Baada ya taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans. Kampuni ya kimarekani ya Symbion Power yenye makao yake makuu Washington DC , leo imethibitisha kwamba imekwisha weka sahihi mkataba wa ununuzi wa mitambo hiyo iliyopo Ubungo Dar es Salaam .
Paul Hinks, Meneja Mtendaji wa Symbion amewaambia wanahabari sasa hivi katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kuwa, “mazungumzo na Dowans yalikuwa ni magumu hasa ukizingatia historia ya mradi wenyewe. Kwa hiyo ilibidi kufanya uchunguzi wa kina kujiridhisha na kila kipengele cha makubaliano na pia ubora wa mitambo na tumejiridhisha kuwa mitambo hii iko katika hali nzuri ya matunzo”.
Hinks aliendelea kusema “nafarijika kusema kwamba sasa tumemaliza na kukamilisha mkataba wetu na Dowans na tupo tayari kuzalisha umeme hapa nchini. 120MW inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya umeme hasa ukizingatia kuwa nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la mgao wa umeme. Lakini, laiti kama TANESCO haitaafiki, tuna miradi mingi duniani ambayo inahitaji mitambo hii.
"Pamoja na ukweli kwamba tunauwezo wa kuitumia mitambo hii pengine duniani, Symbion inakusudia kupendekeza kwa TANESCO waridhie mitambo hii itumike hapa nchini. Mitambo hii imefanyiwa majaribio hivi karibuni na wataalamu wa kimataifa na imedhibitika kuwa iko katika hali nzuri Hinks pia kafafanua kwamba Symbion itashirikiana na kampuni ya Kimataifa ya kimarekani ya ProEnergy Services (PES) ambayo inauwezo na uzoefu mkubwa katika sekta ya umeme yenye makao yake makuu Missouri , Marekani. PES ambayo inajishughulisha na uzalishaji wa umeme sehemu mbalimbali duniani itakuwa ni mbia wa kutoa huduma ya uhandisi na uendeshaji wa mitambo.
Amesema Symbion Power tayari inauzoefu mkubwa katika miradi ya umeme ambayo inafadhiliwa na Serekali ya Marekani kama vile yale yaliyo chini ya Millenium Challenge Corporation. Symbion pia inashughulika na usambazaji wa umeme vijijini Tanzania inayojumuisha takriban kilometa 3,000 ya miundombinu ya kusambaza umeme.
Wakati huo huo, mwenyekiti wa Symbion Africa, Balozi mstaafu wa marekani katika nchi mbalimbali, Joe Wilson, alisema mitambo tuliyoinunua iliyoko Ubungo, imekaa bila kutumika takriban miaka mitatu sasa, wakati nchi imekuwa ikipata matatizo makubwa ya mgao wa umeme inayoleta changamoto katika uchumi wa nchi. Kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi ya Symbion, nasema tutafarijika ikiwa TANESCO itahitaji huduma kutoka kwetu”.
Symbion ni kampuni ya Kimarekani yenye makao yake makuu Washinton DC Marekani. - www.symbion-power.com
Ambassador Alfonso E. Lenhardt's Statement on Symbion Power Acquisition of the Power Plant in Ubungo
"We are pleased with the announcement that Symbion Power has decided to invest in Tanzania by acquiring a 112-megawatt power plant. Energy is essential to support industry, agriculture, the education and health sectors, social services, and reliable water supply. The private sector will have an important role to play in providing long-term energy solutions in Tanzania. We support the Ministry of Energy’s effort to attract investors and facilitate public-private partnerships. We encourage Tanzania to continue improving conditions for investment. The United States actively promotes investment by American companies in Tanzania."
Ambassador Alfonso E. Lenhardt




this is a joke right???????kumbe do once imezimwa wakasingizia gas imefanya nini sjui ndo mana mgao....alafu wanatusaidia kulipa na lile deni ama?
ReplyDeleteNahisi huu mgao unaoendelea ni kwa ajili ya kuwawekea mazingira mazuri hawa jamaa. It will soon be clear...
ReplyDelete"mambo ya siasa kwao hayana nafasi bali ni kazi tu na blah blah pembeni" - hii inafuraisha sana na kutia matumaini. Lakini wakumbushwe kuwa hizo zilizobatizwa 'siasa na blah blah' hapa bongo hazitazuilika iwapo kuna harufu yo yote ya ufisadi. Kama wamewnunua mzigo wa Dowans wakilijua hilo basi tunawakaribisha kwa mikono miwili. welkom to bongoland.
ReplyDeleteWow! Finally, This is one of BREAKING NEWS I've been waiting for. For decades Tanzanians have being living in dark ages, now Americans will light up Tanzania. Symbion is among the biggest power producer in Arab countries now to Tanzania!! Hope this deal will move smoothly without political propagandas
ReplyDeleteGod bless The United States and God bless Tanzania and Tanesco.
Great move for all individuals who made this deal possible
Mdau, Houston TX.
Staff Vacancies
ReplyDeleteSP/TZ/101 Regional Financial Controllers
Project Location: Tanzania, East Africa
Candidates must have a minimum of 5 years experience as a Financial Controller and recognized qualification as an accountant.
Read full description >
SP/TZ/102 Regional Construction Managers
Project Location: Tanzania, East Africa
Distribution line and substation managers with at least 10 years experience of project management in a power engineering construction company.
Read full description >
SP/TZ/103 Commercial Manager
Project Location: Tanzania, East Africa
20 years experience as a Quantity Surveyor with at least 5 years experience as Chief Quantity Surveyor or Commercial Manager.
Read full description >
SP/TZ/104 Distribution Line Supervisors
Project Location: Tanzania, East Africa
Wood pole distribution line supervisors who have at least 10 years experience...
Read full description >
SP/TZ/105 Substation Construction Engineers
Project Location: Tanzania, East Africa
Engineers with a recognized engineering degree who will supervise the erection and commissioning of 132kV and 33kV substations.
Read full description >
SP/TZ/107 Human Resources and Personnel Manager
Project Location: Morogoro, Tanzania
An HR Manager with 10 years experience in Tanzania dealing with a large labor force in excess of 1000 employees. Based in Morogoro. Must speak Swahili.
Read full description >
Wanted: Experienced People for Important Work
Project Location: Africa and Middle East
Position: Various
Symbion Power is continuously seeking intelligent, ambitious, and experienced employees for its work delivering complex power engineering solutions to the world's developing nations.
Read full description >