto.
Shitaka la kwanza ilielezwa kuwa washtakiwa hao waliingia chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Tarime, bila ya kibali wala ruhusa.
Katika shitaka la pili ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walizuia kufanyika kwa shughuli na kuendelea kutolewa kwa huduma za kiafya katika Hospitali hiyo.
Shitaka la tatu ilidaiwa kuwa walifanya makusanyiko ya watu yasiyo na kibali katika Hospitali hiyo, hivyo kuhatarisha amani.
Hata hivyo baada ya kumalizika kusomewa mashtiaka upande wa Serikali ulimuomba Hakimu kutotoa dhamana kwa sababu za kiusalama, ikihofiwa kuwa iwapo wangepewa dhamana kungeweza zuka machafuko.
Ombi hilo lilipokelewa na Hakimu, aliyeahirisha kesi hiyo mpaka kesho atakapotoa uamuzi wa dhamana au la, hivyo washtakiwa hao walipelekwa katika gereza la Tarime.
Hali ya ulinzi ilikuwa imehimarishwa, huku barabara ikiwa imefungwa kuzuia watu kuingia katika mahakama hiyo. Washtakiwa hao walifikishwa wakiwa ndani ya magari saba ya Polisi chini ya ulinzi mkali.



wanafiki na uroho wao wa madaraka .....mwisho wao tutauona..vurugu za nini???upuuz tu....I HATE CHADEMA.....
ReplyDeletemh wewe nawe!
ReplyDelete