Na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania imewataka watalaam wa tasnia hiyo kusaidia wasanii kuhakikisha kuwa wanaandaa kazi nzuri zinazokidhi viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa ili kuchangia katika pato la Taifa na wasanii kujinufaika na kazi zao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo alipokutana na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosoma Shahada ya Uzamili katika tasnia ya sanaa za Maonyesho na Sanaa za Ufundi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu tasnia ya filamu nchini.
Alisema kuwa hivi sasa baadhi ya wasanii wanaharakisha kufanyakazi bila kufanya utafiti wa kutosha kuhusu kazi wanayotarajia kuzalisha hivyo kutoa filamu zisizo na utafiti wa kina na nyingine kutozingatia maadili.
Bi. Fissoo aliongeza kuwa athari zinazojitokeza kutokana na watengenezaji wa filamu kutozingatia Sheria ya Filamu ni kuongezeka kwa vibanda visivyo rasmi vya kuonyeshea filamu zisizozingatia maadili ya kitanzania .
Alisema kuwa athari nyingine ni wasanii kutonufaika na kazi zao pamoja na kutumia gharama nyingi za utengenezaji, akitolea mfano kwamba kama filamu haikuzingatia maadili hata kamaimeshatengenezwa ni lazima irekebishwe hivyo ni wajbu wa mtengenezaji kufuata sheria kabla ya kutengeneza.
Alieleza kuwa ili kuhakikisha kuwa tasnia ya filamu inapata usimamizi mzuri nchini , mwaka 2009 Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo imeunda Bodi katika halmashauri za wilaya zote hapa Tanzania ambazo makatibu wake ni Maafisa Utamaduni wa maeneo chini ya usimamamizi wa Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu.
Naye Mwalimu kutoka Idara ya Sanaa za Maonyesho na Ufundi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bw. Charles Kayoka alisema kuwa ni vizuri wasanii wa filamu wakajenga umoja ili waweze kuwa na nguvu kulinda maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla .
Bw. Kayoka pia aliwataka viongozi wakubwa wa nchi kama Rais, Mawaziri na Viongozi wa vyama vya siasa kushiriki katika Siku ya Utamaduni Duniani ili kujionea changamoto na hali ya wasanii kwa kuwa ndio watengeneza sera za nchi.
Alisema kuwa Bodi iwaelemishe na kuwahamasisha wanahabari ili waweze kuelewa ni nini maana ya msanii kwa kuwa siyo kila anayetokea kwenye filamu na kuigiza ni msanii pia wasanii nao wahamasishwe ili wawe tayarai kujifunza na kujiendeleza katika tasnia hiyo.
Kwa upande wa wanafunzi hao walionyesha kuguswa kwao na namna wasambazaji wanavyowanyonya wasanii wa filamu kiasi cha kuwakatisha tamaa huku wakitolea mfano CD za Filamu zinavyomwagwa chini na kuuzwa shilingi 1000 hali inayodidimiza wasaniii kiuchumi pamoja na kulikosesha taifa kipato.
Walipendekeza kufanyike zoezi la kushitukiza na kuzikamata na kasha kuziharibu ili kutoa fundisho kwa watu wanaoiba kazi za wasanii kwa maslahi yao binafsi.
Naye Bw. Jumanne Samson, ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika masuala ya sanaa chuoni hapo akitoa mchango wake aliipongeza Bodi ya Filamu kwa kazi nzuri pamoja na kuongeza kuwa ni vema ikaongezewa nguvu kwa ajili ya kuifanya tasnia ya filamu kutoa mchango mkubwa kwa pato la Taifa kama ilivyo nchini Marekani na kwingineko.
Hata hivyo, Bw. Samson aliitaka Bodi kushiriki katika Mjadala wa jukwaa la sanaa unaoratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambao hufanyika kila Jumatatu ili kusikiliza mawazo ya wasanii.
Wakati huo huo Katibu huyo alisema kuwa kanuni za utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ya filamu na Michezo ya kuigiza iko katika hatua ya mwisho na itaanza kutumika hivi karibuni kwa jili ya kuipa meno zaidi Bodi hiyo.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuanza kwa kanuni hiyo ndio utakuwa mwisho kwa wazalishaji na wasambazaji wanaopitisha kazi zisizozingatia sheria na maadili kwani zitatoa adhabu kali kwa watakaokiuka.
Kwa mujibu wa Sheria Na. 4 ya mwaka 1976 Bodi ina wajibu wa kupitia miswada na kutoa vibali vya utengenezaji kwa watengenezaji wa filamu toka ndani na nje ya nchi pamoja na kukagua filamu na kutoa ruhusa ya kuonyesha hadharani.
Pia, Bodi ina wajibu wa kukagua na kutoa leseni za majumba ya sinema nchini, kupitia miswada na kuratibu maonyesho ya michezo ya kuigiza na kutoa vitambulisho kwa wasambazaji wa filamu na wafanyakazi wao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...