MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe John Mwankenja (pichani) ambaye ni diwani wa kata ya Kiwira ameuawawa kwa risasi usiku huu majira ya saa 5.00 wakati akishuka kwenye gari lake kuelekea nyumbani kwake.
Habari zilizoufikia mtandao huu zinaeleza kuwa alimiminiwa risasi kadhaa wakati akishusha mguu wake kutoka kwenye gari ili kuingia nyumbani kwake eneo la Kiwira.
Maiti yake inapelekwa hivi sasa hospitali ya Makandana kwa kuhifadhiwa, na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambalo kwa ujumla linaaacha maswali mengi kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe na mkoa kwa ujumla.
Tutaendelea kupeana taarifa zaidi kadri ripota wetu aliopo Rungwe atakavyokuwa anatuhabarisha.
Msiseme ni CDM tu, maana kila kitu siku hizi lawama nimkwa wapinzani.RIP marehemu.
ReplyDeleteMWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMINA.PIA AKAWAPE ADHABU WALE WALIOJICHUKULIA SHERIA NA KUMUUA JOHN.(R.I.P)
ReplyDeleteMaskini ya Mungu, yaani binadamu tumekuwa wakatili kiasi hiki!!!! Eee Mungu umpatie Pumziko la Milele mja wako asiye na hatia.
ReplyDeleteKama sio majambazi then ni siasa tuu!! Watanzania tujiadhari sana na mbegu za chuki zinapandikizwa na wanasiasa!! Nikijiuliza ni faida kiasi gani imepatikana baada ya kumuua huyu bwana sipati jibu!! Police akikisheni wauaji wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za haraka hili hiwe fundisho kwa watu wote wanaofikiria kuwa njia ya kuuwa binadamu ni sahihi katika mambo ya saisa!!
ReplyDeletePoleni sana wafiwa!!
Kwa kweli kuna baadhi ya binadamu wamepoteza kabisa utu; hakuna kitu cha kutisha kama kupoteza uhai wa mtu bila ridhaa ya Mwenyezi Mungu, acha Mungu afanye kazi yake na si kujichukulia sheria mkononi, haipendezi kabisa, Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.
ReplyDeleteMola awape faraja wafiwa.