
- Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, akizungumza na viongozi na wawakilishi wa TUICO, wageni waalikwa , Wakurugenzi na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa hafla ya kutia saini Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinsky jijini Dar es Salaam. Mkataba huo unalenga kufanya maboresho kadhaa kwa wafanyakazi ili kuleta mazingira bora ya kufanyia kazi na mahusiano bora kati ya Mwajiri na Wafanyakazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB Bi. Tully Esther Mwambapa na Katibu wa Benki hiyo Ndugu John Rugambo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, Katibu Mkuu wa TUICO Taifa Ndugu Jonathan Pelesi (wapili kushoto), na Mwakilishi wa ILO, Ndugu Magnus Minja (Kulia), wakisaini Mkataba wa Hali Bora kwa Wafanyakazi wa Benki ya CRDB katika hafla hiyo. Waliosimama, kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Majadiliano TUICO na Benki ya CRDB, Bw.Christopher Mleju na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki hiyo Bi Dorah Ngaliga.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...