Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akimkabidhi Bw. Michael Njumba ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Investment Solution hati maalumu ya shukrani  ya utambuzi wa elimu iliyotolewa na taasisi ya elimu nchini (TEA).

Dr Shukuru Kawambwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa wa kagera, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (OUTSO) na baadhi ya watumishi wa chuo hicho kikuu.

Dr kawambwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa majengo yaliyotolewa na mfanyabiashara maarufu jijini Dar es salaam Bw. Michael Njumba anayemiliki kampuni ya Investment solution. Bw. Njumba ni aliyesimama kushoto  kwa Dr Kawambwa na anayefuata ni mkuu wa mkoa wa kagera Mh. Mohamed Babu.
 

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr Shukuru Kawambwa akipanda ngazi za jengo la utawala ya chuo kikuu huria kituo cha Bukoba kwa lengo la kukata utepe, waziri huyo alikuwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa serikali vyama vya siasa, viongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho na watendaji wa chuo hicho.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr Shukuru Kawambwa akiteta jambo na Michael Njumba (kushoto) ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Investment solution iliyotoa majengo yatakayotumiwa na chuo kikuu huria nchini kituo cha Kagera wakati wa sherehe za uzinduzi wa majengo hayo zilizofanyika chuoni hapo jana, katikati yao ni makamu mkuu wa chuo hicho huria Profesa Tolly Mbwette.
Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii,Bukoba. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...