Matangazo ya Zanzibar  yakionyeshwa katika mechi ya ligi Kuu ya Marekani kati  ya  Seattle Sounders na na timu kutoka Arizona ambapo watazamaji  zaidi ya elfu hamsini walihudhuria mechi hiyo huku  watazamaji zaidi ya milioni ishirini waliona mechi  hiyo  katika TV. 

 Matangazo ya Mlima Kilimanaro yakiamba uwanja
 Tangazo la kuvutia watalii wa Kimarekani watembelee Tanzania
 Afisa wa Ubalozi wetu Washington DC Bw. Suleiman Saleh akikaribishwa kwa matarumbeta wakati ujumbe wa Tanzania ulipotembelea uwanja wa Seattle Sounders kuona jinsi tutavyoweza kujitangaza kwa watalii
Bw. Suleiman Saleh  Afisa  wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC akiwa na Makamo  Mwenyekiti wa Seattle Sounders/Seattle Hawks Bw. Lanz  na Dk. Ezekiel  Dembe wa Tanzania National Parks (TANAPA) wakati wa ziara hiyo. 



Tanzania itapata nafasi hivi karibuni ya kutangazwa zaidi kiutalii  nchini Marekani kufuatia mazungumzo yaliyoanza baina ya  Serikali ya  Tanzania na klabu ya soka ya  Seattle Sounders ya  Washington,Seattle ambayo pia inamiliki timu ya  Seattle  Hawks ya American Football. 

Ujumbe wa Tanzania wa  Bw. Ezekiel Dembe Ofisa   kutoka  Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Bw. Suleiman Saleh, Afisa wa Ubalozi wetu Washington DC umefanya mazungumzo na uongozi wa klabu maarufu  ya soka ya Seattle Sounders na Seattle Seahawks ( American  Football) ambazo wamiliki wake ni wamoja kuangalia uwezekano  wa Tanzania kujitangaza kiutalii nchini Marekani, hususan kwenye michezo ya klabu hizo kubwa. Ujumbe ulifika katika dimba la Seattle Sounders wakati wa mechi  yao ya ligi ya Marekani (MLS) walipocheza na Arizona na  kushinda bao 1-0.


Ujumbe huo ulipokelewa kwa nderemo nje ya uwanja wa  Seattle Sounders ambao kikundi cha matarumbeta kiliwatumbuiza,  kabla ya wageni kwenda kushuhudia mandhari ya  Uwanja wa Saunders ambapo watazamaji  wapatao 50,000  walihudhuria mechi ya Saunders na watazamaji zaidi ya  60,000  walihudhuria mechi Sounders Sea Hawks ya  American Football huku matangazo ya majaribio yakipamba  mechi hizo kuitangaza Tanznaia na Zanzibar, ambapo tayari simu za ubalozini zimeanza kuigwa na  Wamarekani kibao waliovutiwa na Tanzania na vivutio vyake.

 Bw. Lanz, Makamu wa Rais wa  Seattle Sounders 
akimwelezea Bw. Saleh masuala ya klabu yao 
Bw. Saleh na  Bw. Dembe wa TANAPA  wakiwa na mmiliki wa Seattle Sounders Bw.  Adrian ndani ya dimba la Seattle Sounders wakati wa mechi  yao ya ligi ya Marekani MLS walipocheza na Arizona na  kushinda 1-0

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...