Kata funika, piga ua, garagaza hapajapata kutokea mpishi hodar wa pilau na biriani kwenye shughuli kama Saidi Bajia ambaye ameanza shughuli hiyo takribani miaka arobaini iliyopita na hadi sasa hana dalili ya kupunguza spidi. Katika shughuli yoyote iliyo jijini Dar hukosi kumkuta Saidi Bajia akiwa katikati ya shaba akifanya mambo yake. Hivi sasa kuna takriban waishi wa aina yake 12 ambao ni wanafunzi wake na anana fahari kubwa kuwana wanashamiri.
Home
Unlabelled
saidi bajia: bingwa wa kupika mpunga wa shughuli
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ok sawa ila jamani usafi mbele , hilo sufuria duh!
ReplyDeletemichuzi kwanza lazima uzitizame maoni kisha uyaweke huyu jamaa anasema usafi sasa hiyo sufuria amepikiwa sasa vipi itakuwa safi?
ReplyDeleteHilo sufuria ndilo linalomfanya awike zaidi katika hayo mambo ya pilau na biliani.
ReplyDeleteVipi Ali Mapilau?
ReplyDeletemafuta matupu..ndio maana magonjwa sugu yanaongezeka. Lakini afadhali sasa babu anatupatia tiba.
ReplyDeleteSUFULIA SIO CHAFU BALI IMECHAKAA TU. SASA ANZENI HARAMBEE ZA KUMNUNULIA SUFULIA MPYA, STOCK MARKET YAKE ITAONGEZEKA!
ReplyDeleteBABU BAJIA ENDELEA.... USIKATE TAMAA KWA MASIMANGO ..... TAFUTA MRITHI MAANA HIVYO NI VIPAJI ADIMU.
ReplyDeletenyie nyote mliotoa maoni yenu ni mazuli sana kwamba huyo mpishi msimpe lawama kwanza sio mafuta wewe utachompelekea ndicho atacho kupikia wewe mwenyewe sawa kwa hiyo hana lawama pili sufuria yeye ktk mapishi yake kwanza hatumii jiko la umeme,hatumii pia jiko la gesi kwa hiyo jibu unalo mwenyewe ukiwa wewe mtanzania halisi (usiwe mtanzania feki)wa mambo ya magamba na sumu, ni mpishi mzuri na anae jali kazi yake kiwakati, pia asante mr.muhidin issa, kwamba na huyo mpishi anaalikwa mpaka kwenye hafla za taifa sema hamjui tu nyie wengine,freind junior, istanbul,TUR
ReplyDeleteduh huyu mzee bado yu hai??? Allah akbar, lakini ALI MAPILAU noma pia
ReplyDeleteHicho chakula ni kimoto na sio rahisi kupata maradhi ya yanayosababishwa na uchafu. Pia biriani na pilau huwa inapikwa kwa kutumia viungo vingi (spices) ambazo huwa ni dawa pekee kama vile tangawizi, kitunguu maji na thomu, hiliki, mdalasini, uzile, pilipili manga. Pia huwa kuna salad nzuri ambayo hujaa vitunguu maji na malimau na ndimu. Ni chakula bora na kina kinga nyingi. Mdau CT, USA.
ReplyDeleteAli Mapilau mzee wa upanga ndo kiboko ya wapishi wa shughuli Dar nzima
ReplyDeleteSaidi Bajia Anapatikana mitaa ya Rufiji na Nyamwezi Karikoo...Ukimuulizia Humkosi.... Jamaa Mashallah Msosi wake Lazima Ujirambe....Thanks Mdau Kwa Ku Post Picha hii,hakika nina ubao kinoma sasa especially biriani la TZ likipikwa na mtaalam kama saidi bajia...
ReplyDeleteHouston,Tx
yupo wapi huyu mzee details please
ReplyDeletemichuzi huwa unaweka na kontact bwana , sasa tutampataje ?
ReplyDeleteKila kazi ina fani yake na taratibu zake:- kuhusu chakula/mlo Usafi ni
ReplyDeletemisingi wa kutekeleza wadhifa huo. kwa hiyo kila kilicho usika na mapishi lazima liwe na kiwango ikubwa cha usafi usafi usafi hadi mwandalizi na mkaribishaji aandae kwa usafi.
Hii pilau na biriani ikiwa sufuria limechakaa ndio linapika vizuri. Mbona mahotelini mafrying pen wanaonesha kwenye TV zile zilizochakaa ndizo zinazopika vizuri. Ulizani ma chef watawaambia. Huyo anayesema chafu kwao alikotoka vijijini sufuria au chungu cha ugari wa jana kinakoshwa leo ili upikwe ugari mwingine.
ReplyDeleteAchane nao wapata leo, chips vumbi ndio chakula chao tarararara.
Saidi Bajia tunamfagilia. Chakula cha kula watu 300 - 400 bila ya kumwita yeye mtakula ile pilau ya udongo mwekundu wanaopika ma-caterer wa mjini.
Watuachie pilau na biriani yetu hata likiwa sufuria chafu wenyewe tunafaidi.
huyu mzee anapatika mtaa wa muhoro na nyamwezi. kariakoo. wewe ulizia kwa saidi bajia tuu utaelekezwa. au fika msikiti wa makonde mtaa wa nyamwezi muulizie pale utaelekezwa. keep it up babu saidi
ReplyDeleteMWANANYAMALA TUNA MTU ANAITWA JOLIJO NAE HAFAI KTK MAPISHI.....
ReplyDeleteHeshima ma taadhima kwa SHEHE SAIDI huyu bwana ndiye alikuwa mpishi na msimamiaji wa shuguli ya harusi ya baba yangu ilofanyika tabora kabla ya miaka 30 ilopita na ni maarufu sana katika mikoa ya bara mwanza mpaka bukoba naukisafiri naye utastarehe maana hata na taarabu na sumsumiya anaimba
ReplyDeleteMdau wa May 16 09:21:00 AM 2011 Tarararara umenichekesha kweli! pilau nyekunduuuuu kama imetiwa dongo la kimasai! kwanza pilau raha yake utie viungo vizima vizima pilau wa kusaga viungo ya watu wa BARA A.K.A MRIMA huko wamepapia hawajui kupika pilau viungo vinasangwa nakwambia KARAHA TUPU ! kibaya viugno vya kusagwa kabisa havina harufu yote imeishia kwa muuza duka ! watuachie wenyewe hiyo pilau babu! Saidi Bajia kaza mdundo! na mwengine Mzee Ali Mapilau wa Tambaza pale mtaa wa Mindu nae MAshaALLAh hajambo !
ReplyDeleteHaya Kaka Michuzi Ahsante!
nadhani hiyo siyo pilau watu hajaiangalia vizuri hiyo ni jama rost iliyochonganywa na viazi inarangi safi sana asante kaka michuzi kwa kuposti hii wengine tunashiba kwa macho
ReplyDeleteWatu wengine biriani wanaiona kwenye sinia imeshapakuliwa. Hapo ukimpata Saidi umkabidhi mchele wa basmati halafu unampa na ration yako (asilimia ya mchele na nyama) ukiipiga 50-50 inakua ndio mambo tonge nyama.
ReplyDeleteAnkal, nimemtafuta Said Bajia sanaa. Naomba contact zake nina shughuli June. pleasee.
ReplyDeleteCate
Asalam aleykum vp hali zenu jamani nashukuruni sana kwa kujai kazi yangu tupo KARIAKOO mtaa wa MUHORO ST NA CONGO na karibu na msikiti wa makonde na tunapokea oda mbalimbali mnakaribishwa sana
ReplyDeletenapatikana kwa namba zifuatazo
0654 215213
0658 358661
0784 358661
AHSANTENI SANA NA NAWATAKIA KILA LA KHERI