MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba amemshutumu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa amekuwa mtu wa kukimbia, kujificha na kutosema ukweli kuhusu tatizo la umeme nchini.
Ngeleja anatupiwa shutuma kuwa kauli ya Serikali aliyoitoa bungeni juu ya hali ya umeme nchini ikiwemo kukodishwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 260 ifikapo Juni na Julai mwaka huu imeshindikana lakini Waziri yuko kimya.
“Waziri alisema bungeni na akamwambia Rais (Jakaya Kikwete) naye akalitangazia Taifa kuwepo kwa umeme ifikapo Julai, lakini kwa taarifa nilizonazo biashara hiyo imekwama na Waziri yuko kimya anakimbia kusema ukweli,” alidai Makamba.
January alidai kitendo cha Waziri kukimbia na kujificha, kinaonesha kuna ombwe la uongozi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na akaahidi kuwa Kamati yake itambana Waziri huyo aeleze utekelezaji wa mipango yote aliyoiainisha kwenye kauli ya Serikali.
Habari kamili nenda Habari Leo



Go Go Go MANYUZI ....
ReplyDeleteSafi kama una dhati hiyo ya kurekebisha utendaji ukiwa mwana ccm siyo lazima tusubiri wapinzani.fanya kazi januari tuone tofauti katika bunge na serikali hata chama chenu.Ila nawe usiwe nguvu ya soda pigana hadi mwisho.Just go...
ReplyDeleteNahitahi facebook address ya January Makamba au hata email yake binafsi ili tuongee hard facts, kwa sasa naona nisiseme kitu hapa
ReplyDeleteHakuna chochote madini yote yanpelekwa njea bila ushuru na wankijiji hawafaidiki choichote, Tembeeni jamani muone huko vijijini madini yakotoka hali halisi ipo namna gani? Matatizo ni makubwa huwezi ukajuwa kijiji kinazalisha mabilioni na wakati hawana maji , umeme, hospitali na shule bado ni duni. Hakuna dawa? watu hwajui wanchokifanya zaii ya kujwa gongo. Muoambieni aende akalale huko kwa hao wannchi aone maisha yao kwa ujumla na siyo unazungumzia ukiwa Dar kwenye Air condition. Bado hatuna viongozi, viongozi ni wale tu ambao wapo karibu na walal hoi walio wengi.
ReplyDelete