Mbunge Wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji

Na.Mwandishi wetu.

Mbunge Wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji Ameitakia Kila La Kheri Timu Ya Simba Katika Mchezo Wake Wa Kuwania Kufuzu Kwa Hatua Ya Makundi Katika Michuano Ya Klabu Bingwa Afrika Dhidi Ya Wydad Casablanca Ya Morocco.

Mh. Mo Amewaambia Simba Kuwa Yuko Pamoja Nao Katika Dua Akiwaombea Mafanikio Ili Waweze Kuvuka Kizingiti Kilichopo Mbele Yao Na Kuwapa Watanzania Furaha Kwa Kushinda Katika Mchezo Huo Utakaochezwa Juni 28 Mwaka Huu Mjini Cairo.

Amesema Kitendo Cha Rufaa Yao Kukubaliwa Huku Timu Ya Tp Mazembe Ikiondolewa Na Simba Kuendelea Ni Ishara Ya Nyota Njema, Hivyo Wasipoteze Nyota Hiyo Ambayo Tayari Imeshaanza Kung’aa Na Badala Yake Waing’arishe Zaidi Kwa Kuwaadhibu Wamorocco Hao.

Mo Amewataka Wachezaji Wa Simba Kuwa Na Ujasiri Na Kujiamini, Na Kuwataka Wakumbuke Kile Timu Ya Simba Ilichokifanya Katika Michuano Kama Hiyo Mwaka 2003 Kwa Kuwatoa Timu Ya Zamalek, Basi Warudie Kitendo Hicho Hicho Ili Historia Ya Simba Ijirudie Na Kuweka Heshima Katika Medani Ya Soka Tanzania Na Afrika Kwa Ujumla.

Aidha Ametaka Watanzania Wote Tuondoe Tofauti Za Usimba Na Uyanga Na Tushirikiane Pamoja Katika Kuiombea Simba Dua Ili Ishinde, Kwa Kuwa Ushindi Wa Simba Ni Wa Watanzania Wote Na Sio Wa Wana Msimbazi Peke Yao.

Kwa Upande Wake Amewaahidi Zawadi Nono Wachezaji Wa Simba Iwapo Watafanikisha Azma Ya Kuwaondoa Wydad Casablanca Katika Mchezo Huo Wa Mkondo Mmoja Utakaochezwa Kwenye Uwanja Huru.

“Mimi Kama Mohammed Dewji Kwa Niaba Ya Wananchi Wote Wapenda Soka Nawaahidi Donge Nono, Lakini Sita Litaja Mpaka Hapo Mtakapo Tupa Raha Watanzania Kwa Kurejea Na Ushindi”.

Mh. Dewji Ametaka Watanzania Wote Tutumie Mchezo Huu Wa Simba Na Wydad Casablanca Kama Kiunganishi Na Tuwe Wamoja, Kwani Michezo Ni Furaha, Michezo Ni Upendo, Michezo Ni Afya Na Michezo Hujenga Umoja.

Kila La Kheri Simba Nawatakieni Ushindi Mnono Katika Mchezo Wenu.

“Simba Funga Hiyo Casablanca Bao Nyingi Za Kutosha Uingie Hatua Ya Makundi” Alisema Mo.

Mungu Ibariki Simba Sc

Mungu Ibariki Tanzania.

Akhsanteni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2011

    Jana wakati naangalia kipindi cha "soccer africa" kinachorushwa na kituo kimoja cha TV cha Africa kusini maarafu sana katika mambo ya kandanda,niliona kituko."Presenters' walikuwa wanaongelea hili suala la mechi ya Simba na Wydad..katika mambo waliyoyazungumzia ni kwamba Misri haikuwa sehemu huru(neutral ground) kama CAF walivoybainisha na walisema kwamba Cairo inawabeba Wydad..Walipendekeza Mechi ingefanyika Africa ya kati,kusini au magharibu.Baada ya hapo wakaanza kuwahoji viongozi wa timu za Simba na TP Mazembe..Wakaanza na MR.Katumbi wa TP Mazembe(Huyo lugha aliyoitumia kuishambulia CAF haikuwa nzuri kwakweli)...Akaja Kiongozi wa Simba..AZIM DEWJI..akawa anaongea kama anaogopa(regrets)..oh mara tukienda Cairo tutavaa fulana za TP kuonyesha walivyoonewa...mara hatukupenda kucheza nafasi ya TP..mara tuko pamoja na TP kuilaumu CAF.!!!Baadae 'presenter' mmoja maarufu kutoka Africa Magharibi(nchi ya kifaransa) alimponda sana huyo Dewji kwamba kwamba yeye alimwona miaka ya 1990 na siyo kiongozi tena wa Simba..sijui wamemtoa wapi huyu..nk!!

    Presenter huyo huyo kutoka Africa Magharibi(kwenye nchi ya Kifaransa) alinikera sana pale aliposema eti wakati wa Fainali za CECAFA kati ya timu ya Tanzania(Taifa stars na timu ya Ivory coast)na kubeba ubingwa nchi ilikuwa inarindima(...the whole country was vibrating ...) kama vile tulikuwa tumebeba Kombe la dunia..!!Atuombe msamaha!

    David V.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...