KITUO CHA KUKUZA VIPAJI CHA TSA

Kituo cha kukuza vipaji cha Tanzania Soccer Academy (TSA) kinachoendeshwa kwa ubia kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Kiliwood kimesimamisha shughuli zake tangu mwaka jana.

Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha kwanza mwaka huu ilishafanya uamuzi juu ya uendeshaji wa kituo hicho na kutoa maelekezo kwa Sekretarieti ya TFF. Kwa vile kituo hicho kilichokuwa kinachukua vijana wenye umri kuanzia miaka 17 hadi 20 ni cha ubia kati ya TFF na Kiliwood uamuzi wowote juu ya mustakabali wake ni lazima uhusishe pande hizo mbili.

Kwa mantiki hiyo Sekretarieti kwa sasa inafanya mawasiliano na kampuni ya Kiliwood ili pande hizo mbili zikutane na kuelezana juu ya uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF juu ya mustakabali wa kituo hicho.

Wajibu wa TFF katika mkataba kati yake na Kiliwood juu ya uendeshaji wa kituo hicho ni vitendea kazi (facilities) ambavyo ni hosteli na uwanja wa mazoezi.

KOZI YA WAKUFUNZI WA MAREFA

TFF kupitia Kurugenzi ya Ufundi imeandaa kozi ya wakufunzi wa marefa wa mikoa itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 1 hadi 4 mwaka huu.

Kozi hiyo inatarajia kushirikisha wakufunzi wa marefa zaidi ya 20 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara. Mara ya mwisho kozi hiyo ilifanyika nchini mwaka 2008.

Wawezeshaji katika kozi hiyo ni Stanley Lugenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Leslie Liunda, Joseph Mapunda, Hafidh Ally na Juma Hamisi.

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...