Mojawapo ya kiplefti kibao zilizoumuka katika mitaa kibao ya jiji la Dar linaendeleza libeneke katika mtaa wa Chole karibu na International School of Tanganyika, Masaki. Huenda anasubiriwa JK aje afungue rasmi maana hii ni wiki ya nne bado linakenua.
------------------------------------------------
------------------------------------------------
Habari Ankoli
Pole na hongera kwa shughuli za kutuhabarisha kila kukicha. Leo nami napenda nijitokeze kutoa walau comment moja katika hiyo picha ya 'keep left' cha masaki. Kwa kuitazama na kuichunguza kwa undani nadhani nimepata jibu ni kwanini haifanyiwi marekebisho. Jibu ni kuwa ni 'alama ya taifa'. Ukiichunguza vizuri hiyo picha hasa kama umesimama kushoto (kama unaitazama picha) utagundua kuwa imefanana kwa kiasi na ramani ta taifa letu pendwa hence ni kitambulisho kwa wageni na ndo maana linaachwa. Kilichobaki hapo ni kuongezea tu hapo kulia vishimo kadhaa kuwakilisha visiwa vya marashi ya karafuu aka Zanzibar.
Ni hilo tu kwa leo
Its me a candid Michuzi Blog supporter
Raymond Binya
London - UK


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...