Kizungumkuti cha maegesho ya magari kama ambavyo Globu ya Jamii kimeshuhudia asubuhi hii jijini Dar eneo la 'Avalon'. Hapo weka kando foleni ya kuingia na kutoka katikati ya jiji. Je, kifanyike nini kupunguza kwikwi hii? Je, ni nani wa kuwajibika kwa hili?
Je, Mipango miji mpoooo???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2011

    hapo dawa ni kujenga ghorofa 2 tatu zenye floor kadhaa kwa ajili ya parking uwanja mkubwa sana huo....wabongo hata kufikiria tabu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2011

    Mbona jambo dogo tu hilo. Watafute mwekezaji ajenge parking ya ghorofa!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2011

    Hapo serikali ya jiji ilihitajika kama miaka mitano iliyopita kuwa imeishainua jengo la kuegesha magari la ghorofa kama nne au tano hivi katika hiyo parking lot. Tatizo letu bongo - kuanzia serikali ya mtaa hadi kuu - tunazima moto (reactive) badala ya kuzuia moto (proactive). Hiki ndicho kimekuwa kikwazo kikubwa katika suala la miundombinu.

    ReplyDelete
  4. Mangi wa KiboshoMay 11, 2011

    Bongo hakuna watu waliosoma mamabo ya mipango MIJI jamani! Hata pale Chuo cha ardhi wanajua hilo! wapo watu waliosomea kuhusu KUUZA VUWANJA TU!
    Kama kuna anaebisha aingie ktk globu yetu hii nimuumbue

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2011

    Mimi nitakubisha, hakuna aliyesomea kuuza VUWANJA!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2011

    public transportation ndo suluhisho la haya yote.Waendesha magari wakitumia daladala huu msongamano ktk parking lots utapungua vile vile msururu barabarani utapungua.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2011

    Wadanganyika, mbona mawazo yetu ni finyu hivi? Ujenzi wa ghorofa za parking utapunguza usumbufu wa parking, tena kwa muda tuu. Je tatizo la foleni litaisha?

    Mtazamo wangu suluhisho ni kuanzisha miji mipya sehemu kama Mbagara, Kimara au Mbezi, na Tegeta ua Bungu. Na hapo mjini kuziacha ofisi chache tuu ambazo kweli zina mahitaji muhimu ambayo ni taabu kuyapata sehemu zingine, kwa mfano bandari, TRA customs office nk. Office kama Wizara ya Mali Asili, Ardhi na nyinginezo zihamishwe.

    Kutumia vyombo kama NSSF, NHS na wadau wengine hili linawezekana. Na faida yake ni kubwa;

    > si tuu kupunguza foleni bali pia kuwapunguzia raia ukakasi wa maisha na hivyo kuondoa ulazima wa kusaka noti si halali.
    > kuongeza afya kwa raia, hasa watoto maana sasa inawalazimu waamke usiku wa manane ili waweze kuwahi maufisini ua mashuleni.
    > kurahisisha shughulika na mambo ya usafi na usalama.

    FAIDA ZIPO NYINGI SANA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 11, 2011

    tena hapo pana wezi , mimi imenitokea nilikwenda hapo nikawa napaki gari akaja yule kijana anayeosha magari akawa ananielekeza kupaki gari kumbe wakati huo alifungua mlango wa gari yangu wa pili bila mimi kujua , mi nakshuka kwenye gari bila kujua mlango wa abiria uko wazi kule na kilihonisaidia ni kwamba gari yangu ilikuwa inatumia alarm kufunga gari kwa remont , kila nikibonyeza alarm gari inakataa kufunga milango , yule kijana akawa ananiangalia ... nikajua ni yule kaufungua maana alikuwa karibu na huo mlango na alijifanya kunielekeza kupki gari vizuri , nikamfata kijana anayekata parking ticket na kumueleza kilichotokea kuwa huyo kijana alitaka kuiba ktkt gari, lakini kwa bahati mbaya hakuweza kunisaidia , nikajua kwamba yule nae alikuwa najua huo mchezo, nikasoma namba ya yule mwenye kukata ticket parking na nikaenda ofisi ya parking ambayo iko karibu sana na hapo , nilipofika ofisini nikawakuta wahusika nikanza kuwaeleza , wakaniambia hizo kesi zipo hapo kama 99 ya kwangu imekuwa ya 100 , wakaanza kunihadisia sijui juzi mzungu kaibiwa laptop sijui mara hivi , sasa mimi nikawauliza sasa nyie hamchukui sheria yoyote juu ya hawa wezi ? akasema tulishawahi kufuatilia na kuwakamata sana lakini baada ya lisaa limoja wanakuwa washarudi hapo , na akasikitika kwa kusema kuna siku walimkamata mmoja na akafungwa pingu na askari kwa ajili ya kupelekwa kituoni lakini cha kusikitisha kwamba yule askari alimuomba rushwa ya 10,000 yule kijana akawa hana akamwambia ngoje nikachukue kwa wenzangu basi yule askri akamwachia yule mtuhumiwa akiwa na pingu zake aondoke mpaka kwa wenzie akiwa na pingu mkononi na yule askari akabaki huko akimsubiria alete 10,000 ndo alipoleta akawmachia ....

    SASA TAHADHARI KWA WOTE WENYE KUPENDA KUPAKI HAPO NA SEHEMU ZINGINE UKIWA UNAPAKI GARI UKIOONA HAO VIJANA WANAJIFANYA KUKUSAIDIA KUPAKI GARI KWA KUKUELEKEZA BASI KUWA MAKINI , HAKIKISHA UKISHASHUKA KATIKA GARI YAKO THEN ZUNGUKA MILANGO YOTE YA GARI NA HAKIKISHA IMEKUWA LOCK

    ASANTE MICHUZI
    MDAU KKOO

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2011

    hapo wala hata msiwe na wasiwasi mifuko kama LAPF wana mpango kambambe wa kujenga parking ya kisasa ya ghorofa nane kama ambavyo watafanya maeneo ya Mbezi Luis kuondoa msongamano wa mabasi ubungo kwa kutengeneza stendi ya kisasa na kuondoa msongamano uliopo Ubungo ivi sasa mabasi na malori yote hakuna kuingia tena mjini,mwisho wake ni maeneo ya kimara

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 11, 2011

    nimeshangazwa watu hawatoi maoni ya ku-improve public transport..badala yake wanakazania kutaka magorofa ya parking kujengwa..hivi wakijenga twin towers za ghorofa 100 eneo la posta foleni zitapungua..?? watu wananunua magari kwasababu daladala sio usafiri...ukiona mtu anapanda daladala Bongo ujue kichwani anayo ndoto ya kununua gari siku mmoja na sio kwamba anafurahia dala dala...

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 11, 2011

    kila ghorofa inayojengwa iwe ni lazima kuwa na parking garage angalau foor mbili

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 11, 2011

    Moja ya mapato makubwa ya serikali ni kujenga parking za magari katika miji na kuhakikisha kunakuwa na utaratibu wa ukusanyaji wa pesa sio mtu anakuja na ticket zake anakuuzia kama ilivyo hivi sasa, huku ni kuhujumu mapato ya sarikali.Parking zingekuwa zinamilikiwa na serikali za mitaa hicho ni chanzo cha mapato kwa serikali sio kumwachia mtu awakusanyie kwani nchi zingine hizi parking zinasaidia sana na hakuna hata parking mmoja inayomilikiwa na mtu binafsi ila kuna makampuni ambayo yanapewa jukumu la kuendesha, hivyo hapo hakuna ubabaishaji.
    Mtaalamu wa parking space.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 12, 2011

    URBAN PLANNING, TRAFIC MANAGEMENT VIKO WAPI?SERIKALI INATAKIWA IANZE KUENDELEZA CENTRES ZINGINE ZA MJI, TWENDENI NA WAKATI TUANGALIE NA MIJI MINGINE INAENDELEZWAJE! HIYO MIJI LA LONDON NA NEW YORK HATA HAPPA JIRANI TU NAIROBI KUNA BUSINESS CENTRES NYINGI!!!!!!!!!!!!!GOVERNMENT WAKE UP PLEASE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...